Asili Yenye Dhambi ya Mwana wa Daudi
Hii ni ujumbe wa sita kati ya msururu saba za ujumbe uitwayo dhambi ya asili na lengo leo ulimwenguni kwa utukufu wa Kristo. Ujumbe huu unaitwa. “asili yenye dhambi ya Mwana wa Daudi.” Jambo ni hili: Ufalme wa Israeli—kwa kuwa Israeli ilikuwa na wafalme—ilitokana na dhambi. Ilikuwa dhambi mbaya kwa watu wa Mungu kumwambia Muumba na Mkombozi wao, “Tunataka kuwa kama mataifa. Hatutaki uwe mfalme wetu. Tunataka mfalme ambaye ni mwanadamu.” Hiyo ni dhambi kuu. Samueli anaiita, katika mstari 17, uovu mkuu. Ingawa, kama Israeli haikuwa na utawala kwa kifalme, Yesu Kristo hangekuja kama Mfalme wa Israeli na Mwana wa Daudi na Mfalme wa wafalme. Lakini utawala wa Kristo wa kifalme juu ya Israeli na juu ya ulimwengu si wazo la kando moyoni mwa Mungu. Halikuwa jibu lisilopangwa kwa dhambi ya Israeli. Ilikuwa sehemu ya mpango wake.
Kwa nini kuufanya kwa njia hii?
Swali letu ni hii: Kama Mungu aliona dhambi hii mbaya ikija na kujua kuwa atairuhusu na hivyo basi akafanya utawala wa kifalme ya Israeli kuwa sehemu ya mpango wake ya kutukuza Kristo kama mfalme wa Wafalme, Kwa nini hakufanya utawala wa kifalme kuwa sehemu ya utawala wa Israeli tangia mwanzo? Kwa nini hakufanya Musa mfalme wa kwanza? Hatimaye Joshua na wengine wengi? Kwa nini kupanga utawala wa kifalme kutoka kwake yeye mwenyewe hapo mwanzo na baadaye kuleta utawala wa kifalme wa mwanadamu katika historia ya Israeli hapo baadaye kupitia dhambi mbaya.
Abrahamu na Utawala wa Kifalme Ujao
Wacha tuanze na hadithi yenyewe. Mungu aliteua Abrahamu kama Baba ya wana wa Israeli. Katika Mwanzo 12 na anamwahidi kwamba kupitia uzao wake watu wote wa ulimwengu watabarikiwa (Mwanzo 12:1-3). Masiya, Yesu Kristo, atakuja kutoka shina hili.
Mojawapo ya vitu vitukiapo kwa Abrahamu ni kuwa anakutana na mtu asiyemjua aitwaye Melchizedeki katika Mwanzo14:18. Anaitwa “kuhani wa Mungu Aliye Juu sana” na “Mfalme wa Salemu.” Jina lake lamaanisha “mfalme wa haki.” Mwandishi wa kitabu cha Waebrania, katika Agano Jipya,anaona Melkizedeki kama mfano, sura ya kabla, ama taswira ya kutangulia ya Kristo, kwa sababu Zaburi 110:4 inasema kuwa mfalme wa kimasiya ajaye pia ni “Kuhani milele, kwa mfano wa Melkizedeki.” Basi Waebrania inasema, “Melkizedeki…ni wa kwanza, kwa tafsiri la jina lake, mfalme wa haki, na halafu yeye ni mfalme wa Salemu, kusema, mfalme wa amani . . . anayefanana na Mwana wa Mungu . . . ” (Waebrania 7:1-3)
Hannah na utawala wa kifalme uujao
Basi kulingana na kusudio la Mungu, Masiya ajaye atakuwa kuhani-mfalme. Uamuzi wa yeye kuwa mfalme haukuja baadaye. Tunaona hii tena katika hadithi ya kuzaliwa na kukabidhiwa kwa Samweli. Mnakumbuka kuwa mamake Hannah alikuwa tasa. Halafu Eli alitabiri kuwa atapata mtoto. Samweli akazaliwa na Hannah anamleta hekaluni na kumkabidhi kwa Bwana. Baadhi ya mambo ya ajabu Hannah asemayo ni haya katika 1 Samweli 2:10—na ukumbuke, hii miongo kabla kuwa na mfalme yeyote katika Israeli (Wakati Samueli amekuwa mtu mkubwa ndipo watu wakamsukuma kuwapa mfalme). Anasema, “wale wampingao Bwana wataharibiwa kabisa. Atapiga radi dhidi yao kutoka mbinguni, Bwana ataihukumu mwisho wa dunia. “atampa nguvu mfalme wake na kutukuza pembe ya mpakwa mafuta wake.”
