Kudumishwa kwa neema kuu—milele
Hata sasa asema Bwana Mungu wa Israeli juu ya mji ambao mnasema “Kwa upanga, njaa na tauni,mji utatiwa mkononi mwa mfalme wa babeli” 37 "Hakika nitawakusanya kutoka nchi zote nilizowafukuzia katika hasira yangu kali, na ghadhabu yangu kuu, nitawarudisha mahali hapa na kuwaruhusu waishi kwa salama. 38 Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao. 39 Nitawapa moyo mmoja na kutenda pamoja, ili kwamba waniche daima kwa mema yao wenyewe na kwa mema ya watoto wao baada yao. 40 Nitafanya nao agano la milele; kamwe sitaacha kuwatendea mema, nami nitawavuvia kunicha mimi, ili kwamba kamwe wasigeuke mbali nami. 41 Nitafurahia kuwatendea mema, na kwa hakika nitawapanda katika nchi hii kwa moyo wangu wote na roho yangu yote.” 42 Hili ndilo asemalo Bwana, “Vile nilivyoleta maafa haya makubwa kwa watu hawa, ndivyo nitakavyowapa mafanikio niliyowaahidi.”
Neema idumishayo ni nini?
Tunasherekea miaka 125 ya kudumishwa kwa neema ya Mungu. Nini hiyo? Neema idumishayo ni nini? Wacha ni uweke kama shairi yenye mistari minne:
Si neema ya kuzuilia yale ambayo si furaha ya wokovu,
Wala kutoroka kwa matatizo, lakini hii:
Neema ambayo inaamrisha shida na uchungu wetu,
Na baadaye, katika giza, ipo kudumisha.
Nasisitiza hili kwa sababu kusherehekea neema ambayo inazuia yale ambayo si furaha ya wokovu, na kupa kupaa kutoka kwa matatizo yote na haiamrishi uchungu wetu inaweza kuwa uwongo kibiblia na wa kutoaminika.
. . . Kuhusishwa katika ajali mbaya
Matukio yetu na biblia hutufunza kuwa neema hauzuii uchungu, bali huamrisha na kupanga na kupima uchungu wetu, na katika giza, ipo kudumisha. Kwa mfano, jana Bob Ricker, Rais wa kongamano ya Ujumla ya Ubatizo, aliongea kuhusu kumbukumbu yenye thamanai ya neema ya kudumisha ya Mungu. Takriban miaka kumi iliyopita, Bob na mwanawe Dee wa kike walihusika katika ajali mbaya ya gari. Yuko hai leo kwa sababu moja. Kwenye gari lililokuwa nyuma yake, kulikuwa na daktari ambaye alikuwa na mrija wa hewa wakati wa tukio hilo. Wakati alimfikia alikuwa ameanza kupoteza fahamu. Aliuweka mrija huo kwa nguvu kwenye koo lake na kuweza kuokoa maisha yake. Miaka kadhaa kwa harusi yake, Bob alimwambia: hizo kovu za uso, utaishi nazo kama kumbukumbu ya neema idumishayo.
Hakika Bob Ricker si mpumbavu. Anajua kama Mungu aliratibisha kile kilichoko ndani ya gari la nyuma kuwa daktari, na huyu daktari awe na chombo cha kupumua mfukoni mwake, na awe na ufahamu wa kukitumia kuokoa maisha, basi Mungu ana uwezo mkuu kuzuia ajali isitendeke. Mwanzo Bob ananukuu Waefeso 1:11, “katika Kristo sisi nasi tumepata urithi, tukisha kuchaguliwa sawasawa na kusudi la Mungu, Yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na mapenzi yake”. Na anasisitiza; “Vitu vyote, vinamaanisha vitu vyote” – inajumulisha pia njia za magari na ndege na mishale na risasi. Hilo ndilo himizo la shairi langu fupi, “Neema idumishayo ni nini?”
Si neema ya kuzuilia yale ambayo si furaha ya wokovu
Wala kutoroka kwa matatizo, lakini hii:
Neema ambayo inaamrisha shida na utungu wetu,
Na baadaye, katika giza, ipo kudumisha.
