Ni nini kinachotendeka katika kuzaliwa upya? sehemu ya 1
Basi palikuwa na mtu mmoja wa mafarisayo jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. Huyu alimjia usiku akamwambia.’Rabii twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu,kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe.isipokuwa munu yu pamoja naye.” Yesu akajibu,”Akamwambia Amini, amini na kuambia mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” Nikodemo akamwambia, “Awezaje mtu kuzaliwa akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mara ya pili akazaliwa?” Yesu akajibu,”Amin Amin nakuambiamtu asipozaliwa kwa maji na kwa roho hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa roho ni roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, hamna budi kuzaliwa mara ya pili.” Upepo huvuma upendako na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kule mtu aliyezaliwa kwa Roho.” Nikodemo akajibu akamwambia, Yawezaje kuwa mambo haya?” Yesu akajibu, akamwambia,”Je! Wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu?”
Tumeuanzisha mfululizo wa ujumbe wa kuzaliwa upya. Yesu alimwambia Nikodemo katika Yohana 3:3 “Amin Amin na kuambia mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” Alikuwa akinenea na sisi sote aliposema haya. Nikodemo hakuwa mtu maalum. Wewe na mimi sharti kuzaliwa mara ya pili,la sivyo hatutaona ufalme wa Mungu. Kumaanisha hatutaokoka; hatutakuwa sehemu ya familia ya Mungu wala hatutaenda Mbinguni bali jehanamu.
Nikodemo alikuwa mmoja wa wafarisayo, kiongozi wa kichini wa wayahudi.Yesu akawaambia katika Mathayo 23:15 na 33. “Ole wenu waandishi na mafarisayo wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu: na kiisha kufanyika mnamfanya kuwa mwana jehanamu mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe….Enyi nyoka,wana wa majoka,mtaikimbiaje hukumu wa jehanamu?”Sasa somo tuliomaliza si somo la kufikiria, ni ya msingi.umilele huangikwa kwenye mizani tunaponena kuhusu kuzaliwa upya.Mpaka mtu azaliwe mara ya pili hawezi kuona ufalme wa Mungu.”
Kuzaliwa Upya Hakutulizi
Kwenye ujumbe wa kwanza wakati uliopita tuliangazia kuhusu somo hili na baadhi ya maswali tutakayouliza. Swali la leo ni:Ni nini kinachofanyika katika kuzaliwa upya? Kabla ya kujibu swali hili, hebu nitaje kuhusika kwangu kuhusu njia jumbe hizi zitakavyo sikizwa. Ninajua kuwa msururu mafunzo ya jumbe hizi hazitafanya wengi wenu kutulia-Kama vile maneno ya Yesu haufanyi wengi wetu watulie tunapoichukua kwa mkazo. Kuna zaidi ya udhuru tatu:
1) Kwa Sababu ya hali yetu ya kukosa Tumaini
Mafunzo ya Yesu kuhusu kuzaliwa upya yanatuvamia katika hali zetu za kukosa matumaini kiroho, kimaadili na hali ya kisheria kando na neema ya Mungu inayohuisha. Kabla ya kuzaliwa upya kutendeka kwetu tumekufa kiroho. Tumejawa uasi na kukosa maadili. Vile vile tuna hatia mbele za sheria na chini ghadhabu ya Mungu. Yesu anapotuambia kuwa sharti tuzaliwe mara ya pili anatueleza kuwa hali yetu ya sasa hauajibiki kwa kukosa tumaini, uharibifu na hatia. Kando na neema kuu kwa maisha yetu hatutaki kusikiza haya sisi wenyewe. Basi haitulizi Yesu anapotuambia lazima tuzaliwe mara ya pili.
2) Kwa Sababu hatuwezi kusababisha kuzaliwa upya
Mafunzo kuhusu kuzaliwa upya hayatulizi kwa kuwa yanamaanisha jambo linalofanyika kwetu si tunalofanya wenyewe. Yohana 1:13 linasisitiza zaidi. Hii ni kuwa watoto wa Mungu wale ambao “waliozaliwa si kwa damu wala si kwa mapenzi ya mwili wala si kwa mapenzi ya mtu bali kwa Mungu.”Petero anatilia mkazo jambo lilo hilo. “Ahimidiwe mungu Baba wa Bwana wetu Yesu! Ambaye kwa neema zake nyingi alituzoa mara ya pili.” 1 Petero 1:3. Sisi hatufanyi kuzaliwa upya. Yaani kuzaliwa upya hakupo mikononi mwetu wala si kwa udhabiti wetu. Sasa inatuingilia katika ukosefu wetu wa tumaini na kumtegemea mtu aliye nje ya nafsi zetu.
