Ujumbe wa Warumi 1-8 wenye nguvu na wa kurehemu
Paulo anaandika barua kwa kanisa la Warumi kuhamasisha msaada wao kwa ajili ya misheni wake kule Hispania. Katika Warumi 15:2 anaandika, “Nimekusudia kufanya hivyo nitakapokuwa njiani kwenda Hispania. Natarajia kuwaona katika safari yangu na kusafirishwa nanyi mpaka huko, baada ya kufurahia ushirika wenu kwa kitambo kidogo.” Hajawahi Kwenda Roma na hata kukutana na baadhi ya Wakristo hao. Hivyo anaandaa Injili yake kwa ajili ya mtazamo wao katika sura hizi 16.
Ndivyo kwamba wamishenari wetu wote waujue kitabu cha Warumi na kuhubiri katika kitabu cha Warumi. Na pia kwamba wale watumao wamishenari waujue kitabu cha Warumi na kuishi jinsi ya kitabu cha Warumi ili tuweze kutuma wamishenari jinsi Paulo alitaka kutumwa na kuungwa mkono kutoka Roma kwenda Hispania. Ujumbe wa nguvu na huruma wa kitabu huu utawafanya Wamarekani tajiri kuanza kuishi kama vile wakati wa vita, na kumwaga rasilimali zao katika shughuli za kueneza Injili. Na ujumbe wenye nguvu na huruma wa kitabu hiki, katika midomo ya wamishenari wanaoteseka, utavunja nguvu za giza nguvu za giza na kupanda Kanisa la Kristo katika maeneo yaliyoadhirika mno.
Vipengele vya kiutamaduni mbalimbali na kimataifa yaliyomo katika waraka huu
Haishangazi basi unapoanza kusoma barua hii utakutana na vipengele vya kimataifa na tamaduni mbalimbali. Katika Romans 1:5 Paulo anatueleza lengo la utume wake: “Ambaye kwa kupitia Kwake na kwa ajili ya Jina Lake, tumepokea neema na utume ili kuwaita watu miongoni mwa watu wote wasiomjua Mungu, waje kwenye utii utokanao na imani. Warumi inahusu mataifa—makundi ya watu ambao bado hawajamwamini Kristo. Ambao hawajafanyiwa haki na pia hawajatakaswa na hivyo hawatatukuzwa wasipofikiwa na injili.
Basi katika mstari wa 14 anatuambia tena wajibu wake wa kitume: “Mimi ni mdeni kwa Wayunani na wasio Wayunani, kwa wenye hekima na wasio na hekima.” Na ili tusidhani kwamba amewaacha nje Wayahudi, anasema katika msitari wa 16, ”Mimi siionei haya Injili ya Kristo kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwanza kwa Myahudi na kwa Myunani pia.” Wayahudi, Wagiriki, Wenyeji, wenye busara, wajinga! Kwa maneno mengine, huu ujumbe wenye nguvu na huruma katika kitabu cha Warumi inavunja tofauti za kitaifa, tofauti za kitamaduni na tofauti ya elimu.
Hii ni muhimu sana kuona hasa katika wakati wetu wa filosofia ya uwingi wa dini—wakati sawa na karne ya kwanza wakati kanisa ya Kristo ilienea kwa haraka sana. Ukristo siyo dini ya kikabila, lakini inatoa wito wa imani na utii kutoka kwa kila kabila na lugha na jamaa na taifa. Yesu si mmoja kati ya miungu wengi. Yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa Wafalme, na hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.’’ Ujumbe wa Warumi wenye nguvu na huruma si moja wapo wa njia za wokovu miongoni mwa wengi. Ni njia pekee ya wokovu, kwa sababu Yesu Kristo ni Mwana pekee wa Mungu na Mwokozi.