. . . Gari inapoharibika
Siku ya Jumamosi, wiki mbili iliyopita, Noeli, Abrahamu, Barnaba, na Talitha walikuwa wakisafiri kuelekea Georgia gari lao lilipoharibika kwenye barabara ndefu usiotumiwa na watu wengi, kwa muda wa lisali moja, kusini mwa Indianapolis. Rejeta (radiator) ya gari ililipuliwa. Mkulima ambaye umri wake ni kama miaka sitini na tano akasimama kuwapa usaidizi. Noeli akasema kilichohitajika ni kuwa wapate pahali pa kujilaza na watarajie kuwa ifikapo siku ya jumatatu asubuhi labda wangeweza kupata karakana ambayo imefunguliwa kwa ajili ya gari lao. Mkulima akauliza, “Je, mnaweza kaa pamoja name na bibi yangu?” Noeli akasita na hataki kuwakataa, Mkulima akamwambia, “Bwana asema kuwa tukitumikia wengine, ni sawasawa na kumtumikia”. Noeli akasema, “sawa, tunaweza kuenda kanisani pamoja nanyi ifikapo asubuhi?” Akasema , “Kama mnaweza kushiriki kwa Kanisa la Ubatizo.”
Basi wakakaa pamoja na mkulima, ambaye ni fundi wa ndege, na akachunguza shida ya gari, siku ya Jumatatu akaenenda jijini akanunua rejeta ya gari, akawawekelea bila malipo yoyote na akawaaga nao wakaenda zao. Wakati huo Barnaba akatoa nduwano kutoka kwa gari hilo na akavua mlamba kiasi cha inchi kumi na tisa kwa urefu-kama kumbukumbu ya mema yaliyotukia.
Mungu anayeweza kufanya mkulima kusimama na kusaidia Noeli na ambaye anahakikisha kuwa ni Mkristo (hata wa Dini la Ubatizo), na tena Mkulima pamoja na bibiye wanawapa chumba cha kujilaza, na ni fundi, na anahakikisha kuwa kitu cha kwanza asubuhi ya Jumatatu anawatafutia tangi rejeta ya gari, na tena anakubali kuchukua muda wake, tena yuko na bwawa lililo mlamba- huyu Mungu ana uwezo isiyo na kifani kuweza kuzuilia tangi la maji rejeta lisipasuke katikati mwa mji wa Indiana.
. . . Wakati uponyo haufanyiki
Lakini katika ulimwengu huu wa kutafuta bila mafanikio, hiyo sio yote ambayo neema ya kudumisha hutenda.
Si neema ya kuzuilia yale ambayo si furaha ya wokovu,
Wala kutoroka kwa matatizo, lakini hii:
Neema ambayo inaamrisha shida na utungu wetu,.
Na baadaye, katika giza, ipo kudumisha.
Mmoja wa vijana katika kanisa letu anapita katika maji makuu kwa wakati huu-ambayo inajaribu imani yake hadi mwisho. Aliniambia hivi majuzi, ingelikuwa rahisi kama Yesu hangeliponya na badala yake angelipeana neema ya kustahimili kukosa kwa uponyo. Jambo moja ambalo nilimwambia ni hili. Hilo ndilo Yesu alilolitenda - na kwa sababu hiyo- katika kitabu cha 2 Wakorintho 12:9-10. Neema ya Mungu inaratibisha kuwa Paulo ana mwiba kwa nyama kwa ajili ya ukarimu wake na tena hatautoa kwa mujibu kwa jibu la ombi. Lakini akasema,
Neema Yangu [inaodumisha] inakutosha, kwa kuwa uweza wangu hukamilika katika udhaifu.
Na Paulo anajibu,
Kwa hiyo nitajisifu kwa furaha zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. 10 Hii ndiyo sababu, kwa ajili ya Kristo,nafurahia udhaifu, katika kutukanwa, katika taabu, katika mateso, na katika shida, kwa maana ninapokuwa dhaifu, ndipo nina nguvu.
Si neema ya kuzuilia yale ambayo si furaha ya wokovu,
Wala kutoroka kwa matatizo, lakini hii:
Neema ambayo inaamrisha shida na utungu wetu,
Na baadaye, katika giza, ipo kudumisha.
