Kuitwa kuteseka na kufurahi: Ili tuweze kumpokea Kristo
Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana! Mimi kuwaandikia mambo yale yale hakuniudhi, kwa maana ni kinga kwa ajili yenu. Jihadharini na mbwa, wale watenda maovu, jihadharini na wale wajikatao miili yao, wasemao ili kuokoka ni lazima kutahiriwa. Kwa maana sisi ndio tulio tohara, sisi tumwabuduo Mungu katika Roho, tunaona fahari katika Kristo Yesu, ambao hatuweki tumaini letu katika mwili, ingawa mimi mwenyewe ninazo sababu za kuutumainia mwili. Kama mtu ye yote akidhani anazo sababu za kuutumainia mwili, mimi zaidi. Nilitahiriwa siku ya nane, mimi ni Mwisraeli wa kabila la Benyamini, Mwebrania wa Waebrania. Kwa habari ya sheria, ni Farisayo, kwa habari za juhudi, nilikuwa nalitesa kanisa, kuhusu haki ipatikanayo kwa sheria, mimi nilikuwa sina hatia. Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, sasa nayahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara tupu nikiyangalinisha na faida kubwa ipitayo kiasi ya kumjua Kristo Yesu Bwana wangu, ambaye kwa ajili Yake nimepata hasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nimpate Kristo, nami nionekane mbele Zake nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu kwa njia ya imani. Nataka nimjue Kristo na uweza wa kufufuka Kwake na ushirika wa mateso Yake, ili nifanane naye katika mauti Yake, ili kwa njia yo yote niweze kufikia ufufuo wa wafu. Kukaza Mwendo Ili Kufikia Lengo Si kwamba nimekwisha kufikia, au kwamba nimekwisha kuwa mkamilifu, la hasha! Bali nakaza mwendo ili nipate kile ambacho kwa ajili yake, nimeshikwa na Kristo Yesu. Ndugu zangu, ijihesabu kuwa nimekwisha kushika. Lakini ninafanya jambo moja: Ninasahau mambo yale yaliyopita, nakaza mwendo kufikia yale yaliyo mbele. Nakaza mwendo nifikie ile alama ya ushindi iliyowekwa ili nipate tuzo ya mwito mkuu wa Mungu ambao nimeitiwa huko juu mbinugni katika Kristo Yesu.
Biblia Anaahidi Mateso kwa Watu wa Mungu
Wiki hii tunaangazia haja ya kujitayarisha kwa mateso. Sababu ya hii sio tu hisia zangu kuwa ni nyakati za uovu na njia ya haki ni ya gharama, bali ahadi ya Biblia kuwa watu wa Mungu watateseka.
Kwa mfano, katika Matendo 14:22, inasema kuwa Paulo aliwaambia makanisa yake yote machanga, “Inatupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa kupitia katika taabu nyingi.” Na Yesu alisema, “Kama wamenitesa mimi, nanyi pia watawatesa,” (Yohana 15:20). Na petro akasema, “Wapenzi, msione ajabu katika yale mateso yanayotukia miongoni mwenu, kana kwamba ni kitu geni kinachowapata” (1Petro 4:12). Ni kusema si geni; inafaa itarajiwe. Na Paulo anasema (katika 2 Timotheo 3:12), “Naam, yeyote anayetaka kuishi maisha ya utauwa ndani ya Kriso Yesu atateswa.”
Hivyo nalichukua kama ukweli wa biblia na vile tunazidi kushawishika zaidi juu ya kuwa chumvi wa dunia na nuru ya ulimwenguni, na kuwafikia watu wa ulimwengu ambao hawajafikiwa, na kufunuakazi za giza, na kufungua vifungo vya dhambi na shetani, ndivyo tutaendelea kuteseka. Ndio maana inafaa tujitayarishe. Na ndio maana ninahubiri wiki hii kutoka kwa maandiko yatakayotusaidia kujiandaa.
Ujumbe unashughulikia makusudio manne Mungu anayo katika mateso yetu katika huduma yake. Moja ni kusudio la kimadili ama kiroho: kupitia mateso tunatumainia kwa ukamilifu zaidi kwa Mungu na kuweka tumaini dogo kwa vitu vya ulimwengu. Ya pili, kunayo kusudio la mshikamano; tunakuja kufahamu Kristo zaidi tunaposhiriki katika mateso yake. Ndio mtazamo wetu leo.
