Ni nini mapenzi ya Mungu na tunaijuaje?
Kwa hiyo, ndugu zangu nawasihi kwa rehema zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana. Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuze kwa kufanya mpya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na ukamilifu.
Lengo la Warumi 12:1-2 ni kuwa maisha yote yatakuwa “ibada ya kiroho.” Mstari 1, “Itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana.” Lengo la uhai wote wa mwanadamu machoni pa Mungu ni kuwa Kristo akafanywe mwenye thamani vile alivyo. Kuabudu kunamaanisha kutumia mawazo na moyo na miili yetu kuonyesha thamani ya Mungu ni vile alivyo kwa ajili yetu katika Yesu. Kuna njia ya kuishi—njia ya kupenda—inayofanya hiyo. Kuna njia ya kufanya kazi yako ambayo inaonyesha thamani ya kweli ya Mungu. Kama huwezi kuipata, basi inafaa ubadilishe kazi. Ama inaweza maanisha pia kwamba mstari wa 2 haufanyi kazi kwa kiwango inafaa iwe inafanya.
Mstari wa 2 ni jibu la Paulo ya vile tunaweza kugeuza maisha yote kuwa ibada. Lazima tufanywe upya. Sio tu tabia zetu za nje, bali vile tunavyohisi na kuwaza—mawazo yetu. Mstari 2: “Mgeuze kwa kufanywa upya nia zenu.”
Kuwa Yule uliye
Wanaoamini Yesu Kristo ni viumbe vipya ambao wamenunuliwa tayari katika Kristo. “Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya,” Lakini sasa lazima tufanyike wale tulivyo “Ondoeni chachu ya kale ili mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu.” (I Wakorintho 5:7)
Nanyi mmeva utu upya unaofanya katika ufahamu sawasawa na mfano wa Mwamba wake.” (Wakolosai 3:10) Mmefanya wapya ndani ya Kristo; na sasa mnafanywa upya siku baada ya siku. Hiyo ndiyo tuliyoyaangazia wiki iliyopita.
Sasa tunaangazia sehemu ya mwisho ya mstari wa 2, uitwayo, lengo la wazo lililiofanywa upya: “Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgheuze kwqa kufanywa upya ni zenu, [Huu hapa ndilo lengo] ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema yanayopendeza machoni pake na ukamilifu.” Basi leo tunaangazia juu ya neno “mapenzi ya Mungu” na vile tunayahakikisha.
Mapenzi mbili ya Mungu
Kuna maana mbili wazi na pia tofauti ya neno “mapenzi ya Mungu” katika Bibilia. Tunastahili kuyajua na kujua ni gani inatumiwa hapa katika Warumi 12:2. Yamkini, kujua tofauti ya maana hizi mbili ya “mapenzi ya Mungu” ni muhimi kwa kufahamu mojawapo ya vitu vikuu na vitu vya kushangaza sana katika Bibilia yote, vinavyoitwa, kuwa Mungu ni mkuu kuliko vyote na bado hukubaliana na baadhi ya vitu alivyothibitisha vifanyike. Kusema, anakataza baadhi ya vitu anavyovileta. Na anaamrisha kusema, anakataza baadhi ya vitu anavyovileta. Na anaamrisha vitu vingine anavyovizuia. Ama kuiweka kwa wazi zaidi: Mungu anapendezwa na matukio mnengine kwa njia mmoja na hapendezwi na nyingine kwa njia nyingine.