Madai haya daima inapingwa. Na inapingwa leo, hasa nchini Marekani, hata miongoni mwa wanaojiita Wakristo, na, bila shaka, kati ya Waislamu na Wayahudi. Katika StarTribune wa Ijumaa kulikuwa na makala nyingine iliyokanusha umuhimu wa imani katika Kristo. Tume ya pamoja ya Maaskofu Katoliki na Wanazuoni wa Marekani ilitoa hati iitwayo "kutafakari juu ya ahadi na Misheni." Kichocheo kikuu, mwandishi alisema, ni hii: "Juhudi ya kubadilisha Wayahudi 'haikubaliki tena kiteolojia' . . . kwa sababu Wayahudi tayari 'wanakaa katika agano na Mungu " (Ijumaa Septemba 20, 2002, p. A23). Kwa maneno mengine, kuna njia moja ya wokovu kwa Wayahudi wanaomkataa Kristo, na kuna njia nyingine ya wokovu kwa Wakristo wanaompokea Kristo.
Hii ni taarifa ya uongo na unaovunja moyo kutoka kwa Maaskofu wa Kikristo, hasa tukizingatia matamshi wa Yesu, "Yeyote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake." (Yohana 3:36). Ndiposa, kwa watu wa mataifa mengine wanaomkubali na wale Wayahudi wanaomkataa, Yesu alisema, "wengi [watu wa mataifa mengine] watatoka mashariki na magharibi nao wataketi karamuni pamoja na Abrahamu, Isaki na Yakobo katika Ufalme wa Mbinguni. Lakini warithi wa ufalme [Wayahudi ambao wanamkataa] watatupwa katika giza la nje, ambako kutakuwa na kulia na kusaga meno." (Mathayo 8:11-12).
Hivyo ni muhimu sana kwamba tuyaone madai zima wa ujumbe wenye nguvu na rehema ya Warumi. Hatushughuliki hapa na maoni ya binadamu, au falsafa za binadamu, au mpango wa kujiboresha binafsi, au dini ya kikabila, au kitu hafifu nz dogo. Tunazungumzia hapa na habari mmoja ya kweli kuwa Mungu mmoja ametenda jambo la kipekee katika historia kuokoa watu kwa kumtuma Mwana wake wa pekee kufa kwa ajili ya wenye dhambi na kufufuka tena. Kukataa habari hii ni kuangamia.
Kusudi ya waraka Huu: Warumi 1:16-17
Hivyo Paul anataja lengo lake katika Warumi 1:16-17 na kisha anaelezea jinsi inavyotumika katika maeneo mengine wa barua. "Mimi siionei haya Injili ya Kristo kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwanza kwa Myahudi na kwa Myunani pia. 17 Kwa maana katika Injili haki itokayo kwa Mungu imedhihirishwa, haki ile iliyo kwa njia ya imani hadi imani. Kama ilivyoandikwa: ‘‘Mwenye haki ataishi kwa imani."
Kwanza, Paulo anasema kwamba ujumbe wake—Injili yake—ni wenye nguvu na huruma ya kuokoa: ni nguvu ya Mungu kwa wokovu. Na wokovu hii ni kwa kupitia njia ya imani. Nguvu ya Injili ya kuokoa hupenya roho zetu kwa imani katika Yesu Kristo.
Alafu katika mstari wa 17 anaelezea sababu injili ina uwezo huu: "Kwa maana ndani yake haki itokayo kwa Mungu imedhihirishwa." Injili ina uwezo wa kuokoa wale wanaomwamini Kristo kwa sababu inadhihirisha haki ya Mungu. Hii inamaanisha nini?
