Raha ya Mungu katika Mwanawe

Huyu ni mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye sana.

Utangulizi

Tunaanza mfululizo mpya ya ujumbe asubuhi hii ambayo itatufikisha, Bwana akitujalia, hadi asubuhi ya Jumapili ya Pasaka, Aprili 19. Hivyo ningependa kwanza kueleza jinsi nimeendelezwa kupanga mfululizo huu.

Kuona ni kuwa

Ifikapo wakati wa kuelewa yale ambayo yafaa kufanyika katika tendo la kuhubiri mimi huongozwa na maandikokadhaa ya biblia, hasaa 2 Wakorintho 3:18.

Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji tunaakisi utukufu wa Bwana, kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, utokao kwa Bwana, ambaye ndiye Roho.

Naamini Nakala hii inatufundisha kwamba moja ya njia tunazoendelea kubadilishwa kuwa katika mfano wa Kristo ni kwa kuangalia utukufu wake. “Sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji tunaakisi utukufu wa Bwana, kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye.” Njia ya kuwa zaidi na zaidi kama Bwana ni kuweka nadhari yako katika utukufu wake na kushikilia mwanga wake.

Tunavuma musiki ambayo tunasikiliza. Tunaongea kwa lafudhi ya ujirani wetu. Tunachukua stahifu ya wazazi wetu. Na kwa kawaida huwa tunaiga watu wenye tuna sharifu zaidi. Hivyo ndivyo ilivyo na Mungu. Tukimakinika kwa kumtazama na kushikilia utukufu wake  katika mtazamo wetu, tutabadilishwa kutoka kiasi cha utukufu mmoja hadi mwingine tukiendelea kufanana na yeye. Ikiwa vijana huunda nywele zao kama za wasanii wanaosharifu, vile vile Wakristo huunda mienendo yao kama Mungu wanayemsharifu. Katika hiyo shughuli ya kiroho kuona si kuamini tu; kuona ni kuwa.

Kuhubiri kama dhihirisho wa utukufu wa Mungu

Funzo ninalopata kuhusu kuhubiri ni kuwa kwa kadiri kubwa kuhubiri lazima ikuwe onyesho la utukufu wa Mungu, kwa sababu lengo la kuhubiri ni kubadilisha watu kuwa onyesho la Mungu. Nadhani hii inafaa na maoni ya Paulo ya kuhubiri kwa sababu  mistari minne tu baadaye, katika 2 Wakorintho 4:4, anaelezea maudhui ya mahubiri yake kama nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu.” Na mistari miwili baadaye katika mstari wa 6 anaielezea tofauti kidogo kama "nuru ya maarifa ya utukufu wa Mungu katika uso wa Kristo.

Hivyo, kulingana na Paulo, mahubiri ni njia ya kuwasilisha mwanga kwa mioyo yenye giza ya wanaume na wanawake.

Katika mstari wa 4 nuru inaitwa “nuru ya Injili,” na katika msari wa 6 nuru inaitwa “nuru ya maarifa.”

Katika mstari wa 4 injili ni habari njema ya utukufu wa Kristo, na katika mstari wa 6 maarifa ni maarifa wa utukufu wa Mungu.

Hivyo katika hizo mistari miwili nuru iliyowasilishwa ndani ya moyo ni nuru wa utukufu - utukufu wa Kristo na utukufu wa Mungu. Lakini hayo si utuku miwili tofauti. Katika mstari wa 4 Paulo anasema ni ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano wa Mungu. Na katika mstari wa 6  anasema kwamba utukufu wa Mungu iko katika uso wa Kristo. Hivyo nuru iliyowasilishwa katika kuhubiri ni nuru wa utukufu, na unaweza kuongea kuhusu utukufu hivi kama utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano wa Mungu, au utukufu wa Mungu invyojitokeza kikamilifu katika Kristo.

Kuhubiri ni kusimulia au kuonyesha au kuangaza utukufu takatifu kwa mioyo ya wanaume na wanawake (4:4-6), ili kwamba kwa kutazama utukufu huu wanaweza badilishwa kuwa katika mfano wa Bwana kutoka kiasi moja ya utukufu hadi mwingine (3:18).