1. Mapenzi ya Mungu ya Kukiri, ama ya Ukuu.
Wacha tuone sehemu ya andiko ambazo zinatufanya tufikirie kwa njia hii. Kwanza zingatia sehemu ambazo zinaongea kuhusu “mapenzi ya Mungu” kama utawala wake kuu juu ya yote yanayopita. Mojawapo ya iliyo wazi sana ni vile Yesu aliongea juu ya mapenzi ya Mungu kule Gethsemane alipokuwa akiomba. Alisema katika Mathayo 26:39, “Baba yangu, kama inawezekana kikombe hiki kiniepuke, lakini sasa kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.” Je Mapenzi ya Mungu yamaanisha nini katika mstari huu? Yamaanisha mpango mkuu wa Mungu ambao utafanyika katika masaa yajayo. Unakumbuka vile Matendo 4:27-28 inasema haya: ‘Ni kweli Herode na Pontio Pilato pamoja na Waisraeli, walikusanyika katika Injili huu dhidi ya Mwanao Yesu uliyemtia mafuta. Wao wakafanya yale ambayo uweza wako na mapenzi yako yamekusudia yatokee tangu zamani.” Sasa “mapenzi ya Mungu” ilikuwa Yesu afe. Huu ndio ulikuwa mpango wake, na amri yake. Haungeweza kuibadilishwa na Yesu alijisalimisha na kusema, “Huu hapa ni ombi langu, lakini fanya yanayofaa kufanyika.” Hiyo ndiyo mapenzi kuu ya Mungu.
Na usikose jambo muhimu sana hapa kuwa inajuumlisha dhambi za mwanadamu. Herode Pilato walinzi, viongozi wa kiyahudi—wote walitenda dhambi kwa kutimiza mapenzi ya Mungu kuwa mwanawe asulubishwe (Isaya 53:10) Basi kuwa wazi kabisa kwa hii: Mapenzi ya MUngu huja kupita mambo mengine ambayo anayachukia.
Huu hapa ni mfano kutoka Petero wa kwanza. Katika 1 Petero 3:17 Petero anaandika, “kwa maana ni afadhali kupata mateso kwa ajili ya kutenda mema kama kuteseka huko ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kuteseka kwa kutenda maovu.” Kwa maneno mengine, inaweza kuwa mapenzi ya Mungu kuwa Wakristo wateseke kwa sababu ya kutenda wema. Anayo mawazoni mwake mateso. Lakini kuteseka kwa Wakristo ambao hawastahili kuteswa, ni dhambi. Basi tena, Mungu saa zingine Mungu hupenda kuwa matukio yaje yaliyojumulisha dhambi.
Paulo anapeana neno ya kujumulisha na ya kufagilia juu ya ukweli hii katika Waefeso 1:11 “Katika Kristo sisi nasi tumepata urithi, tukisha kuchaguliwa sawasawa na kusudi la Mungu, Yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na mapenzi yake.” Mapenzi ya Mungu ni uongozi wake kiungu juu ya yote yanayo kuja kutimia. Na kuna sehemu nyingine nyingi katika Bibilia zinazofundisha kwamba upeanaji wa Mungu juu ya dunia ni mbingu unaendelea hadi mpaka kwa mambo ya umbile na kauli ndogo za binadamu. “Lakini hakuna hata shomoro mmoja wao atakayeanguka pasipo Baba yenu kujua (Mathayo 10:29). “ Kura hupigwa katika kufunika, lakini kila uamuzi wake hutoka kwa BWANA” (Methali 16:33) “Mipango ya moyoni ni ya mwanadamuj, bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana.” (Methali 16:1). “Moyo wa mfalme uko katika mkono wa Bwana, humuongoza kama mkondo wa maji, popote apendapo” (Methali 21:1).
Hiyo ndiyo maana ya kwanza ya mapenzi ya Mungu: ni uongozi mkuu wa Mungu juu ya vitu vyote. Tutaita huu mapenzi yake kuu ama “mapenzi yake ya kuamrisha.” Hayawezi kuharibiwa. Lazima yatimie. “Hufanya kama atakavyo kwa majeshi ya mbinguni na kwa mataifa ya dunia. Hakuna anayeweza kuuzuia mkono wake au kumwambia, “Umefanya nini Wewe?” (Danieli 4:35)
2. Mapenzi ya Mungu ya kuamrisha
Sasa maana nyingine ya “mapenzi ya Mungu” katika Bibilia ni ile tunaweza kuita mapenzi yake ya kuamrisha. “Mapenzi yake ni yale anatuamrisha kuyatenda. Hii ndio mapenzi yake ambayo tunaweza kukataa ama kosa kutenda. Kwa mfano, Yesu alisema, “Si kila mtu aniambiaye Bwana, Bwana atakeyeingia katika Ufalme wa Mbinguni bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye Mbinguni.” Si wote wataingia katika Ufalme wa Mbinguni.” Kwa nini? Kwa sababu si wote wanafanya mapenzi ya Mungu.