Warumi 1:18 - 3:20: Sababu sote tunahitaji kuokolewa
Kabla ya kueleza maana yake, Paulo anatumia Warumi 1:18 - 3:19 kuonyesha kwa sababu sote tunahitaji kuokolewa. Waweza kuona muhtasari wake katika Warumi 3:9, "Tumekwisha kuhakikisha kwa vyo vyote kwamba Wayahudi na watu Mataifa wote wako chini ya nguvu ya dhambi." na mstari wa 19: "Kila kinywa kinyamazishwe na ulimwengu wote uwajibike kwa Mungu." Kwa hivyo sisi ni wenye dhambi. Sote tuko chini ya ghadhabu ya Mungu (1:18). Hatuna haki iwezayo kutuelekeza kwake, na 3:20 hueleza wazi kwamba kamwe hatuwezi kujihalalisha wenyewe: Kwa hiyo hakuna binadamu hata mmoja atakayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa matendo ya sheria. "Sisi ni wenye dhambi. Tumo chini ya ya ghadhabu ya Mungu ambayo ni wenye haki na pia takatifu. Na hatuwezi kujikomboa au kujihalalisha wenyewe kupitia matendo.
Warumi 3:21-31: Ufunuo wa haki ya Mungu kwa imani katika Yesu na athari yake
Sasa Paulo anarudia lengo lake kuu katika Warumi 1:16-17 na anaeleza kwamba injili ni nguvu ya Mungu kuwaokoa waumini kwa sababu inadhihirisha haki ya Mungu katika imani. Anasema katika msitari 21 - 22, "Lakini sasa, haki itokayo kwa Mungu imedhihirishwa [hapa anachagua ufunuo wa haki ya Mungu katika aya ya 17] pasipo sheria, ambayo Torati na Manabii wanaishuhudia – 22 haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa Yesu Kristo kwa wote wamwaminio."
Ufunuo wa haki ya Mungu ambayo inaipatia injili uwezo wake na kuokoa waumini ni nini? Ni dhihirisho wa "haki ya Mungu ijayo kupitia imani katika Yesu." Ni haki ya Mungu. "Ni haki ya Mungu inayofunuliwa kwetu kama kipaji kupitia imani. Ndiyo tuitayo imani. Hivyo Paulo anasema katika mstari 24 kwamba wenye dhambi wamwaminiye Kristo "wamehalalishwa kwa neema kama kipaji, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo yesu." Ufunuo wa haki ya Mungu ifanyayo injili uwezo wa Mungu kwa wokovu ni dhihirisho na kipaji ya haki ya Mungu kwa wenye dhambi wanaomwamini Kristo.
Warumi 3:25 inaeleza jinsi Mungu anavyoweza kuwahalalisha wenye dhambi bila yeye kuwa mwovu: "Yeye [Kristo] ambaye Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu Yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki Yake, kwa sababu kwa ustahimili Wake aliziachilia zile dhambi zilizotangulia kufanywa." Yaani, Mungu alimteua mwanawe kufa kwa ajili yetu ili kwamba ghadhabu na laana ya Baba iwe juu yake, wala sio juu ya walio amini. Hivyo anaonyesha chuki kwa dhambi na jinsi anavyoishughulikia. Basi, kama ilivyo katika mstari wa 26, anaweza kuwa "mwenye haki na mfanyishaye haki wa wale walio na imani katika Yesu."
Hivy kifo cha Kristo ndiyo msingi wa haki yetu. Tukimwamini, Mungu anatuhesabu wenye haki kwa ajili ya Yesu. Tunaonekana na kutendewa kama wenye haki. Hiyo ni kuhesabiwa haki. Na katika mstari wa 28 anaeleza wazi kwamba kusimama imara na Mungu si kwa matendo bali ni kwa imani, "Kwa maana twaona kwamba mwanadamu huhesabiwa haki kwa njia ya imani wala si kwa matendo ya sheria."