Musa na utawala wa Kifalme Ujao
Tukirudia Kumbukumbu la Torati 17:14-20 Musa alishapeana maagizo juu ya utawala wa kifalme ikiwa watu walitaka kuenenda katika upande huo. Na Kumbukumbu la Torati 28:36 uliongea juu ya kupelekwa kwa watu katika taifa wasiolijua pamoja na mfalme wao kama wangemuasi Bwana. Basi naamini kuwa yaliyotukia katika 1 Samueli 12 haikuwa mshtuko kwa Mungu. Alijua kuwa atairuhusu. Na Mungu akikusudia kuruhusu kitu, analifanya kwa hekima, si kipumbavu. Basi, dhambi hii mbaya ni sehemu ya lengo kuu ya Mungu kwa utukufu wa Mwanawe.
Vile Utawala wa kifalme ulivyokuja
Wacha tuione vile ilikuja kabla ya kutafakari ni kwa nini angeufanya kwa njia hii. Hoja ya kuwa na mfalme ulianza katika sura ya 8 ya kitabu cha 1 Samueli, lakini tutachukulia kwanza 12. Msatri 8b: BWANA “aliwatoa baba zenu kutoka Misri na kuwakilisha mahali hapa.” Mstari 9 “Lakini wakamsahau Bwana Mungu wao hivyo Mungu akawauza katika mkono wa Sisera, jemedari wa Moabu, ambaye alipigana dhidi yao.” Mstari 10: “Wakamlilia (Wana wa Israeli) Bwana na Kusema. ‘Tumetenda dhambi tumemwacha BWANA na kutumikia Mabaali na Maashtorethi. Lakini sasa tuokoe kutoka katika mikono ya adui zetu, nasi tutakutumikia.” Mstari 11. “Ndipo BWANA akawatumia Yeru-Baali, Baraka, Yeftha na Samueli, naye akawaokoa kutoka katika mikono ya adui zenu kila upande, ili ninyi mpate kukaa salama.
Watu waliukata Utawala wa Kifalme wa Mungu
Lengo la mistari hiyo ni kuonyesha kwamba Mungu alikuwa mwaminifu kama mfalme mwenye uweza. Walipomlilia aliwaokoa. Aliwapa ulinzi. Hilo ndilo jukumu la mfalme-kuwapa watu amani. Na nini jibu lao? Mstari 12. “Lakini nilipomwona yule Nahashi mfalme wa Waamoni anakuja dhidi yenu mliniambia [Samueli]’ Hapana, tunataka mfalme atutawale, hata ingawa BWANA Mungu wenu alikuwa mfalme wenu.”
Unaweza kusikia hali ya kutoamini katika sauti ya Samueli. Mlihitaji mfalme, hata ingawa Bwana Mungu wenu alikuwa mfalme wenu! Samueli atafanyaje? Tayari Bwana alikwisha mwambia katika 1 Samueli 8:7-9, “Sikiliza yale yote watu wanayokuambia, si wewe ambaye wamekukataa, bali wamenikataa mimi kuwa mfalme wao . . . sasa wasikilize, l akini waonye kwa makini na uwafahamishe yale watakayotendewa na mfalme atakayewatawala.”
Dhambi ya kushangaza: “Uovu wenu ni mkuu”
Basi samuelki anasema katika 1 Samueli 12:13b. “Tazameni BWANA amemweka mfalme juu yenu .” Kisha anamwomba Bwana kuwapa ishara kwa ngurumo na mvua, na anasema kuwa dhambi zao ni kama uovu mkuu. Mstari 17: “Je, sasa si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA ili alete ngurumo na mvua. Nanyi mtatambua jambo hili lilivyo baya mlilolifanya mbele za macho ya Bwana mlipoomba mfalme.