Paulo anasema katika I Wathesolanika 4:3, “Kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu ninyi muwe watakatifu, ili kwamba mjiepushe na usherati.” Hapa tuko na hali ya pekee juu ya yale Mungu anatuimarisha kwayo: utakatifu, utakaso, uadilifu katika hali ya ngono. Haya ni mapenzi yake ya kuamrisha. Lakini, lo, wengi hawatii.
Halafu Paulo anasema katika I Wathesolanika 5:18,” Shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.” Hapo pia ni hali ya pekee juu ya mapenzi yake ya kuamrisha: Shukrani kwa kila jambo. Lakini wengi hawatendi mapenzi haya ya Mungu.
Mfano mwingine mmoja zaidi: “Nao ulimwengu unapita pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele.” (1 Yohana 2:17). Si wote wadumu milele. Mapenzi ya Mungu, katika hali hii, huwa mara nyingi hayatendeki.
Basi natamatisha kutoka kwa haya na sehemu zingine nyingi ya Bibilia kuwa kuna njia ya kuongea juu ya mapenzi ya mungu. Yote ni kweli, na ya muhimu kuelewa na kuyaamini. Moja tunaita mapenzi ya Mungu kukiri (ama mapenzi yake ya ukuu) na nyingine tunaita Mapenzi ya Mungu ya kuamrisha. Mapenzi yake ya kukiri yanakuja kutimia ama tusipoamini. Mapenzi yake ya kuamrisha yanaweza kuharibiwa na hukubaliwa kila siku.
Thamani ya Kweli hii
Kabla nilinganishe hii na Warumi 12:2 wacha nitaje juu ya vile ukweli hii miwili ni ya thamani. Yote yanalingana na hitaji ya ndani tulio nalo sisi sote wakati tumejeruhiwa kwa ndani ama wakati tumekumbwa na hasara kuu. Kwa njia moja, tunahitaji hakikisho kwamba Mungu yu ushukani na hivyo basi anaweza kufanya uchungu wangu wote na kupoteza kwangu kwa pamoja kwa ajili ya wema wangu na kwa wema wa wale wanaompenda. Kwa njia nyingine, yafaa tujue kuwa Mungu anasikia yale tunayosikia pamoja nasi na hafurahii katika dhambi na machungu kati na kwao wenyewe. Haya mahitaji mawili yanalingana na mapenzi ya Mungu ya kukiri na kuamrisha.
Kwa mfano kama ulidhulumiwa vibaya kama mtoto, na mtu akuulize, “Je unafikiri hiyo ilikuwa mapenzi ya Mungu?” Uko na njia sasa ya kupata ufahamu wa Bibilia katka hii, na upeane jibu isiyo kinyume na Bibilia. Unaweza sema, “La haikuwa mapenzi ya Mungu; kwa sababu anaamrisha wanadamu kutodhulumu, lakini kupendana. Udhalimu ulivunja amri yake na hivyo kufanya moyo wake kuwa na hasira na huzuni (Marko 3:5). Lakini katika njia nyingine, ndio ilikuwa mapenzi ya Mungu (mapenzi yake ya ukuu), Kwa sababu kuna mamia ya njia angeuzuilia. Lakini kwa sababu ambazo sielewi sana, hakuuzuilia.
Na yanayoambatana na mapenzi haya mawili ni mambo mawili unayohitaji katika hali hii. Moja ni Mungu mwenye nguvu na makuu ya kutosha kuubadilisha kwa wema; na nyingine ni Mungu aliye na uwezo ya kuhisi vile unavyohisi. Kwa upande mwingine, Kristo ni Mfalme mkuu, na hakuna kinachofanyika ila tu mapenzi yake (Mathayo 28:18) Tena, Kristo ni kuhani mkuu mwenye rehema anayeweza kuchukuliana na sisi katika udhaifu na uchungu wetu (Waebrania 4:15). Roho mtakatifu hututawala na kushinda dhambi zetu anapopenda (Yohana 1:13; Warumi 9:15-16), na akijiruhusu kuzimwa na akahuzunishwa na kukasirishwa alipopenda (Waefeso 4:30; 1 Wathesolanika 5:19). Mapenzi yake ya ukuu hauna pingamizi, na mapenzi yake ya kuamrisha yaweza kuharibiwa vibaya.