Hii haiwezi kutuliza. Tumeambiwa ya kwamba hatuwezi kuona ufalme wa Mungu kama hatutazaliwa mara ya pili.Pia tumeambiwa kuwa hatuwezi fanya sisi wenyewe kuzaliwa mara ya pili.Hii haitulizi.
3) Kwa sababu uhuru kamili ya Mungu unatuvamia tu:
Sababu ya tatu katika mafunzo ya Yesu kuhusu kuzaliwa upya kutotuliza ni kwamba inatuvamia na uhuru kamili ya Mungu. Mbali na Mungu, tumekufa kiroho katika ubinafsi na uasi wetu,kiasili sisi ni wana wa ghadhabu Wafeso 2:3 Kuasi kwetu ni kuingia zaidi ya kutogundua wala kutamani Kristo katika Injili (2. Wakorintho 4:4) Kama tutazaliwa mara ya pili utategemea uamuzi wa Mungu.Uamuzi wake kutaweka hai hautategemea sisi tuliokufa kiroho tunavyofanya lakini tunachotenda kitakuwa matokeo ya kutufanya hai.Kwa wengi mwanzoni haitulizi.
Tumaini langu kuthibitika na kuokoka bali si kutotulia tu
Ninavyoanza fumo hili najua vile mafundisho haya hayatatuliza kuhusu kuzaliwa upya. Na lo! Kiasi gani nahitaji kuwa mwangalifu. Sitaki nitie wasi wasi usio na maana kwa nafsi thabiti.;sitaki niwape tumaini ya uwongo kwa wale waliochanganyisha maadili au dini kwa maisha ya kiroho. Nawasihi mniombee najihisi kwamba nazichukua nafsi za milele mikononi mwangu siku hizi. Ilhali nafahamu kwamba mimi sina nguvu ndani yangu kuwapa uzima lakini Mungu anaweza. Nina matumaini kwamba atafanya anavyosema katika Waefeso 2:4-5 lakini Mungu kwa kuwa ni mwingi wa rehema kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda,hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu,alituhusisha pamoja na kristo-tumeokolewa kwa neema.” Mungu angependa kudhihirisha wingi wa neema yake iletayo uzima mahali Yesu ameinuliwa katika kweli. Ndio tumaini langu: Kwamba funzo hili halitakutuliza tu lakini kukuthibiti na kukuokoa
Nini kinafanyika katika kuzaliwa upya?
Tulitazame sasa swali hili: Nini hufanyika katika kuzaliwa upya?Nitajaribu kuweka jibu katika maelezo matatu: mawili ya asilani tutayafafanua leo na la tatu tutashughulikia (Mungu akipenda) wiki ijayo. 1) Kinachofanyika kwa kuzaliwa upya si kupata dini mpya bali uzima upya. 2)kinachofanyika katika kuzaliwa upya si kuonyesha uungu ndani ya Kristo bali kushuhudia uungu ndani yako. 3) yanayotendeka katika kuzaliwa upya si kustawisha maumbile yako ya asilia bali kuumbwa kwa ubinadamu wa asilia mpya -Asili ambayo kwa hakika ni wewe na imesamehewa,kusafishwa na ni asilia ambayo kweli ni mpya na inaundwa kwa ukaaji wa roho wa Mungu.Hebu tuyafafanue moja baada ya nyingine.
1) Uzima mpya,si dini mpya.
Kinachotendeka katika kuzaliwa upya si kupata dini mpya bali uzima mpya.soma nami mistari ya kwanza tatu ya Yohana 3: “Basi palikuwa na mtu mmoja wa mafarisayo jina lake Nikodemo mkuu wa wayahudi.Huyu alimjia Yesu usiku moja akamwambia ,“Rabi twajua ya kuwa u mwalimu,umetoka kwa Mungu,kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya ishara hizi uzifanyazo wewe , isipokuwa Mungu yu pamoja naye. Yesu akajibu akamwambia “Amin Amin nakuambia mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona mfalme wa Mungu.”
Yohana anahakikisha kuwa tunafahamu Nikodemo kama mfarisayo aidha mkuu wa Wayahudi. Wafarisayo ndio walikuwa wataua wa dini kuliko wayahudi wote. Kwa lili Yesu anamwambia (Katika Mstari wa 3) “amin amin nakuambia mtu asipolzaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” Zaidi kibinafsi mstari wa 7:”Huna budi kuzaliwa mara ya pili.” Jambo la Kwanza muhimu la Yohana ni :Katika kila kitu cha Nikodemo:Dini,uwalimu wake wa ufarisayo,heshima utiifu wa sheria-haviwezi kubadilisha kuhitaji kwa kuzaliwa upya.
