Yafungue macho yangu nipate kuona
Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi, nitalitii neno lako. 18 Yafungue macho yangu nipate kuona mambo ya ajabu katika sheria yako. 19 Mimi ni mgeni duniani, usinifiche maagizo yako. 20 Nafsi yangu inalika kwa shauku kubwa juu ya sheria zako wakati wote. 21 Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa waendao mbali na amri zako. 22 Niondolee dharau na dhihaka, kwa kuwa ninazishika shuhuda zako. 23 Ingawa watawala huketi pamoja na kunisingizia, mtumishi wako atatafakari juu ya maagizo yako. 24 Shuhuda zako ni furaha yangu, nazo ni washauri wangu.
Reli sambamba na njia za nafsi zetu
Tunapoanza mwaka wa 1998, lengo la mungu kwetu sisi ni tutayarishwe katika njia mbili ya gari la moshi ya kuelekea katika utukufu na upendo na huduma na mbingu. Njia hizi mbili ni maombi mbele cha kiti cha enzi cha Mungu na tafakari juu ya neno la Mungu. Wengine wenu wanaweza kumbuka nakala ya pili ya kitjitabu juu ya malengo yetu, “ The Spiritual Dynamics (Njia za kiroho)” inasema,
Tunaungana na Mungu baba kupanua ukuu wa utukufu wake kupitia Bwana wetu Yesu Kristo, kupitia nguvu za Roho Mtakatifu, kwa kuthamini yale yaliyo ya Mungu, kupenda wote anaowapenda, kuombea makusudio yake yote , kutafakari neno lake lote, kudumishwa na neema yake yote.
Kuomba mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na kutafakari Neno la Mungu ni kama reli sambamba linalowezesha gari la nafsi zetu kudumu katika njia itupelekayo kwa utukufu na mbingu. Inatupasa tufanye upya ari yetu ya kuomba na kutafakari juu ya Bilblia kuanzia mwanzoni mwa mwaka. Kila kitu kinazeeka, na kuisha, na kuwa dhaifu bila ya kutoamshwa tena na kufanywa upya na kurudishwa katika hali yake ya zamani. Basi katika wiki ya maombi ya kila mwaka tunatilia mkazo mambo haya makuu na yenye thamani kwa ajili ya kurudisha tena ari ya maombi na neno.
Mambo matatu yakujifunza kutoka Zaburi 119:8
Mwaka huu mambo mawili yanayozingira wiki wa maombi yanaota kutoka kwenye Zaburi 119:18. “Yafungue macho yangu nipate kuona mambo ya ajabu katika sheria yako.” Mstari huu unajumulisha maombi na Neno, na inatupasa tuone vile, ndipo tuyaunganishe kwa njia hii katika maisha yetu na katika kanisa letu. Kuna mambo matatu tunayojifunza kutoka mstari huu.
- Kwanza, ni kwamba kuna mambo ya ajabu katika Neno la Mungu. “Yafungue macho yangu nipate kuona mambo ya ajabu katika sheria yako. “Neno Sheria” ni “Torah” na maana yake ni “agizo” ama “funzo” katika zaburi hii. Kuna mambo ya ajabu katika mafundisho ya Mungu kwetu sisi. Yamkini, ni ya ajabu mno ambapo ukiyaona, yanaweza kukubadilisha na kuinua utakatifu na upendo na malengo yako (2 Wakorintho 3:18). Ndilo sababu kusoma na kujua na kutafakari na kuweka akilini neno la Mungu linakuwa muhimu sana.
- Jambo la pili tunalojifunza katika mstari huu ni kuwa hakuna anayeweza kuona haya mambo ya ajabu pasipo usaidizi kutoka kwa Mungu. “Yafungue macho yangu nipate kuona mambo ya ajabu katika sheria yako.” Mungu asipofungua macho yetu, hatuwezi kuyaona maajabu ya Neno.hatuwezi kuona urembo wa kiroho vile tulivyo. Tunaposoma biblia bila usaidizi kutoka kwa Mungu, utukufu wa Mungu katika mafundisho na matukio katika Biblia ni kama jua imulikayo usoni mwa kipofu. Sio eti kwamba huwezi kufasiri maana yake ya kawaida, lakini huwezi kuona ajabu, urembo, na utukufu wake kiasi cha kushawishi moyo wako.