Na papa hapa usikose kidokezo ilioko katika mambo ya kimataifa, kimishenari, na tamaduni mbalimbali. Paulo mwenyewe anaionyesha katika msitari wa 29-30, "Je, Mungu ni Mungu wa Wayahudi peke yao? Je, Yeye si Mungu wa watu Mataifa pia? Naam, Yeye ni Mungu wa watu Mataifa pia. 30 Basi kwa kuwa tuna Mungu mmoja tu, atawahesabia haki wale waliotahiriwa kwa imani na wale wasiotahiriwa kwa imani iyo hiyo." Kufanyiwa haki kupitia imani katika Kristo ndio ujumbe wa rehema na wenye uwezo ulio angazwa kwa mataifa na kwa makundi ya watu wote na wengine wote tutakao kutanan nao. Kuna mkombozi mmoja tu, msalaba mmoja, ufufuo mmoja na njia mmoja ya kuwa na haki mbele ya Mungu mmoja, mabyo ni ku kuwa na haki yake iliyohesabiwa lkwetu kupitia imani katika Kristo, na si kwa matendo.
Warumi 4: kuhesabiwa kwa Abrahamu kwa haki kupitia imani pasipo matendo
Katika sura ya 4 Paulo anafanya ufafanuzi juu ya kuhesabiwa haki kupitia imani pasipo matendo kwa kutumia Abrahamu kama mfano. "Abrahamu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki" (mstari wa 3). Mojawapo wa mistari wenye thamana katika kitabu hiki imetolewa kutokana na mfano wa Abrahamu (mstari wa 5): "Lakini kwa mtu ambaye hafanyi kazi na anamtumaini Mungu, Yeye ambaye huwahesabia waovu haki, imani yake inahesabiwa kuwa haki." Si matendo, bali ni imani ambao hufanya watu kuhesabiwa haki. Hakika hii ni habari njema—Huu ndio ujumbe wa Warumi wenye uwezo na rehema.
Warumi 5: Matumaini na usalama katika uso wa mateso na kifo
Katika sura la 5 Paulo anajumuisha katika mstari wa 1, "Kwa hiyo, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa imani, tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo." Kisha anafunua uwemo wa mateso na mauti kwa wale walihesabiwa haki—hata anapotarajia kusisitiza zaidi kuhusu mateso katika sura ya 8. Msitari wa 3 inatueleza sababu tunaweza kushangilia katika mateso—inaelekeza katika uvumilivu na kuidhinisha na matumaini.
Alafu kulingana na hayo, anaendelea kutoa hoja katika sura la 8 vile alivyo hapo awali—kutoka kwa mkubwa hadi kwa mdogo—maanake, kama Mungu aweza kufanya mambo ambayo ni magumu, hivyo anaweza kufanya yale ambayo rahisi. Kumbuka katika Warumi 8:32 anaposema, "Ikiwa Mungu hakumhurumia Mwanawe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote [ni vigumu], atakosaje basi kutupatia vitu vyote kwa ukarimu pamoja Naye [ni rahisi]?" Hiyo ndiyo hoja ambao Paulo anatoa katika Warumi 5:9, "Basi, kwa kuwa sasa tumehesabiwa haki kwa damu Yake, si zaidi sana tutaokolewa kutoka katika ghadhabu ya Mungu kwa Yeye!" Hivyo ndivyo asemavyo katika mstari wa 10: "Kwa kuwa kama tulipokuwa adui wa Mungu tulipatanishwa naye kwa njia ya kifo cha Mwanawe [huu ndio jambo ngumu], si zaidi sana tukiisha kupatanishwa, tutaokolewa kwa uzima Wake [huu ndio jambo rahisi]."
Suala nyeti ni matumaini yetu na usalama katika uso wa mateso na mauti, kama vile ilivyo katika Warumi 8. Ukristo wa kawaida ni dhiki. "Imetupasa kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa kupitia katika taabu nyingi" (Matendo 14:22). Usisahau kamwe kwamba ujumbe Wa Warumi wenye nguvu na rehema imewekwa katika muktadha ya mateso iliyotarajiwa.