Tunahitaji ukweli hii yote—ufahamu huu wote kwa mapenzi ya Mungu—si tu kuleta ufahamu kutoka kwa Bibilia, bali pia kushikilia sana kwa mateso katika Mungu.
Mapenzi gani yanaongelewa katika warumi 12:2?
Sasa, ni gani kati ya haya yamemaanishwa katika Warumi 12:2, “Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuze kwa kufanywa mpya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na ukamilifu. Jibu hakika ni kwamba Paulo anaongea juu ya mapenzi ya Mungu ya kuamrisha. Nasema hili kwa sababu zaidi ya mbili. Mungu hakusudii tujue mapenzi yake ya ukuu mbele ya wakati.” “Mambo ya siri ni ya BWANA Mungu wetu, bali yaliyofunuliwa ni yetu.” (Kumbukumbu la Torati 29:29). Kama unataka kujua mambo ya usoni ya mapenzi ya Mungu ya kukiri, huhitaji wazo lililofanywa mpya, unahitaji mpira wa chembe. Hii haiitwi kufanywa upya na kutii; inaitwa uungu na kutabiriwa.
Sababu nasema mapenzi ya Mungu katika Warumi 12:2 ni mapenzi ya Mungu ya kuamrisha na si ya kukiri ni kuwa tamshi “ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha” inaonyesha kuwa inafaa tukubali mapenzi ya Mungu na hatimaye kwa utiifu tuyatende. Lakini, yamkini hatufai tukubali dhambi ama tutende dhambi, ingawa ni sehemu ya mapenzi ya Mungu ya ukuu. Maana ya Paulo katika Warumi 12:2 limenukuliwa kwa njia ambayo ni karibu sawa katika Waebrania 5:14, ambayo inasema, Llakini chakula kigumu ni kwa ajili ya watu wazima, ambao kwa kujizoeza wamejifunza kupambanua kati ya mema na mabaya.” (tazama ufananisho mwingine katika Wafilipi 1:9-11). Hilo ndilo lengo la mstari huu “Si kufafanua mapenzi ya Mungu ya siri ambayo anapanga kutimiliza, lakini kupambanua mapenzi ya Mungu yaliyodhihirishwa ambayo yanatupasa tuyatende.
Hatua tatu ya kujua na kutenda mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa
Kuna hatua tatu ya kujua kufanya mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa, hiyo ni kusema, mapenzi yake ya kuamrisha; na hayo yote yanahitaji moyo uliofanywa upya ulio na upambanuzi uliopeanwa na Roho mtakatifu tulio ongea juu yake wakati uliopita.
Hatua ya kwanza
Kwanza, mapenzi ya Mungu ya kuamrisha imefunuliwa kwa nguvu ya kutosha na ya mwisho katika Bibilia pekee. Na tunahitaji moyo uliofanywa upya ili kuelewa na kukumbatia yale Mungu anatuamuru katika Andiko. Pasipo Moyo uliofanywa upya, tutaharibu maandiko ili kukwepa amri yao muhimu ya kujinyima, na upendo na usafi na utosheleshaji mkuu katika Kristo pekee. Mapenzi ya Mungu ya kuamrisha yenye nguvu yapatikana tu katika Bibilia. Paulo anasema kuwa maandiko yamevuviwa na Mungu na yanafanya Mkristo awe kamili, aliyekamilishwa ili apate kutenda kila kazi njema. (2 Timotheo 3:16) Si tu baadhi ya kazi nzuri. “Kila kazi njema.” Lo, ni bidii na muda na ukakamavu gani Wakristo wanafaa kuwa nayo kwa kutafakari neno la Mungu lililoandikwa.
Hatua ya pili
Hatua ya pili ya mapenzi ya Mungu ya kuamarisha ni vile tunautumia ukweli wa Bibilia katika hali mbaya ambayo yaweza kuwa yameelezwa kinaga ubaga ama kutoelezwa katika Bibilia. Bibilia haikuambii ni mtu wa aina gani inafaa uoe, ama ni gari gani unastahili kuliendesha, ama kama unaweza kumiliki nyumba, pahali pa kujistarehesha, aina ya huduma ya simu ya rununu ya kununua, ama aina ya maji ya machungwa ya kunywa. Ama aina ya hatua ya kuchukua.