. . . Wakati kanisa linaungua
Siku ya Jumatatu, Mechi, Tarehe 16, 1885, wakati Kanisa la Ubatizo wa Bethlehemu lilikuwa na miaka kumi na minne na lilikuwa limejengwa katika msunguko wa barabara la 12th Avenue na njia ya 6th street (pahali ambapo kwa sasa kuna kampuni kwa jina, Douglas Company) kanisa lilishika moto. Liliungua kwa kiasi ya kutoweza kufanyiwa ukarabati. Lakini katika giza huo, kulikuwa na neema ya Mungu ya kushangaza. Upande wa paa pahali wazima moto walikuwa wamesimama ndiyo iliyokuwa imebaki bila kuanguka. Kwa muda wa wiki saba, kanisa lilinunua jengo la Second Congregational Church, pahali ambapo tuliabudu kwa takriban miaka 106 mpaka jengo hili lilipomalizika mwaka wa 1991.
Sasa Mungu ambaye anaweza hifadhi maisha ya wazima moto kwa kushika pande la paa ambalo ni dhaifu, na tena ambaye anaweza kupangia jengo jipya na la kifahari kwa muda wa wiki saba, si angezuilia moto kuzuka pia. (?? Paragraph/missing sentence)
Neema ambayo inaamrisha shida na utungu wetu,
Na baadaye, katika giza, ipo kudumisha.
Mungu kila mara huwa hazui majanga
Andiko katika Yeremiah 32 ni juu ya hii neema ya kudumisha, na inashikilia ufunguo wa kuwa hai kwa kanisa la Ubatizo wa Bethlemu jijini miaka 125 baada ya majaribio.Yerusalemu na wateule wa Mungu wako katika giza na taabu. Mungu mwenyewe ndiye Yule ambaye ameamrisha iwe hivyo. Tazama mstari wa 36: “Hata sasa asema BWANA Mungu wa Israeli kuhusu mji huu mnasema kuihusu, “Kwa upanga , njaa na tauni , mji utatiwa mkononi mwa wafalme Babeli.” Hivyo ndivyo wanasema kuihusu. Na ni kweli. Neema ya Mungu haijawaepusha na janga hili. Vivyo hivyo neema ya Mungu hautakuepusha na janga uliowekewa.
Lakini kile wanasema kuhusu wateule wa Mungu sio neno la mwisho. Mungu analo neno la mwisho. Na ni neno la neema. Mstari 37: “Hakika nitawakusanya kutoka nchi zote nilizowafukuza katika hasira yangu kali, na ghadhabu yangu kuu, nitawarudisha mahali hapa na kuwaruhusu waishi kwa salama.” Mungu anasisitiza kuwa aliamrisha shida na uchungu. “Nimewaondosha” kwa nchi hizi za kigeni. Na anasisitiza tena kuwa yeye mwenyenye atawaondoa na kuwarudisha kwake na kwa shamba lao. Ni kumaanisha kuwa, neema kuu, hatimaye itashinda dhidi ya janga.
Tunawezaje kuwa na hakika wa ushindi wa neema?
Tunawezaje kuwa na uhakika kuhusu ushindi wa neema? Kama Mungu ni Mungu wa haki ni nani anayeweza kutuma Israeli katika utumwa, pahali wengi wanapotea kwa sababu ya dhambi zao na kutotii, basi inawezekanaje tuwe na ujasiri kuwa haya hayatatendeka kwa wateule wa Mungu wa wakati huu-Kanisa bi harusi wa Kristo, Israeli wa kweli, wewe na mimi, ambao wameitwa katika ushirika wa Mwanawe? Ni swali moja la kuuliza: kwa nini Bethlehemu ilistahimili kwa miaka 125? Lakini swali la dharura ni, Je tunaweza kuwa na uhakika kuwa neema itashindania Bethlehemu na katika maisha yetu ya kibinafsi wakati wa usoni? Unawezaje kuwa na uhakika kuwa neema itakudumisha hadi tamati kwa imani na utakatifu ikupelekayo mbinguni salama?
Arafa ufuatayo ni kuhusu hii. Jibu ni: neema ya kudumisha kwa wateule wa Mungu ni neema kuu. Hivyo ni kusema, neema ya kudumisha ni neema usiokoma. Ni neema inayoshinda dhidi ya visingiti na kuhifadhi imani na utukufu ambao unatuleta kwa makao yetu mbinguni. Hili pekee ndilo ujasiri wetu wa hakika kwa siku za usoni. Wewe pamoja nami, kivyetu, tu wadhaifu na rahisi kubadilisha. Kama tungeachwa kuvumilia kwa nguvu zetu, tungepotosha imani yetu, ni hakika. Ndiyo maana watakatifu wameomba kwa karne.