- Ambacho kinatupeleka kwa jambo la tatu tunalojifunza katika mstari huu, nalo ni, lazima tuombe kwa Mungu kupokea mwangaza wake tunaposoma Biblia. “Yafungue macho yangu nipate kuona mambo ya ajabu katika sheria yako.” Kwa kuwa hatuna uwezo wa kuona urembo wa kiroho na maajabu ya Mungu katika mafundisho na matukio ya Biblia bila mwangaza wa neema wa Mungu, tunastahili kumwomba. “Yafungue macho yangu.”
Ukweli yenye hatua tatu
Wiki ujao nina mpango ya kutilia mkazo mambo ya ajabu katika Neno la Mungu na jinsi ya kuyatia akilini mwetu na moyoni mwetu. Lakini leo nitatilia mkazo maombi. Nataka tuyaone hatua hizi tatu za dharura: Neno ni muhimu kwa kuishi maisha ya kuegemea Mungu ituelekezayo mbinguni na pia ina nguvu na maana duniani. Hatuwezi kuona jinsi Neno lilivyo bila usaidizi kutoka kwa Mungu. Basi inatupasa tuwe watu wa kuomba kila siku ili Mungu akafanye chochote awezayo kutia maajabu ya Neno moyoni mwetu na maishani mwetu.
Wacha tukachukue hatua hizi tatu moja baada ya nyingine na tuzione vile zimethibitishwa na kuonyeshwa kwenye sehemu zingine za Biblia.
1. Neno ni muhimu katika maisha ya utakatifu
Jambo la kwanza ni kwamba kuona Neno na kulijua na kuliweka ndani yetu ni muhimu katika maisha yetu ya utakatifu na upendo na nguvu kwa ajili ya Mungu.
Tazama tena katika mstari 11, “Nimelificha Neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.” Ni vipi basi tunaweza kuepuka dhambi maishani mwetu? Kwa kuficha Neno la Mungu moyoni mwetu. Ni wangapi wanaharibu maisha yao kwa kutotafakari na kupenda kutii Neno la Mungu? Je, unataka kuwa mtakatifu, yaani ,unataka nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha ya kiungu na upendo wa dhabihu na kudumu kabisa katika njia ya Kristo? Basi shika njia. Mungu ametengeneza njia ya uungu na nguvu: na ni njia ya kuficha biblia moyoni mwetu.
Naisema kwa wakongwe na wazazi wa wachanga. Tafakari na ukariri na ulinde sheria na maonyo na ahadi za Mungu katika maandiko. La, sisemi kuwa ni rahisi, hasa ukiwa ume. Lakini vitu vinavyofaa kutendwa si rahisi kuvitenda. Kutengeneza vifaa vya mbao vinavyong’aa, kutunga shairi nzuri, kutunga wimbo mzuri, kutayarisha mlo mzuri ama kuandaa sherehe-hakuna ile ambayo ni rahisi. Lakini yafaa kufanywa. Je maisha mema ni muhimu na lafaa kufanywa?
Talitha ana umri wa miaka miwili sasa. Anaanza kujifunza aya za biblia moyoni mwake. Anjifunza pia aina tofauti ya maombi. Kwa nini? Haja gani kujitaabisha akichukua muda na jitihada ya kurudia rudia Biblia kwake? Ni rahisi sana-wakati atakuwa katika ujana nataka afuate njia za Mungu na kuwa msafi na takatifu na mwenye upendo na mnyenyekevu na mwenye huruma na hekima. Na Biblia inasema wazi, kama mchana, hii huja kwa kuficha Neno la Mungu moyoni mwako. “Nimeficha Neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.”
Yesu analiweka hivi katika ombi lake kuu kwetu katika Yohana 17:17, “Uwatakase kwa ile kweli; Neno lako ndilo kweli.” “Takasa” ni Neno la Biblia ya kufanya mtu takatifu ama kiungu, kwa upendo ama msafi ama kuwa na utu wema ama kumakinika kiroho. Na mambo haya nayahitaji kwangu miye na kwa ajili ya watoto wangu na kwa ajili yako.Ni nini basi inafaa tufanye mwaka huu? Kama tumetakaswa kwa kweli, na Neno la Mungu ndilo kweli, tufanye nini basi?