Inajulikana kama kweli kutokana na ustadi wa kuzoea

Hii si ujenzi bandia au wa kitaaluma. Ni wazi kile najua kuwa ni kweli kutokana na uzoefu wangu mwenyewe (kama vile wengi wenu!): kuona Mungu kuwa yule aliye kwa kweli umeonyesha tena na tena kuwa na nguvu zaidi ya kulazimisha katika kunihamasisha kutaka utakatifu na furaha ndani yake.

Mimi na wewe tunajua kutokana na uzoefu kwamba chanzo cha migogoro katika nafsi ya binadamu ni kati ya utukufu wawili  - utukufu wa dunia na anasa zote fupi inaweza kupeana, dhidi ya utukufu wa Mungu na raha ya milele yote inaweza kupeana. Hizi utukufu miwili zinashindana kwa ajili ya utii, pongezi, na furaha ya mioyo yetu. Na kazi ya kuhubiri ni kuonyesha na kufafanua na kuashiria utukufu wa Mungu katika namna ambayo ubora wake kuu na yenye thamani uangaze ndani ya moyo wako ili kwamba ubadilishwe kutoka kwa kiasi cha utukufu hadi mwingine.

Changamoto zinazomkabili mhubiri

Hiyo ina maana kwamba kama mhubiri daima ninakabiliwa na swali: jinsi gani mimi  nitaonyesha ubora wa utukufu wa Mungu ili kwamba idadi kubwa ya watu wauone na kupata kubadilika? Nilipokuwa ninajiuliza swala hiyo wakati wa faragha wiki mbili zilizopita, jibu mpya ilinikujia katika mawazo.

Nilikuwa nasoma tena sehamu ya kitabu cha Henry Scougal The Life of God in the Soul of Man (Maisha ya Mungu Katika Nafsi ya Mtu). Alitoa maoni ya kupenyesha: “Thamani na fahari ya nafsi inapimwa na kile kipendacho” (k. 62). Nami nikayaona kama ni kweli kabisa. Na mawazo yakanijia kwamba kama ni kweli kwa mtu, kama Scougal alivyosema, bila shaka ni kweli kwa Mungu pia: “Thamani na fahari ya nafsi ya MUNGU inastahili kupimwa na kile apendacho.”

Hivyo nikatafuta katika maandiko kwa siku kadhaa nikitafuta maeneo yote ambayo yanayotumbia yale ambayo Mungu anapenda na anafurahia na kuridhikia anapoifurahia. Matokeo ni mpango wa kuhubiri ujumbe 13 ziitwazo raha ya Mungu.

Hivyo ni ombi langu, na ninatumai kwamba utaifanya kuwa ombi lako, kuwa kwa kuona vitu ambayo yanamfurahisha Mungu tutaona fahari na thamani ya nafsi yake; na kwa kuona thamani na fahari ya nafsi yake tutauona utukufu wake; na kwa kuuona utukufu wake tutabadilishwa kutoka kwa kiasi mmoja ya utukufu hadi nyingine katika kufanana na yeye; na kwa kubadilishwa kufanana naye tutakabiliana na mji huu, na wale watu wa ulimwengu ambao hawajafikiwa na shahidi ulio hai wa Mwokozi mkuu mwenye nguvu na kuvutia. Tunaomba Bwana aridhike na atume uamsho mkubwa wa upendo na utakatifu na nguvu hata tukimtazama na kuomba kwa bidii zaidi ya wiki ijayo 13.

Ufafanuzi

Katika kuonyesha thamani ya nafsi ya Mungu katika kile apendacho lazima tuanzie mwanzoni. Kitu cha kwanza na msingi ambayo tunaweza kusema kuhusu raha ya Mungu ni kwamba yeye huridhika ndani ya Mwana wake. Nitajaribu kufunua ukweli huu katika thibitisho tano.

1. Mungu ana raha katika Mwanawe.

Katika Mathayo 17, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane juu ya mlima mrefu. Walipokuwa peke yao jambo la kushangaza lilifanyika. Kwa ghafla Mungu alimpa Yesu muonekano wa utukufu. Funfu la 2: "Uso wake ukang'aa kama jua na nguo zake zikawa na weupe wa kuumiza macho." Alafu katika fungu la 5 wingu linalong'aa likawafunika na sauti ikatoka kwenye hilo wingu ikisema, "Huyu ni mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye sana, msikilizeni Yeye."