Na ili kuhakikisha kwamba hatujakosa kazi takatifu ya Mungu katika uovu huu usio takatifu, Paulo katika Matendo 13:20-22, anauweka wazi kwamba ni Mungu aliyewaapa Israeli mfalme wa Kwanza. “Mungu akawaapa waamuzi mpaka wakati wa nabii Samueli. Ndipo watu wakaomba wapewe mfalme, naye Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi wa kabila ya Benyamini, aliyetawala kwa miaka arobaini. Baada ya kumuondoa Sauli katika ufalme, akawainulia Daudi kuwa mfalme wao.” Tumeona hii ikirudiliwa katika dhambi ya kihistoria ya kushangaza. Mwanadamu aliukusudia kwa uovu, na Mungu akaukusudia kwa wema.
Tunajifunza nini kutoka kwa hii?
Swali basi ni hili. Kama Mungu alishaona dhambi hii ya kushangaza ikija na akajua kuwa atairuhusu na hivyo basi akafanya utawala ya kifalme juu ya Israeli kuwa sehemu ya lengo lake la kutukuza Kristo kama mfalme wa wafalme, kwa nini hakufanya utawala wa kifalme kuwa sehemu ya utawala juu ya Israeli kutokea mwanzo? Kwa nini hakufanya Musa kuwa mfalme wa kwanza? Hatimaye Yoshua na wengine wengi? Kwa nini Mungu alianza na Yeye mwenyewe kama mfalme, hala halafu kuleta ufalme wa kibinadamu katika historia ya Israeli baadaye kupitia dhambi ya kushangaza? Tunajifunza nini kutokana na haya?
Zaidi ya vitu sita.
1) Sisi ni Shingo Nguvu, Waasi na Wasio na Shukrani.
Yafaa tujifunze kutoka kwa hii vile tulivyo na shingo ngumu, waasi na wasio na shukrani. Ndiyo maana 1 Samueli 12 inaanza vile ilivyo kwa kukumbusha watu vile Mungu alivyowakomboa kutoka kwa nchi ya Misri na kuwapa ahadi na halafu baadaye akawaokoa kutoka kwa wafalme waovu. Na kila mara wanamsahau Mungu na kufuata vitu vingine. Hiyo sio tu hadithi ya Israeli. Ni hadithi ya ubinadamu. Ni hadithi kuhusu maisha yako na yangu. Hata ingawa sisi ni Wakristo, hatuna ukakamavu katika upendo wetu kwa Mungu. Tuko na siku ya shukrani na siku zingine isiyo ya shukrani. Na hata siku zetu za shukrani hazina shukrani kwa viwango vinavyohitajika. Hebu fikiria vile utajawa na furaha na shukrani kama moyo wako utauitikia Mungu mwenyewe na zawadi zake elfu kumi kwa kutamani na shukrani ambayo anastahili. Basi Mungu anatupatia taswira yetu katika hadithi kama hii. Anawaruhusu watu wake kusogelea katika aina ya nyakati isiyo na shukrani na ya kuabudiwa kwa miungu ndipo kila kinywa kifungwe na ulimwengu wote watoe habari zao mbele za Mungu (Warumi 3:19)
2) Mungu ni mwaminifu katika jina lake mwenyewe.
Yafaa tujifunze kutoka kwa hii vile Mungu ni mwaminifu kwa jina lake mwenyewe. Tazama mstari 22: “Ilimpendeza BWANA kuwafanya kuwa wake mwenyewe.” Ni nini msingi wa ndani kabisa ya uaminifu wa Mungu? Utiifu wa Jina lake mwenyewe. Ila na shauku lake kwa utukufu wake mwenyewe. Soma mstari huu kwa utaratibu na huku ukitafakari: “Kwa ajili ya jina lake kuu BWANA hatawakataa watu wake.” Haisemi kwa ajili ya “jina lao kuu” bali kwa ajili ya jina lake mwenyewe. Hivyo basi hadithi kama hizi ziko katika Bibilia kutufundisha kwamba njia za Mungu hutawalwa kwa hekima isiyo na kifani ukiongozwa na thamani isiyo na kikomo ya jina lake
3) Neema Zatiririka kwa Wenye Dhambi kupitia Egemeo kuu la Mungu katika Jina Lake.