Kwa nema, mwenye deni amefanyika mkuu.
Kila siku nimefanyika kuwa!
Wacha wema wako kama kifungio
Ufunge moyo wangu ambao unayumbayumba, Kwako:
Umefanyika kuyumbayumba, Bwana ninauhisi,
Umefanyika kuacha Mungu ninayempenda;
Huu hapa moyo wangu, E, Bwana uuchukue na kuifunga;
Uufunge kwa ajili ya mahakama yako ya juu.
Ni hivyo ndivyo watakatifu wanapaswa kuomba? Hivyo ndivyo njia ya kuombea siku zako za usoni na za Bethlehemu? Je ni njia ya kuomba inayo ambatana na biblia? Fanya wema wako kama kifungo- mnyororo- ufungao moyo wangu unaoyumbayumba kwako. Funga roho yangu na kifungo ambacho hakiwezi kufunguliwa, kwa ajili ya mahakama ya mbingu. Kwa tafsiri nyingine. Niweke! Nihifadhi! Shinda uasi unaoinuka! Shinda tashwishi yote! Komboa kutoka kwa jaribu lolote la kuharibu! Vunja anasa za kimauti! Dhihirisha uwongo zote za kishetani! Vunja maneno yote yasiyofaa! Niumbe! Niinue! Nishike! Nifahamu! Fanya chochote ambacho unaweza kukifanya kwa ajili ya kunifanya niendelee kukuamini na kukuucha mpaka Yesu atakapokuja ama kuita. Inafaa-inatupasa- tuimbe na kuomba hivyo?
Jibu la arafa huu ni ndio. Jinsi ya kuimba na kuomba imekita mizizi katika ahadi ya agano jipya la neema kuu inayodumisha. Wacha tukausome. Tia hii akilini; hii ni mojawapo wa ahadi ya agano la kale kuhusu agano jipya ambalo Yesu alisema kuwa aliifunga kwa damu yake kwa wale wote waliodumu ndani Mwake. Sio tu kwa Wayahudi, ila kwa Wayahudi wa kweli ambao wameunganishwa na Yesu kupitia uzao wa Abrahamu (Wagalatia 3:7, 16). Yeremia 32:38-41 unasema,
Watakuwa wangu nami Nitakuwa Mungu wao. 39 Nitawapa moyo mmoja na kutenda pamoja, ili kwamba waniche daima kwa mema yao wenyewe na kwa mema ya watoto wao baada yao.40 Nitafanya nao agano la milele; kamwe sitaacha kuwatendea mema, nami nitawavuvia kunicha mimi, ili kwamba kamwe wasigeuke mbali nami. 41 Nitafurahia kuwatendea mema, na kwa hakika nitawapanda katika nchi hii kwa moyo wangu wote na roho yangu yote.
Ahadi nne za neema kuu unaodumisha
Tazama ahadi nne za neema kuu unaodumisha.
1. Mungu atakuwa Mungu wetu
Mungu anaahidi kuwa Mungu wetu. Mstari 38: “Watakuwa watu wangu nami niwe Mungu wao.” Ahadi zake zote kwa watu wake zimejumulishwa hapa: “Nitakuwa Mungu wenu.” Hivyo ni kusema, Nitatumia yote nilivyo kama Mungu-hekima zangu zote, nguvu zangu zote, upendo wangu wote-ili nione kuwa mmebaki watu wangu. Vyote nilivyo kama Mungu, nayasisitiza kwa wema wenu.
2. Mungu anaahidi kubadilisha mioyo yetu
Mungu anaahidi kubadilisha mioyo yetu na kutufanya tumpende na kumcha. Mstari 39: “Nitawapa moyo mmoja na kutenda pamoja, ili kwamba waniche daima…..(mstari 40 sehemu b)nitawavuvia kunicha mimi.” Kwa muktadha mwingine, Mungu hatasimama tu na atutazame kama kwa nguvu zetu, tutamcha, kwa ukuu, na huruma, atatupa mioyo ambayo inatupasa tuwe nayo, na atatupa imani na uoga wa Mungu ituelekazo mbinguni. Hii ni neema kuu inayodumisha. (Tazama Kumbukumbu la torati 30:6, Ezekieli 11:19-20; 36:27.)