Kifo ni ukweli mkubwa katika kila tamaduni. Ukiwa na injili lazima uwe na maelezo kuhusu kifo na matumaini katika uso wa kifo. Huo ndio jukumu uchuliwao na Paulo katika Warumi 5:12-21, na anaitekeleza kwa kulinganisha Adamu, ambaye uasi wake ulileta dhambi na mauti, na Kristo, ambaye utii wake ulileta haki na uzima. Mstari wa 19 inaonyesha wazi huo tofauti: "Kwa maana kama vile kwa kutokutii yule mtu mmoja wengi walifanywa wenye dhambi, vivyo hivyo kwa kutii kwa mtu mmoja wengi watafanywa wenye haki." Dhambi ya Adamu na hukumu wake ulihesabiwa kwetu kwa sababu tunajumuishwa naye kupitia kuzaliwa; hivyo utii na kutolaumiwa ilihesabiwa kwetu kwa sababu tumejumuishwa naye kwa imani.
Paulo anajumuisha ushindi wa neema kupitia kristo katika mstari 21: " . . . vivyo hivyo neema iweze kutawala kwa njia ya kuhesabiwa haki hata uzima wa milele katika Yesu Kristo Bwana wetu."
Warumi 6: Umoja na Kristo ni kifo kwa dhambi na ukombozi kutoka utumwa
Nayo ili sababisha tatizo iliohitaji utatuzi: Ikiwa kweli tunahesabiwa haki kupitia imani pekee, na ikiwa panapo dhambi kuna neema zaidi, basi kwa nini tusitende dhambi ili neema ipate kuongezeka? Paulo ana jawabu katika sura ya 6 na mafundisho kuwa imani hutuunganisha kwa Kristo kwa njia ya kweli ili kwamba tu zoee na yeye kifo kwa dhambi na ukombozi kutoka utumwa (6:6, 17-17). Wote waliohesabiwa haki wanatakaswa.
Warumi 7: Kufa kwa sheria ili kwamba tuweze kujumuika pamoja na wengine
Katika sura ya 7 Paulo atoa hoja kuwa si mwelekeo juu ya kutunza sheria ambao hututakasa—ou inatufanya kama Kristo. Hapana, "Vivyo hivyo, ndugu zangu, ninyi mmeifia sheria kwa njia ya mwili wa Kristo, ili mweze kuwa mali ya mwingine, Yeye ambaye alifufuka kutoka kwa wafu, ili kwamba tupate kuzaa matunda kwa Mungu. 5Kwa maana tulipokuwa tunatawaliwa na asili ya dhambi, tamaa za dhambi zilizochochewa na sheria zilikuwa zikitenda kazi katika miili yetu, hivyo tulizaa matunda ya mauti" (7:4, 6).
Tunaishi maisha ya Ukristo katika kipaji cha bure na bidii kwa harakati za kuendeleza uhusiano na Yesu Kristo "ili mweze kuwa mali ya mwingine!" (7:4). Yeye ni uwezo na rehema na mfano na mamlaka wa maisha ya Kikristo.
Warumi 8: Hakuna kitakachotutenga na upendo wa Kristo
Hii ili tuelekeza, katika hizi wiki chache zilizopita, hadi Warumi 8. Nani atakayetutenga na upendo wa Kristo (mstari wa 35)? Je, waona uhusiano kati yake na Warumi 7:4? Kufa kwa sheria ili tuweze kuwa mali ya mwingine—kwa yule aliyefufuliwa kutoka wafu, yesu Kristo. Hiyo ndiyo kiini cha kuishi na cha kufa. Nani basi atatutenga na upendo wa Kristo? Jibu: Hakuna. Nani atakayetutenga na upendo wa Mungu katika Kristo? Jibu: Hakuna.
"Kama tunaishi, tunaishi kwa Bwana, nasi pia tukifa twafa kwa Bwana. Kwa hiyo basi, kama tukiishi au kama tukifa, sisi ni mali ya Bwana. Kwani kwa sababu hii hasa, Kristo alikufa na akawa hai tena kusudi apate kuwa Bwana wa wote, yaani, waliokufa na walio hai" (Warumi 14:8-9). Tuishi chini ya uongozi wake, tufe ndani ya uongozi wake. Na daima tuimbe kwa upendo wa Mungu usioonekana, katika Kristo.