Kwanza, Mungu huwapa wanafunzi mtazamo mfupi wa utukufu wa mbingu wa kweli wa Yesu. Hii ndio Petro asemalo katika 2 Petro 1:17—"[Kristo] alipewa heshima na utukufu kutoka kwa Mungu Baba" Basi Mungu akaonyesha moyo wake kwa ajili ya Mwanawe kusema maneno mawili: "Nakupenda mwanangu" ("Huyu ni Mwanangu mpendwa"), na "Ninapata raha katika mwana wangu " ("ninayependezwa naye").

Alisema hayo katika tukio nyingine tena: katika ubatizo wa Yesu, Roho Mtakatifu anapokuja chini na kumpaka Yesu kwa ajili ya huduma yake, alionyesha upendo wa Baba na usaidizi-"Huyu ni Mwanangu mpendwa, ambaye nimependezwa."

Na katika Injili wa Yohana, Yesu anazungumza mara kadhaa kuhusu upendo wa Baba kwake: kwa mfano, Yohana 3:35,"Baba anampenda Mwana, naye ametia vitu vyote mikononi Mwake."Yohana 5:20, "Baba ampenda Mwana na kumwonyesha yale ambayo Yeye Baba mwenyewe anayafanya."

(Angalia pia Mathayo 12:18 ambapo Mathayo ananukuu Isaya 42:1 akimaanisha Yesu: "Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza, mteule wangu, ambaye ninapendezwa naye" Neno "radhi" hutokana na neno la Kiyahudi ratsah , ambaye maana yake ni "furahia katika")

Hivyo taarifa yetu ya kwanza ni kwamba Mungu Baba ampenda Mwana, na si kwa dhabihu ya huruma yoyote ya kujikana, lakini kwa upendo wa furaha na raha. Amefurahishwa zaidi na Mwanawe! Anapomtazama mwanawe, anafurahia na kusharifu na kulitunza na kumtuza na kupendeza anachoona.

2. Mwana wa Mungu ana utimilifu wa uungu.

Ukweli huu utatusaidia kuzuia kosa kuhusa ukweli wa kwanza. Waweza kukubaliana na thibitisha kwamba Mungu anaridhika katika Mwanawe, lakini kufanya kosa la kufikiri kwamba Mwana ni mtu tu mwenye utakatifu la ajabu ambaye Baba alichagua kuwa Mwanawe kwa sababu aliridhika naye sana.

Lakini Wakolosai 2:9 inatupa mtizamo tofauti sana juu ya mambo. “Ukamilifu wote wa uungu umo ndani ya Kristo katika umbile la mwili wa kibinadamu.” Mwana wa Mungu si tu mtu aliyekuchaguliwa. Ana ukamilifu wa uungu ndani yake.

Kisha Wakolosai 1:19 inahusisha hii na furaha ya Mungu: “Ilimpendeza Mungu kwamba ukamilifu Wake wote wa kimungu uwe ndani Yake.” Kwa maneno mengine, ilikuwa ni furaha ya Mungu kwa kufanya hivyo. Mungu hakutazama dunia na kupata mtu aliyehitimu kupokea furaha yake na kisha kumchagua kama Mwanawe. Bali Mungu mwenyewe alichukua hatua ya kuhifadhi ukamilifu wake kwa mtu katika tendo la kufanyika mwili. Au tunaweza sema ya kwamba alichukua hatua ya ku mvalisha ukamilifu wa uungu wake mwenyewe na asili ya binadamu. Na Wakolosai 1:19 inasema alifurahishwa na kufanya hivyo! Ilikuwa mapenzi na furaha yake.

Tunaweza jikuta tukisema kwamba Mungu hakupata Mwana ambaye alikuwa anapendeza, lakini alimtengeneza Mwana ambaye alimpendeza. Hata hiyo, itakuwa inapotosha, kwa sababu ukamilifu wa uungu, ambayo sasa umo kimwili (Wakolosai 2:9) katika Yesu , tayari alikuwepo katika muundo binafsi kablaya kuchukua asili ya mwanadamu katika Yesu. Hii inatusukuma zaidi katika Uungu na hadi uthibitisho 3.