Lengo la mshikamano mkuu pamoja na Kristo
Mungu anatusaidia kujiandaa kwa mateso kwa kutufundisha na kutuonyesha kwamba kupitia mateso tunastahili kuingia kwa undani katika uhusiano wetu na Kristo. Unapata kumfahamu vyema unaposhiriki katika uchungu wake. Wale ambao wanaandika kwa undani sana na kwa njia nzuri kuhusu dhamana ya Kristo ni wale ambao wameingia pamoja naye kwa undani katika mateso.
Mateso katika maisha ya Jerry Bridges
Kwa mfano, kitabu cha Jerry Bridges, Kumtumainia Mungu, Hata kama Maisha inaumiza, ni kitabu kilicho cha ndani na chenye usaidizi juu ya mateso na kwenda kwa undani pamoja na Mungu kupitia mateso. Na si ajabu kujifunza kwamba wakati alikuwa na umri wa miaka 14, alisikia mamake akiitana kutoka kwa chumba kilichokuwa karibu, bila kutarajia kabisa, na akafika kumwona akipumua pumzi yake ya mwisho. Vile vile yuko na hali ya kimaumbile ambayo inamzuia kushiriki kwenye michezo ya kawaida. Na miaka michache iliyopita bibiye alikufa kutokana na ugonjwa wa saratani. Kumtumikia Mungu pamoja na watembezi hakujamfanya kutokuwa na uchungu. Anaandika kwa undani kuhusu mateso kwa sababu ameenda ndani pamoja na Yesu katika mateso.
Mateso katika maisha ya Horatius Bonar
Zaidi ya miaka mia moja iliyopita, Horatius Bonar, mchungaji mwenye asili ya Uingereza na mwandishi wa nyimbo, aliandika kijitabu kiitwacho Usiku wa Kilio, ama “Wakati wana wa Mungu wanateseka.” Ndani mwake alisema lengo lake lilikuwa, “kuhudumia watauwa . . . kutafuta kubeba mizigo yao, kuponya vidonda vyao, kupanguza angalau baadhi ya machozi yao.” Ni kijitabu chorororo, na cha ndani na chenye hekima. Basi si ajabu kumsikia akisema,
Kimeandikwa na yule ajitafutaye kufaidi kupitia jaribu, na kutetemeka ndipo isije ikapita kama upepo unaovuma juu ya mwamba, na kuuacha ngumu vile ulivyokuwa; kupitia yule ambaye kwa kila hali ya huzuni angesogelea Mungu ili amjue zaidi, na yule hayuko tayari kukiri ajuavyo kwa kuwa bado ni kidogo.
Bridges na Bonar wanatuonyesha kuwa mateso ni njia iliyo kilindini mwa moyo wa Mungu. Mungu ana ufunuo sahihi ya utukufu wake kwa ajili ya wanawe wanaoteseka.
Maneno ya Ayubu, Stefano na Petro
Baada ya miezi ya mateso, Ayubu hatimaye anamwambia Mungu, “Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako, lakini sasa macho yangu yamekuona” (Ayubu 42:5). Ayubu alikuwa amekuwa mtu wa kumcha Mungu na tena mwongofu, aliyependeza machoni mwa Mungu, lakini tofauti ya yale alijua juu Yake kwa maendeleo na ukuu ilikuwa tofauti kati ya kumsikia na kumwona.
Wakati Stefano aliposhikwa na kuwekwa chini ya majaribu kwa sababu ya imani yake na alipopewa nafasi kuhubiri, matokeo ni kwamba viongozi wa kidini walighadhabika na wakamsagia meno Stefano. Walikuwa tu karibu kumvuruta nje ya mji na kumwua. Kwa muda huo, Luka anatuambia, “Stefano akiwa amejazwa na Roho Mtakatifu, alikaza macho mbinguni, akaona utukufu wa Mungu naye Yesu akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu” (Matendo 7:55). Kuna ufunuo halisi, mshikamano halisi, uliotayarishwa kwa wale wanateseka pamoja na Kristo.
Petro anaiweka kwa njia hii, “Kama mkilaumiwa kwa ajili ya Jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa sababu Roho wa utukufu, yaani, Roho wa utukufu ambaye ndiye Roho wa Mungu, anakaa juu yenu” (1 Petro 4:14). Kwa maneno mengine Mungu anatenga kuja na kuishi maalum kwa Roho Wake na utukufu wake juu ya wana wake wanaoteseka kwa ajili ya Jina Lake.