Daktari anaposema, “Wewe ni mgonjwa sana na unaweza kufa kwa sababu ya ugonjwa wako, lakini ukimeza dawa hili, utapona na kuishi,” na ukatae kumeza dawa – unashughuli nyingi , madawa ni makubwa mno na vigumu kuyameza, unasahau – utabaki ukiwa mgonjwa na waweza kufa. Hivyo ndivyo ilivyokatika dhambi na kutokomaa kiroho. Ukipuuza yale Mungu anakuambia yatakutakasa na kukufanya ukomee na kuwa mwenye nguvu na mtakatifu, basi hutakomaa, na kuwa na nguvu na utakatifu. Kusoma, na kutafakari na kutia akilini na kutii Neno la Mungu ni njia iliyochaguliwa na Mungu ya kushinda dhambi na kuwa mjasiri, kiungu, mkomavu, mwenye upendo na mwenye hekima.
Kuna mambo ya ajabu ya kuonekana katika Neno la Mungu ambayo yatakubadilisha sana ukiyaona na kuyaficha ndani mwako.
2. Hatuwezi kuona bila usaidizi wa Mungu
Jambo la pili katika andiko hili ni kwamba hatuwezi kuyaona mambo haya ya ajabu katika Neno vile yalivyo bila usaidizi kutoka kwa Mungu
Sababu ni kwamba tumeanguka na kuwa wafisadi na kufa katika dhambi na hivyo basi tumefanyika vipofu, wapuuzi na wagumu. Paulo anaeleza juu yetu hivi katika Waefeso 4:18 – “Akili zetu zimetiwa giza, na tumetengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga na ugumu wa mioyo yetu.”
Huu hapa ni jinsi Musa alivyoandika kuhusu shida hii katika Kumbukumbu la Torati 29:2-4 , “Musa akawaita waisraeli wote akawaambia: macho yenu yameona yale yote BWANA aliyofanya kwa Mfalme farao huko misri … ishara zile za miujiza na maajabu makubwa [yaani, mambo ya ajabu]. Lakini hadi leo BWANA hajawapa akili ya kuelewa au macho yanayo ona au masikio yanayosikia” Tazama: Umeona ... lakini huwezi kuona bila kazi kuu ya Mungu.
Hayo ndiyo mapito yetu. Sisi ni wenye dhambi na wafisadi na wagumu na wa kutoelewa na vipofu bila mwamsho, uisho, urahisi, unyenyekevu, usafi, na kurahisisha kazi ya Mungu maishani mwetu. Hatuwezi kuona uzuri wa ukweli wa roho bila mwangaza wa Mungu. Hatuwezi kuona maajabu na utukufu wa yale Neno linatufundisha bila Mungu kuyafungua macho ya mioyo yetu na kutupa ufahamu wa kiroho juu ya mambo haya.
Sababu ya kufundisha na kujua haya ni kutufanya kuwa na shauku na njaa ya kujua Mungu na kutufanya kusihi na kulilia Mungu atupe usaidizi wake wa kusoma Biblia.
(Juu ya jambo la pili angalia pia Mathayo 16:17 na pia 11:4, na Luka 24:45 ; 1 Wakorintho 2:14-16; Yohana 3:6-8; Warumi 8:5-8)
3. Inatupasa tuombe ili Mungu atusaidie tukaone
Inatuelekeza kwa jambo la mwisho: ikiwa kujua na kuficha ukweli wa Neno la Mungu moyoni ni muhimu katika kuwa takatifu na kupenda na kukomaa na kuelekeza mbinguni, na kama sisi kwa kawaida hatuwezi kuona maajabu ya Neno la Mungu na kuhisi mvuto wa utakatifu wake,basi tuko katika hali mbaya na tunahitaji kuomba Mungu ili atusaidie kuona. “Yafungue macho yangu kupata kuona mambo ya ajabu katika sheria yako.”