3. Mwana ambaye Mungu anafurahia ni mfano wa milele na picha ya Mungu na hivyo ni Mungu mwenyewe.

Hapa katika Wakolosai 1:15 Paulo asema,

Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, na kifungua mimba wa viumbe vyote [maanake, yule ambaye ana hadi ya kupandishwa ya uwana wa Mungu juu ya viumbe vyote, kama vile maneno yanayofuata yanathibitisha]; kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa mbinguni na duniani.

Mwana ni mfano wa Baba. Nini maana ya maneno hayo? Kabla ya kueleza, hebu tutazame baadhi ya nyadhifa nyingine kama hayo.

Wahebrania 1:3 wasema hivi kuhusu Mwana,

Ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi Yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno Lake lenye uweza.

Katika Wafilipi 2:6 Paulo anasema,

Ingawa alikuwa na namna ya Mungu, hakuhesabu usawa na Mungu kama kitu cha kushika, lakini alikubali kuacha vyote, akachukua hali ya mtumwa.

Hivyo Mwana ambaye Mungu anafurahia ni mfano wake; ni mng'ao wa utukufu wake; ni mfano halisi ya nafsi yake; ana namna ya Mungu; na usawa na Mungu.

Kwa hiyo hatupaswi kushangaa wakati Mtume Yohana, katika Yohana 1:1, anasema,

Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

Hivyo itakuwa upotovu kabisa kusema kwamba Mwana ambaye Mungu anafurahia, aliumbwa wakati wowote. "Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu." Kwa wakati wote kumekuwa na Mungu, kumekuwa na neno la Mungu, Mwana wa Mungu, ambaye alichukuwa asili ya binadamu katika Yesu Kristo.

Sasa tunaweza kupata wazo bora ya kile Biblia inamaanisha inapomwita picha au mng’ao au mfano halisi au namna ya Mungu ambaye ni sawa na Mungu.

Tangu milele iliyopita ukweli moja ambayo daima imekuwa, ni kuwepo wa Mungu. Hii ni fumbo kubwa, kwa sababu ni vigumu kwetu kufikiria kuwa Mungu hakuwa kabisa na mwanzo na yuko tu hapo milele na milele bila chochote au mtu yeyote ambaye anamfanya akuwe - ukweli kamili ambaye inambidi kila mmoja wetu kuhesabu tupende tusipende.

Biblia inafundisha kwamba huyu Mungu wa milele daima alikuwa

  • picha kamili ya mwenyewe
  • mng’ao kamili ya asili yake,
  • mfano halisi kamili au alama ya asili yake,
  • namna (fomu) kamili au onyesho wa utukufu wake.

Tuko ukingoni mwa yale hayawezi kutamkwa hapa, lakini pengine tunaweza kuthubutu kusema sana kwamba: bora tu wakati wote Mungu amekuwa Mungu, amekuwa na ufahamu wa nafsi yake, na mfano aliyo nayo kumhusu ni kamilifu na hivyo kamili na kamili kiasi cha kuwa hai, kujizalisha (au zaa, fanya) mwenyewe. Na hii hai, picha binafsi au mng'ao au namna ya Mungu ni Mungu, yaani, Mungu Mwana. Na kwa sababu hiyo, Mungu Mwana ni wa milele pamoja na Mungu Baba na sawa katika kiini na utukufu.

4. Furaha ya Mungu kwa mwanawe ni furaha kwake mwenyewe.

Kwa vile Mwana ni picha wa Mungu na mng’ao wa Mungu na mfano wa Mungu na namna wa Mungu, sawa na Mungu, na hakika NI Mungu, Hivyo furaha wa Mungu katika Mwanawe ni furaha kwake mwenyewe. Hivyo basi asili, mwanzo, kamili, msingi wa furaha wa Mungu ni furaha anayo katika ukamilifu wake mwenyewe anavyoviona vinavyotokeza katika Mwanawe. Anapenda Mwanawe na anafurahia ndani ya Mwanawe na kufurahishwa katika Mwanawe maanake mwana ni Mungu mwenyewe.

Inaonekana kama ubatili na inakaa makeke na kujikinai na enye choyo kuihusu kwa sababu hiyo ndiyo ingekuwa maana yake kama yeyote kati yetu angepata furaha asili na zaidi kwa kujiangalia mwenyewe kwenye kioo. Tutakuwa bure na wenye majivuno na kujikinai na wachoyo.