Mitazamo mitatu kutoka kwa andiko
Basi angazo la ujumbe wa leo ni juu ya hali hii ya mshikamano katika mateso. Mojawapo ya malengo ya mateso ya watauwa ni kwamba uhusiano wao na Mungu usiwe ya kupangwa sana na usiwe ule usio ya kimaumbile na usio wa mbali na kuwa moja kwa moja, na ya hakika na ya kushikamana na ya karibu na ya ndani zaidi.
Katika andiko letu (Wafilipi 3:5-11) nataka tuone mambo yasiyopungua matatu:
Ya kwanza, matayarisho ya Paulo kuteseka kwa kubadilisha maadili yake;
Ya pili, vile Paulo anakumbana na mateso na kupoteza kama gharama ya utiifu wake kwa Kristo;
Ya tatu, lengo la Paulo katika haya yote, kusema, kumpokea kristo: kumjua na kuwa ndani yake na kushiriki kwa mshikamano zaidi na hakika kuliko vile alijua pamoja na marafiki yake Barnaba na Sila.
1) Matayarisho ya Paulo kuteseka
Katika mstari wa 5 na 6 anaandika tofauti za yale aliyoyafurahia kabla ya kuwa Mkristo. Anapeana mtazamo wake wa kikabila kama shina kamili ya Abrahamu, Muhibrania wa Waebrania. Hii inamleta faida kuu, hisia kuu ya umuhimu na hakikisho. Alikuwa Mwisraeli. Baadaye anataja mambo matatu yanayoenda hadi ndani ya moyo wa maisha ya Paulo kabla awe Mkristo (mwishoni mwa mstari wa 5): “Kwa habari ya sheria, ni Farisayo, kwa habari za juhudi, nilikuwa nalitesa kanisa, kuhusu haki ipatikanayo kwa sheria, mimi nilikuwa sina hatia.”
Maadili ya Paulo kabla kukutana na Kristo
Hii ndiyo ilikuwa maisha ya Paulo. Hii ndiyo iliyompatia maana na hadhi. Hii ndiyo ilkuwa faida kwake, bahati yake, furaha yake. Mipigo tofauti kwa watu tofauti—na ya Paulo ni kuwa alikuwa katika cheo cha juu ya wahifadhio sheria, Wafarisayo, na kati yao alikuwa mwenye shauku kuu hata aliongoza njia ya kutesa mahasidi wa Mungu, kanisa la Yesu, na alizitii sheria kwa hali ya juu. Alipigwa mijeledi kwa kuwa, alipigwa mijeledi kwa kufanikiwa, alipigwa mijeledi kutoka kwa Mungu—ama ni hivyo alivyodhania—kwa ajili ya kutii kwake sheria bila dosari.
Na alikutana na Kristo, Mwana wa Mungu aishiye, njiani kuelekea Damaski. Kristo alimwambia vile atateseka (Matendo ya Mitume 9:16). Na Paulo alijitayarisha.
Paulo alihesabu thamani yake ya awali kama hasara
Vile alijitayarisha imeelezwa katika mstari wa 7. “Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, sasa nayahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.” Paulo anaangalia msimamo wake katika hadhi ya juu ya jumuia ya kidini, Wafarisayo; anangalia utukufu kuwa juu ya kikundi hicho pamoja na mipigo yote na kushangilia; anaangali jitihada ya kuzitii sheria kwake na hali ya kiburi ya maisha aliyoifurahia; na anajiandaa kuteseka kwa kuchukua maisha yake yote na kuigeuza juu chini, kwa kugeuza maadili yake: “Yale yaliyokuwa faida kwangu [mstari wa 5-6], sasa nayahesabu kuwa hasara.”
Kabla awe Mkristo alikuwa na kitabu cha hesabu kilichokuwa na vipande viwili: moja uliokuwa ukisema, faida, na mwingine uliokuwa ukisema hasara. Upande wa hasara kulikuwa na jambo mbaya kuwa vuguvugu huu wa Yesu yaweza pita mpaka na Yesu kujidhihirisha kuwa hakika na kupata ushindi. Alipokutana na Kristo aishiye njiani akielekea Damaski, Paulo alichukua kalamu kubwa nyekundu na kuandika “HASARA” kwa herufi kubwa nyekundu juu ya upande wa kitabu ulioandikwa faida. Na akaandika “FAIDA” kwa herufi kubwa juu ya upande wa hasara ambao ulikuwa na jina moja tu kwalo: Kristo.