Kile Nikodemo anahitaji pamoja na wewe na mimi si dini bali uzima. Sababu ya kutaja kuzaliwa upya ni uzao huu unaleta uzima mpya ulimwenguni.Kwa hisia hakika Nikodemo yu hai,anapumua,uweza kufikiri,ana hisia,ana vitendo ni mwanadamu aliyeumbwa kwa sura ya Mungu. Lakini kwa dhibitisho Yesu anafikiria amekufa. Hakuna maisha ya kiroho kwa Nikodemo kiroho hajazaliwa. Anahitaji uzima wala si kazi ya dini wala nguvu na uwezo wa dini ziada.Tayari anazo zakutosha.
Je,wakumbuka kile Yesu alisema katika Luka 9:60 kwa Yule aliyekataa kumfuata Yesu ili aende akamzike baba yake? “Waache wafu wawazike wafu wao.” Kumaanisha kuwa kuna wale wliokufa kimwili wanaohitaji kuzikwa na kuna wafu kiroho ambao wapaswa kuwazika. Kwa maneno mengine: Yesu aliwafikiria kama watu ambao watembea wakiwa wazima dhahiri bali ni wafu. Katika mfano wa mwana mpotevu baba anasema “Kwa kuwa mwanangu alikuwa amekufa na amefufuka.” (Luka 15-24)
Nikodemo alikuwa ahitaji dini lakini uzima wa Kiroho.Kinachotendeka kwa kuzaliwa upya ni kwamba uzima ambao haukuwa mwanzo huja.Uzima mpya hufanyika katika kuzaliwa upya. Hii si kazi ya dini wala heshima wala uamuzi. Hii ni kuja kuwepo kwa uzima. Hii ndiyo njia ya kwanza ya kufafanua kinachofanyika kwenye kuzaliwa upya.
2) Kushuhudia uungu si tu kuonyesha
Kinachotendeka katika kuzaliwa upya si tu kuonyesha uungu ndani ya Yesu bali kushuhudia uungu ndani yako. Katika mstari wa 2, Nikodemo anasema, “Rabi twajua ya kuwa u mwalimu umetoka kwa Mungu, kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya Ishara hizi uzifanyazo isipokuwa Mungu yu pamoja naye.”kwa maneno mengine:Nikodemo anaona ndani ya Yesu tendo la kiungu halisi. Anakubali kuwa yesu ametoka kwa Mungu. Yesu anatenda kazi za Mungu. Yesu hujibu kw akusema,Ningesihi kila mmoja wa palestina angeona ukweli unaona ndani yangu.badala yake anasema ,”Lazima uzaliwe mara ya pili la sivyo hutauona ufalme wa Mungu.”
Kuona ishara na maajabu na kustajabia, kushukuru kazi yake ya miujiza kwamba ametoka kwa Mungu haziwezi kuokoa mtu yeyote. Hii ni moja wapo wa hatari za Ishara na maajabu. Huitaji moyo mpya ili ushangazwe nazo. Yule utu wa kale ulioasi ndiye anayehitajika ili astaajabie ishara na maajabu. Mtu wa kale aliyeasi anapenda kusema kuwa anayetenda kazi ya muijiza ametoka kwa Mungu. Shetani mwenyewe amejua kuwa Yesu ni mwana wa Mungu na anatenda miujiza (Mariko 1:24). Kwa Nikodemo kuniona kama atendaye miujiza aliyetumwa na Mungu si kibali cha kuingia katika ufalme wa Mungu. “Amin amin nakwambia mpaka uzaliwe mara ya pili ndipo utakapoingia kwa ufalme wa Mungu.”
Yaani, kilicho muhimu si tu kudhibitisha tu uungu ndani ya Yesu bali kushuhudia uungu huu ndani yako.Kuzaliwa upya ni ya kiungu si asili.Haihesabiki kwa mambo ambayo hupatikana ulimwenguni. Mstari wa 6 unasisitiza asili ya uungu katika kuzaliwa upya.”Kilichozaliwa na mwili ni mwili na kilichozaliwa na roho ni roho.”Mwili ndiyo tuko kiasili. Roho wa Mungu ni mtu wa kiungu aletaye kuzaliwa upya.Yesu anasema haya tena katika mstari wa 8: “Upepo huvuma upendako,na sauti yake waisikia lakini hujui unakotoka wala unakokwenda,kadhalika na hali yake kile mtu aliyezaliwa kwa Roho.”Roho si sehemu ya ulimwengu asili. Ni zaidi ya asili.Yeye ni wa kiuungu. Kwa hakika ni Mungu.Yeye ndiye kwa karibu huleta kuzaliwa upya.
Sasa Nikodemo, Yesu anamwambia kinachotendeka katika kuzaliwa upya si tu kudhibitisha uungu ndani yangu bali kushuhudia uungu ndani yako. Lazima uzaliwe mara ya pili.Si kwa mfano yoyote ya kiasili bali kwa njia ya kiungu. Mungu roho mtakatifu lazima aje juu yako na kuleta uzima mpya.