Lakini kwa nini? Kwa sababu tuliumbwa kwa minajili ya kitu bora yenye ukubwa zaidi na yenye cheo kuu na mkuu tena zaidi kuliko kujitafakari. Nini? Kutafakari na kufurahia Mungu! Chochote chini ya hayo itakuwa kuabudu sanamu. Mungu ni mtukufu zaidi ya viumbe vyote. Kutompenda na kutomfurahia ni matusi zaidi kwa thamani yake.

Si pia hiyo ni kweli kwake Mungu? Mungu atawezaje kutomtusi yule ambaye ana urembo zaidi na yenye utukufu? Kunaweza kuwa tu na jibu mmoja: Lazima Mungu apende na kufurahia uzuri (urembo) na ukamilifu wake kuliko chochote. Kufanya hivyo mbele ya kioo, kwetu, ndicho kiini cha ubatili; lakini Muungu kuifanya mbele ya mwanawe ndicho kiini cha haki.

Si kiini cha haki ni kuongozwa na furaha kamili katika kile utukufu kamilifu? Na si kinyume ya haki tunapoweka shauku zetu kuu kwa mambo yenye thamani ndogo au yale ambayo hayana thamani?

Kwa hivyo haki ya Mungu ni juhudi usio na mipaka na furaha na radhi aliye nazo katika thamani na utukufu wake mwenyewe. Na kama angetenda kinyume na shauku hii ya milele kwa ukamilifu wake, angekuwa mwovu; na atakuwa ana abudu sanamu.

Humu imo kikwazo kikubwa kwa wokovu wetu: kwani itakuwaje Mungu mwenye haki anaweka shauku yake katika wenye dhambi kama sisi? Lakini humu pia limo msingi halisi ya wokovu wetu, kwa kuwa ni mahsusi wa suala usio na mipaka yenye Baba aliyo nayo kwa Mwana ambayo hufanya inawezekana kwangu, mwovu, kupendwa na kukubalika katika Mwana, kwa sababu katika kifo chake alirejesha matusi na majeruhi yote niliyokuwa nimefanyia utukufu wa Baba katika dhambi zangu.

Tutaiona hii mara kadha katika wiki zijazo - jinsi radhi ya Baba katika ukamilifu wake ndio chemichemi ya ukombozi na matumaini na furaha ya milele. Leo ni mwanzo tu.

Nita funga na thibitisho la tano na tendo la kutia ya mwisho. Ikiwa Scougal hajakosea - kwamba thamani na fahari ya nafsi inapimwa na kifaa (na ningependa kuongeza, kiwango) ya upendo wake – basi …

5. Mungu ni bora zaidi na mwenye thamani kuu zaidi ya viumbe vyote.

Kwa nini? Kwa sababu amependa Mwanawe, mfano wa utukufu wake mwenyewe, kwa kiasi na nguvu kamilifu kutoka milele yote. Jinsi Baba na Mwana na Roho wa upendo wamekuwa na utukufu na furaha unaopita kati yao tangu milele!

Hebu tusimameni katika hofu kwa huyu Mungu wa ajabu! Na tugeukeni kutoka kwa machukio ndogo ndogo na anasa za kidunia na shughuli ndogo ndogo za maisha, na tujiunge na furaha ambayo Mungu anayo katika sura ya ukamilifu wake mwenyewe, yaani, Mwanawe. Tuombe:

Mungu usio na mwisho, wa milele na mwenye haki, tunakiri kwamba mara nyingi tumekurahisisha na kujiinua sisi wenyewe katikati ya shauku wako ambapo wewe mwenyewe unastahili katika nafsi ya Mwana wako. Tunatubu na kuacha ufidhuli wetu na kwa furaha tunasimama katika hofu kwa furaha wako wa milele na wa kujitosheleza katika ushirika wa utatu. Na ombi letu, kwa maneno la Mwana wako (Yohana 17:26), ni kwamba upendo ambayo umempenda nayo uweze kuwa ndani yetu, ili nasi tuchukuliwe katika huo ushirika wa furaha na katika huo bahari wa upendo wa milele na milele. Amina.