Na si tu hiyo, vile Paulo alivyofikiri zaidi juu ya thamani kamili ya uhai duniani na ukuu wa Kristo, alienda zaidi ya mambo machache yaliyotajwa katika mstari wa 5-6 na kuweka kila kitu isipokuwa Kristo katika huo upande wa kwanza: Mstari wa 8: “Zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara tupu nikiyalinganisha na faida kubwa ipitayo kiasi ya kumjua Kristo Yesu Bwana wangu.” Alianza kuyahesabu yaliyo ya thamani aliyoyafanya kama hasara, na akamaliza kwa kuhesabu kila kitu kama hasara, isipokuwa Kristo.
Ukristo wa kawaida
Hiyo ndiyo ilimaanisha kwa Paulo kuwa Mkristo. Na ndipo yeyote miongoni mwetu akadhani alikuwa wa ajabu ama kutojulikana, tazama kuwa katika mstari wa 17 anasema kwa nguvu zake zote za utume, “Ndugu zangu, kwa pamoja fuateni mfano wangu.” Hii ni Ukristo wa kawaida.
Kile Paulo anafanya hapa ni kuonyesha vile mafundisho ya Yesu yafaa yaishiwe. Kwa mfano, Yesu alisema, “Ufalme wa Mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani, ambayo mtu mmoja alipoiona akaificha tena. Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akainunua lile shamba” (Mathayo 13:44). Kuwa Mkristo kunamaanisha kugundua kuwa Kristo (Mfalme) ni kifua cha hazina ya furaha takatifu na kuandika “HASARA” juu ya vitu vingine vyote vya ulimwengu ili umpokee. “Aliuza vyote alivyokuwa navyo ili akainunue lile shamba.”
Ama tena katika Luka 14:33 Yesu alisema, “Yeyote miongoni mwenu ambaye hawezi kuacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.” Kwa maneno mengine, kuwa mwanafunzi wa Yesu kunamaanisha kuandika “HASARA” kwa herufi kubwa nyekundu juu ya vitu vyako vyote—na vyote dunia hii vyapeana.
Yale haya yanamaanisha kwa vitendo
Sasa haya yanamaanisha nini kwa kawaida? Nadhani yanamaanisha vitu vinne:
Inamaanisha kuwa kila mara ninapoitwa kuchagua kitu chochote hapa duniani na Kristo, nachagua Kristo.
Inamaanisha kuwa nitakabiliana na vitu vya duniani hii kwa njia zinazonisogelesha kwa Kristo ili nipate kupokea uwingi wa Kristo na kufurahia mengi kutoka kwake kupitia vile ninavyotumia ulimwengu.
Inamaanisha kuwa nitakabiliana na vitu vya dunia hii kwa njia ambazo zinaonyesha si hazina yangu, bali kuonyesha kuwa Kristo ndiye hazina yangu.
Inamaanisha kuwa nikipoteza moja ama vitu vyote ambavyo dunia hii yaweza peana, sitapoteza furaha yangu ama hazina yangu ama uhai wangu, kwa sababu Kristo ni yote.
Basi huo ni mwito ambao Paulo aliuitikia rohoni mwake (mstari wa 8): “Nayahesabu mambo yote kuwa hasara tupu nikiyalinganisha na faida kubwa ipitiayo kiasi ya kumjua kristo Yesu Bwana wangu.” Kristo ni yote na yote yale ni hasara.
Kwa nini hii ni njia ya kujiandaa kuteseka?
Wacha tusimame nyma kwa dakika na tupate mielekeo. Bado nashughulika na hoja ya kwanza: iitwayo, kuwa hii ni njia ya kujitayarisha kwa Paulo kuteseka. Kwa nini nasema hiyo? Kwa nini kuwa Mkristo na kuandika “HASARA” juu ya kila kitu maishani mwako isipokuwa Kristo, njia ya kujitayarisha kuteseka?
Jibu ni kwamba kuteseka ni bure isipokuwa kuachilia mambo mazuri au mabaya ambayo dunia yapeana kwa ajili ya furaha—hadhi, kujiinua kati ya rika, kazi, pesa, mchumba, maisha ya ngono, watoto, marafiki, afya, nguvu, kuona, kusikia, kufanikiwa na kadhalika. Vitu hivi vinapochukuliwa (kwa nguvu, kwa hali fulani ama kwa hiari), tunateseka. Lakini kama tumefuata Paulo na mafundisho ya Yesu na tayari tumeyahesabu kama hasara tukiyalinganisha na faida ya kumpokea Kristo, basi tuko tayari kuteseka.