Yafaa tujifunze kutoka kwa hii vile neema ya ajabu kwa wenye dhambi kama sisi zatiririka kupitia egemeo kuu la Mungu katika Jina lake kati kati mwa dhambi. Tazama taswira ya ajabu katika mistari hii 19-22. “Katika mstari 19, watu wana uoga juu ya dhambi ya kushangaza ambazo wamezitenda dhidi ya Mungu. Wanasema, “Mwombe BWANA Mungu wako, kwa ajili ya watumishi wako ili tusije tukafa, kwa kuwa tumeongeza uovu juu ya dhambi zetu nyingine kwa kuomba mfalme.” Maneno yanayofuata hii ni taswira ya injili ya bure ya neema kwa wenye dhambi Samueli akawajibu (mstari 20), Msiogope mmefanya uovu huu wote.”
Hebu komea hapo na ushangae. “Msiogope, mmefanya uovu huu wote.” Je hiyo ni maandishi ya kosa? Je inafaa iseme, “Muogope; mmefanya uovu huu wote.” Lakini inasema, “Msiogope, mmefanya uovu huu wote.” Hiyo ni neema kamili. Neema ya Mungu inatupeleka katika njia ambayo hatustahili: “Muogope mmefanya uovu huu wote.” Lakini kuliko vile tunavyostahili: “Msiogope mmefanya uovu huu wote.”
Hii yawezekanaje? Ni nini chanzo cha neema hii? Sio sisi! Tumetenda tu uovu. Nini basi? Tayari tumeiona. Mstari 22: Msiogope kwa ajili ya jina lake kuu BWANA hatawakata watu wake.” Egemeo la Mungu kwa ajili ya jina lake ndiyo msingi y a uaminifu wake kwako. Kama Mungu angeliacha egemeo lake kuu kwake mwenyewe, hakungekuwa na neema kwetu sisi. Kama angelisisitisha ukarimu wake wa thamani yetu, hangekuwa na ukarimu kwetu sisi. Sisi ni shingo ngumu, waasi, na wasio na shukrani. Neema ya bure na isiyo na kipimo ndio tumaini letu la kuwa vingine. Na chanzo cha neema hiyo sio thamani ya majina yetu, lakini ni thamani isiyo na kifani ya jina lake la Mungu. Kumbuka 2 Timotheo 2:13: “Kama tusipoamini, Yeye hudumu kuwa mwaminifu-kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.” Mungu anatukusudia tujifunze kutoka kwa dhambi hii ya kushangaza kuwa neema ya wokovu wetu hakika umethibitishwa sio kwa thamani yetu bali kwa thamani yake Mungu mwenyewe.
4) Utawala wa kifalme ni wa Mungu pekee.
Yafaa tujifunze kutokana na njia ya Mungu ya kuleta utawala wa kifalme katika Israeli kuwa utawala wa kifalme ni wa Bwana pekee. Mungu anatawaza uhusiano wake na Israeli bila mfalme mwanadamu ili kufanya wazi kabisa kuwa Mungu pekee ndiye anastahili kuwa mfalme wa Israeli. Mungu pekee ndiye mfalme. Wakati Israeli walipoomba kuwa na mfalme, walikuwa wakikataa ukweli huu. Mungu anaisema wazi katika 1 Samueli 8:7 “Wamenikataa Mimi kuwa mfalme wao.”Kama Mungu angeuanzisha historia ya Israeli kwa Musa na Yoshua kuwa wafalme wa kwanza, haungekuwa wazi kuwa ni Mungu pekee anaweza kuwa mfalme wa Israeli. Hatakuwa na washindani wanadamu.
5) Mwanadamu-Mungu lazima awe Mfalme.
Yamkini, yafaa tujifunze kutoka kwa njia ya Mungu ya kutawaza mfalme mwanadamu kuwa malengo yake ni kutawaza shina la wafalme wanadamu ambao wote watashindwa hadi mfalme aje ambaye hakuwa tu mwanadamu bali pia Mungu, kwa sababu ni Mungu tu anaweza kuwa mfalme wa Israeli. Jambo ni kwamba Mungu pekee ndiye mfalme wa Israeli, na kuna mfalme ajae, Mwana wa Daudi, ambaye hatashindwa kama wengine. Hatakuwa kama mwanadamu mwingine mwenye dhambi. Atakuwa mwanadamu ambaye ni Mungu.