Kile cha muhimu ni kuwa tuwe na moyo uliofanywa upya, ambao umetengenezwa na kudhibitiwa na mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa katika Bibilia, ili tuweze kuona na kupekua hali yote yanayofaa na moyo wa Kristo na kupambanua yale Mungu anatuita tukayafanye. Hii ni tofauti sana na kujaribu kila mara kusikia sauti ya Mungu akisema fanya hiki ama kile. Watu wanaojaribu kuishi maisha yao kwa kusikia sauti zisizoambatana na Warumi 12:2.
Kuna tofauti ya kilimwengu kati ya kuomba na kutafuta kufanywa upya kwa wazo ambalo hupambanua jinsi ya kutumia Neno la Mungu, kwa upande mwingine, mazoea ya kuomba Mungu ili akupatie ufunuo mpya ya kitu cha kutenda, kwa upande mwingine. Uungu hauhitaji kufanywa upya. Lengo la Mungu ni wazo jipya, njia mpya ya kufikiria na uamuzi, si tu habari mpya. Lengo lake ni kuwa tufanywe upya, tutakaswe, tuwekwe huru na ukweli wa neno lake lililofunuliwa (Yohana 8:32; 17:17). Basi hatua ya pili ya Mapenzi ya Mungu ya kuamrisha ni uwezo wa kupambana kwa maandiko na pia hali mpya katika maisha kwa njia ya kufanywa upya mawazoni.
Hatua ya tatu
Ya mwisho, hatua ya tatu ya mapenzi ya Mungu ya kuamrisha ni sehemu kubwa ya kuishi pahali hakuna ufahamu wa kuonekana kabla tuchukue hatua. Namaanisha kusema asilimia 95 ya matendo yako hufikirii kabla ya kuyatenda. Ni kusema, wingi wa fikira zako, matendo yako na mienendo zako ni ya ghafla. Yatokana na yale yaliyo ndani. Yesu alisema, Yesu alisema, “Kwa maana kinywa cha mtu huyanena yale yaliyoujaza moyo wake. Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina ya mambo mema yaliyo hifadhiwa ndani yake. Lakini nawaambia, katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu kuhusu kila neno lisilo kuwa na maana alilonena” (Mathayo 12:34-36).
Kwa nini naliita hili sehemu ya mapenzi ya Mungu ya kuamrisha? Kwa sababu moja. Kwa sababu Mungu anaamuru vitu kama: Usikasirike. Usijawe na Kiburi. Usiwe na tamaa. Usiwe na hila. Usiwe na wivu. Usiwe na chuki. Na hakuna kati ya matendo haya ambayo yanapangwa kabla. Hasira, kiburi, tamaa, hila, wivu, chuki—yote yainuka kutoka kwa roho bila kufahamu ama kusudia . Na tunakuwa na hatia kwa sababu yao. Yanavunja sheria za Mungu.
Si ni wazi basi kwamba kuna jukumu moja kuu katika maisha ya Mkristo: Ubadilishwe kwa kufanywa upya mawazoni mwako. Tunahitaji moyo na mawazo mapya. Ufanye mti kuwa mzuri nayo matunda yake yatakuwa mazuri (Mathayo 12:33). Ndiyo changamoto kuu—Mungu anakuita kwayo. Huwezi kufanya kivyako. Unahitaji Kristo, ambaye alifilia dhambi zako. Na mnahitaji Roho mtakatifu kuwaeleza kwa ukweli wa Kristo unaoinua na kufanya kwako katika unyenyekevu ukumbatiayo ukweli.
Jisalimishe kwa hii. Jitumbukize kwa neno la Mungu lililoandikwa; jaza mawazo yako nayo. Na uombe kwamba Roho wa Kristo akufanye upya kwa Kiasi kuwa mabara yatakuwa mema, yaliyokubalika na kamilifu—mapenzi ya Mungu.