Tutachunguza wakati mwingine maneno kwenye mistari wa 5: Amin amin nakuambia mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho huwezi kuungia ufalme wa mungu.” Maji na Roho yana maana gani hapa? Na inatusaidia vipi kufahamu yanayotendeka katika kuzaliwa upya
Yesu ndiye uzima
Tunafunga kwa leo kwa kufanya uunganifu muhimu kati ya kuzaliwa mara ya pili katika roho na kuwa na uzima wa milele kwa imani ndani ya Yesu. Kile ambacho tumeona ni kuwa kinachotendeka kwenye uzao mpya ni kiungu ndani ya Roho mtakatifu aletaye uzima wa kiroho mahali haupatikani.Yesu alisema tena katika Yohana 6:63 Ni Roho ndiyo atiaye uzima ,mwili haufai kitu.
Walakini injli ya Yohana inafafanua jambo jingine vile vile kwa uwazi:Yesu ndiye uzima ambao roho mtakatifu hutupa au tuseme uzima wa kiroho ambao hutupa tu kulingana na uunganifu na Yesu. Hapo ndipo tunashuhudia uzima wa kiroho tena wa kiungu.Yesu alisema katika Yohana 14;6 “mimi ndimi njia,na kweli, na uzima.Mtu haji kwa baba ila kwa njia yangu mimi. Katika Yohana 6;35 alisema “mimi ndimi chakula cha uzima “na katika 20;31 Yohana anasema “lakini hizi zimeaandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye kristo,mwana wa Mungu na kwa kuamini muwe na uzima kwa jina lake.
Hakuna Uzima bila Yesu
Sasa hakuna uzima wa kiroho wala wa milele bila kuunganishwa na Yesu na kumwamini. Tutakuwa na mengi ya kusema kuhusu uhusiano baina ya kuzaliwa upya na kumwamini Yesu. Wacha tuiweke hivi kwa sasa :katika kuzaliwa upya Roho mtakatifu hutuunganisha na Kristo katika muungano ulio hai. Yesu ni uzima.Yesu ni mzabibu patokapo uzima. Sisi ni matawi (Yohana 15:1) kinachotendeka kwa kuzaliwa upya ni maumbile ya kiungu ya uzima wa kiroho mpya,na huumbwa kupitia kuunganishwa na Yesu Kristo.Roho mtakatifu hutuleta kwenye muungano huu muhimu na Kristo ambaye ndiye njia ,kweli na uzima. Hili ndilo lengo la hakika la kinachotendeka katika kuzaliwa upya.
Kwa upande wetu- vile tunavyoshuhudia haya ni kwamba imani kwa Yesu huinuliwa katika mioyo yetu, uzima wa kiroho na imani kwa Yesu yanaja kwa pamoja. Maisha au uzima mpya huwezesha imani na kwamba uzima wa kiroho huinua na kuonyesha imani basi hakuna uzima bila Imani kwa Yesu. Basi haifai kutenganisha kuzaliwa upya na kumwamini Yesu. Upande wa Mungu ni kuwa tumeunganishwa na Kristo katika kuzaliwa upya .Hii ndiyo Roho mtakatifu hutenda. Kwa upande wetu tunashuhudia muungano huu tukiwa tumemwamini Yesu.
Usiwahi Kamwe kutenganisha kuzaliwa upya na kumwamini Yesu
Sikiza vile Yohana anavyoiweka pamoja katika 1 Yohana 5:4 Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu,na huku ndiko kuushinda kuushindako ulimwengu.Kuzaliwa na Mungu ndiyo ufunguo wa ushindi. Imani ni ufunguo wa Ushindi.kwa sababu imani ndiyo njia tunayoshuhudia kuzaliwa na Mungu.
Au sikiza Yohana anavyosema katika 1 Yohana 5:11-12 “Na huu ndio ushuhuda ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele na uzima huu umo katika mwanawe.Yeye aliye naye Mwana,anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.”Basi Yesu anaposema, “Ni Roho atiaye uzima, mwili haufai chochote” Yohana 6:63 na anaposema, “Lazima uzaliwe kwa Roho ili kuwa na uzima ana maana kuwa :Katika kuzaliwa upya Roho mtakatifu kwa njia ya kiungu hutupa uzima wa kiroho mpya kwa kutuunganisha na Kristo kupitia imani. Kwa kuwa Yesu ni Uzima.
Basi usitenganishe misemo hii miwili katika Yohana 3. “Mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” (Mstari 3) na “Amwaminiye Mwana wa Mungu ana uzima wa milele” (Mstari 36)