Swali la mwisho kinywani mwa Yesu ambalo linanyamazisha Wafarisayo latolewa kwenye Zaburi 110:1, pahali Daudi asemavyo, “BWANA [Yahwe] anamwambia Bwana wangu [Mfalme ajaye na Masiya]: “Keti mkono wangu wa kuume, mpaka niwafanye adui zako kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”Yesu ananukuu haya halafu anawauliza wapinzani wake, “Hivyo basi Daudi anamwita Bwana, basi anakuwaje mwanawe?” Kwa maneno mengine, kwa wale wako na masikio na wasikie, Yesu ni zaidi ya Mwana wa Daudi. Ni zaidi ya mfalme mwanadamu tu. “Hapo mwanzo alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu . . . Na neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukaona utukufu Wake, utukufu kama wa mwana Pekee atokaye kwa Baba.” (Yohana 1:1, 14) Ni Mungu pekee ndiye anaweza kuwa mfalme wa mwisho na mwenye haki juu ya Israeli.
6) Mfalme alifilia watu wake.
Mwisho yafaa tujifunze kutoka kwa vile Mungu anavyoleta mfalme mwanadamu kwa Israeli kuwa kulihitajika kuwa na mfalme mwanadamu. Ni Mungu pekee anaweza kuwa mfalme mwenye haki wa Israeli. Kulihitajika kuwe na mfalme mwanadamu. Kwa nini? Kwa sababu ndipo Mungu awe na watu wa kutawala na kuwapenda, ambao hawakuwa jehanamu kwa sababu ya dhambi, mfalme alihitajika kufa kwa ajili ya watu. Basi mfalme wa Israeli ndiye Mungu-mwanadamu ndipo mfalme aweze kuwa Mungu, lakini yeye pia ni Mungu-Mwanadamu ndipo mfalme aweze kufa.
Wakati Samueli alisema, “Msiogope, ninyi waasi, watenda dhambi wasio na shukrani; mmetenda uovu huu wote” (1 Samueli 12:20). Ni nini kilikuwa chanzo cha neema hii? Ilikuwa thamani ya jina la Mungu. “Kwa ajili ya jina lake kuu BWANA hatawakataa watu wake” (Mstari 22). Kuinuliwa na kuburai kwa jina la Mungu ni chanzo cha neema. Na ni wapi hiyo kuburai kulionyeshwa kwa uwazi na kwa uhisho? Jibu: Msalabani mwa Kristo. Warumi 3:25: “Yeye ambaye Mungu alimtoa awe dhabibu ya upatanisho kwa njia ya Imani katika damu yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki yake, kwa sababu kwa ustahimili Wake aliziachilia zile dhambi zilizotangulia kufanywa.”
Msalabani, kwa ajili ya Jina Lake
Hakika alifanya. Katika siku hiyo wakati watu walistahili kuangamizwa kwa sababu ya kuomba mfalme, Mungu aliwasamehe na kuwaachilia dhambi zaok—kwa ajili ya jina lake. Lakini huwezi kuficha dhambi chini ya mkeka wa ulimwengu na bado uliinue jina lake kama Mungu mwenye haki na takatifu. Dhambi lazima ishughulikiwe. Lazima iadhibiwe. Na ndipo wakati Yesu alitufilia.
Sababu pekee ambayo watu wenye dhambi kama sisi wanaweza kuwa na mfalme aliye mkuu, na tukufu na mwenye nguvu na mwema na mtakatifu na mwenye hekima kama Yesu bila kumezwa na dhambi zetu ni kuwa Mungu alipanga mfalme afilie watu wake na kufufuka tena. Katika kila Injili, Yesu anaulizwa kabla tu afe, “Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi? Na anjibu, “Unasema hivyo” (Mathayo 27:11; Marko 15:2; Luka 23:3; Yohana 18:33)
Mfalme wa wote ajaye
Na si tu mfalme wa wayahudi, lakini wa wote—haswa wale wanaomtumaini. Ameketi katika mkono wa kuume wa Baba sasa hadi maadui wake watakapowekwa chini ya miguu yake na wateule wake waote wamekusanyika kutoka kwa watu wote wa ulimwengu. Hatimaye mwisho utafika. Naye Kristo atakuja mara ya pili, si ili kuchukua dhambi bali kuwaletea wokovu wanaomngoja kwa shauku” (Waebrania 9:28). Na “kwenye vazi lake na paja lake liliandikwa jina hili”—Si mfalme wa Wayahudi lakini “MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA” (Ufunuo wa Yohana 19:16). Amina. Kuja, Yesu mfalme.