3. Mungu anaahidi kuwa hatutageuka kutoka kwake
Mungu anaahidi kuwa hatatugeukia nasi pia hatutamgeukia. Mstari 40: "Nitafanya nao agano la milele; kamwe sitaacha kuwatendea mema, nami nitawavuvia kunicha mimi, ili kwamba kamwe wasigeuke mbali nami. Kwa muktadha mwingine, kazi ya moyo ina nguvu ya kutuhakikishia kuwa hatutamgeukia. Hili ndilo jambo jipya kuhusu agano jipya: Mungu anaahidi kutimiza yale tunakumbana nazo kupitia nguvu zake. Lazima tumche na kumpenda na kumwamini. Anasema, nitahakikisha, “nimewavuvia kunicha mimi.”-sio kuona yale watafanya nayo, “lakini ila tu wasije wakanigeukia.” Hii ni neema kuu unaodumisha.
4. Mungu anaahidi kufanya hiki kwa nguvu ya ajabu
Hatimaye, Mungu anaahidi kufanya hiki kwa nguvu kuu ya kutofikiriwa. Anaweka haya kwa njia mbili, moja mwanzoni mwa mstari wa 41: “Nitafurahia kuwatendea mema, na kwa hakika nitawapanda katika nchi hii kwa moyo wangu wote na roho yangu yote." Kwanza anasema atasisitiza neema kuu unaodumisha kwa furaha: Nitafurahia kuwatendea mema.” Halafu anasema (mwishoni mwa mstari 41) atasisitiza neema kuu unaodumisha "kwa moyo [wake] wote na roho [yake] yote."
Mungu Yuko na ari kuu ya kiwango gani kukutendea mema?
Anafurahia kukudumisha na anafurahia kwa moyo wake wote na roho (nafsi) yake yote. Sasa nakuuliza, siyo kwa mafundisho ambayo yamepita kiasi, maneno ya kupapasa ama kwa hisia ya maneno mengi- nakuuliza, nakupa changamoto, unaweza tafakari kiwango cha ari ambao ni kuu kuliko ari iliyopata motisha kutoka kwa moyo wa Mungu na roho ya Mungu, ukijumulisha hamu ya chakula na ngono na pesa na umarufu na mamlaka na maana na marafiki na ulinzi mioyoni na rohoni mwa wanadamu walioko ulimwenguni- tuseme karibu bilioni sita-na na uweke hiyo ari yote , ujumulisha mioyo na roho mara bilioni sita kwenye nyungu. Unaweza ukauilinganishaje na ari ya Mungu kukutendea mema jinsi imenukuliwa kwa maneno haya, “ kwa moyo Wake wote na kwa roho Yake yote.” Italinganishwa na subano kwa Bahari la Pacific. Kwa sababu moyo na roho wa Mungu hauna kikomo. Na moyo na roho ya binadamu ina mwisho. Hakuna kiwango kikuu kuliko kiwacho cha “Moyo wa Mungu wote na Roho ya Mungu yote.”
Na hicho ndicho kiwango cha furaha anacho ya kukudumisha na neema kuu. “Nitafurahia kuwatendea mema….. kwa moyo wangu wote na roho yangu yote.” Wengine wenu wanaweza kuwa wanaonja utamu wa neema huu kwa mara ya kwanza asubuhi hii. Hiyo ni kazi ya roho mtakatifu maishani mwako, na ninakusihi unyenyekee kwayo na ufahamishwe na neema kuu unaodumisha.
Wale mlioishi katika uhakikisho huu mtamu kwa miongo na mjumuike nami asubuhi hii kufurahia utukufu wa kweli maishani mwetu. Nawaalika muimbe nami, kubariki Baba, Mwana na Roho Mtakatifu kwa neema kuu unaodumisha uliotuhifadhi kama Kanisa kwa miaka 125 na utahifadhi wateule wa Mungu kwa imani mpaka Yesu atakapokuja ama Yesu kuita.
Si neema ya kuzuilia yale ambayo si furaha ya wokovu,
Wala kutoroka kwa matatizo, lakini hii:
Neema ambayo inaamrisha shida na utungu wetu,
Na baadaye, katika giza, ipo kudumisha.
Wacha tukabariki Bwana kwa pamoja na wimbo nambari 9, “ Imba sifa kwa Baba”- na tukifika mstari wa 3, burudika nami katika ukweli kuwa roho huarakisha na kuvuta na kumeza na kutufunga na kutuandaa bila dosari kwa Mungu.