Kama wakati unakuwa Mkristo uandike “HASARA” kwa herufi nyekundu juu ya vitu vyote duniani isipokuwa Kristo, basi Kristo anapokuita kuacha baadhi ya vitu hivyo, si ya kushangaza ama isiyo ya kutarajiwa. Uchungu na huzuni unaweza kuwa mkuu. Machozi yanaweza kuwa mengi, vile yalivyokuwa kwa Yesu kule Gethsemane. Lakini tutakuwa tayari. Tutajua kuwa thamani ya kristo yapita vitu vyote ulimwengu unaweza kutupa na kwa kuvipoteza tunapokea Kristo kwa wingi.
2) Kukumbana na mateso kwa Paulo
Basi katika nusu ya pili ya mstari wa 8 Paulo anasonga kutoka kwa kujitayarisha kuteseka hadi kuteseka kwenyewe. Anatoka kutoka kwa kuhesabu vyote kuwa bure katika nusu ya kwanza ya mstari wa 8 hadi katika kupatwa na hali ya kupoteza vyote katika nusu ya pili wa mstari “ . . . ambaye kwa ajili Yake [huyo ni Kristo] nimepata hasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nimpate Kristo.” Tutaona haya wiki unaofuata: Paulo alishashuhudia hasara yenyewe ya faida ya kawaida na starehe za dunia ambapo angesema kuwa kuwa hakuwa anahesabu tu hasara ya vitu; alikuwa akipata hasara. Alishajitayarisha kwa kugeuza thamani yake juu chini, na sasa alikuwa akijaribiwa. Je, alimthamini Kristo juu ya yote?
3) Lengo la Paulo (na kusudi la Mungu) katika mateso
Wacha nitamatishe kwa kushikilia fikira zetu kwa lengo la Paulo na kusudi la Mungu katika mateso haya. Kwa nini Mungu aliteua na Paulo kukubali hasara ambayo iliyomaanisha kwa yeye kuwa Mkristo?
Paulo anapeana majibu mara kwa mara katika mistari hii ndipo tusipate kukosa hoja. Hayuko yahe katika kupata hasara hii. Ana lengo. Na lengo lake ni kumjua Kristo.
Mstari wa 7: “Nayahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.”
Mstari wa 8a: “Nayahesabu mambo yote kuwa hasara tupu nikiyalinganisha na faida kubwa ipitiayo kiasi ya kumjua Kristo Yesu bwana wangu.”
Mstari 8b: “Kwa ajili Yake nimepata hasara ya mambo yote.”
Mstari 8c: “Nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nimpate Kristo . . . .”
Mstari 9: “Nami nionekane mbele Zake [nisiwe na haki yangu bali ya kutoka kwa Mungu] . . . “
Mstari 10a: (bado kupeana lengo lake la kukubali hasara ya vyote) . . . . nataka nimjue
Mistari 10b-11: (Ukifuatwa na vitu vinne ya vile inamaanisha kumjua Kristo)
“ . . . [kujua] uweza wa kufufuka Kwake”; na
“Ushirika wa mateso yake” ;
“Kufanana naye katika mauti Yake” ;
“Ili kwa njia yoyote niweze kufikia ufufuo wa wafu.”
Kwa maneno mengine, kile kinadumisha Paulo katika kupoteza vyote ni hakika kwamba kwa kupoteza vitu vyenye thamani duniani anapata kitu chenye thamani zaidi—Kristo.
Mara mbili hiyo kufaidika kunaitwa kujua— Mstari 8a “. . . nikiyalinganisha na faida kubwa ipitayo kiasi ya kumjua Kristo Yesu Bwana wangu.” Mstari wa 10: “Ndipo nimjue.” Hii ndiyo jambo ya mshikamano katika mateso. Je, twataka kumjua? Je, tunataka kuwa karibu naye na ndani naye na hakika naye na kushikamana naye—kwa wingi mpaka tunahesabu vyote kama hasara ili tupate kupokea hazina hii kuu kuliko yote?
Kama tunataka, tutakuwa tayari kuteseka. Kama hatutaki, itatuchukua na bumbwazi na tutaasi. Na Mungu akayafumbue macho yetu kwa thamani ya kupita yote ya kumjua Kristo!