Kwa maneno mengine, maombi ni muhimu katika maisha ya mkristo, kwa sababu ndiyo ufunguo wa kufungua nguvu za Neno maishani mwetu. Utukufu wa Neno la Mungu ni kama jua unaoangaza machoni mwa kipofu Mungu asipofungua macho yetu kwa utukufu huo.Tusipoona utukufu, hatutabadilika ( 2 Wakorinth3:18 ; Yohana 17:17 ), na tusipogeuzwa, sisi sio Wakristo.
Katika Waefeso 1:18 , Paulo aomba kwa njia hii. Anasema, “Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru ili mpate kujua tumaini mliloitiwa …” Kwa maneno mengine, “Nimewafundisha mambo haya na mmeyapokea kwa ufahamu wenu wa nje, lakini iwapo tu mtatambua utukufu kupitia ufahamu wenu wa kiroho (“macho ya mioyo yenu”) hamtabadilika. (Tazama pia Waefeso 3:14-19 ; Wakolosai 1:9 na pia 3:16). Hawa ni Wakristo ambao anawaandikia, ambayo inatuonyesha kuwa yafaa tuendelee kuomba hadi tufike mbinguni ili mioyo ya kiroho yapate kuona.
Aina saba ya maombi ya kuloweza kusoma Biblia kwetu
Kwa kuwa ujumbe wetu ni Zaburi 119:18 ,“Yafungue macho yangu kupata kuona mambo ya ajabu katika sheria Yako.” Turuhusu mwombaji huyu kutuonyesha vile anaomba kwa kawaida kuhusu kusoma kwake Neno la Mungu. Basi wacha nifunge kwa safari ndogo ya zaburi 119, na nikuonyeshe aina saba ya maombi ambayo unaweza kuloweza Biblia yako unapousoma mwaka huu.
Yafaa tuombe …
- Kuwa Mungu atatufunza Neno lake. Zaburi 119:12b, “Nifundishe amri zako” (Tazama pia mstari 33,64b, 66, 68b, 135). Masomo ya kweli la Neno la Mungu inawezakana tu kama Mungu mwenyewe anakuwa mwalimu ndani na pia kupitia njia zingineza mafundisho.
- Kuwa Mungu hataficha maagizo yake kwetu sisi. Zaburi 119:19b , “Usinifiche maagizo yako.” Biblia inaonya kuhusu njaa ya kusikia maneno ya BWANA (Amos 8:11). (Tazama pia mstari 43).
- Kuwa Mungu atatufanya kuelewa Neno lake. Zaburi 119:27 , “Nieleweshe mafundisho ya mausia yako” (mistari 34,73b, 144b, 169). Hapa tunauliza Mungu kutuelewesha – kufanya yale awezavyo kutuwezesha kuelewa Neno lake.
- Kuwa Mungu atageuza mioyo yetu kwa Neno lake. Zaburi 119:36, “Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako, na sio kwenye mambo ya ubinafsi.” Shida tuliyo nayo sio sababu zetu, lakini uwezo wetu – tumeguzwa vibaya na hali ya maumbile, kusoma, kutafakari na kutia akilini Neno lake. Basi ni lazima tuombe ili Mungu ageuze uwezo wetu.
- Kuwa Mungu atatupa uhai wa kuhifadhi Neno lake. Zaburi 119:88. “Yahifadhi maisha yangu sawasawa na upendo wako, nami nitatii sheria ya kinywa chako.” Anajua kuwa tunahitaji uhai na nguvu ya kujipa kwa Neno na utiifu wake. Basi anauliza Mungu kumpa mahitaji yake muhimu. (Tazama pia mstari 154b)
- Kuwa Mungu ataongoza hatua zetu katika Neno lake. Zaburi 119:133 , “Ongoza hatua zangu kulingana na Neno lako.” Tunategemea Mungu sio tu kwa kuelewa na uhai, bali pia kwa utendaji wa Neno. Kuwa litaongoza katika maisha yetu. Hatuwezi kufanya haya pekee yetu.
- Kuwa Mungu atatutafuta tunapotangatanga kutoka kwa Neno lake. Zaburi 119:176 , “Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea. Mtafute; mtumishi wako.” Ni ajabu kuwa huyu mtumishi wa Mungu anatamatisha zaburi kwa kukiri dhambi na haja ya Mungu kumtafuta na kumrudisha. Hivi kwetu inafaa tuombee tena na tena.
Neno, hazina yetu
Natamatisha kuwa tunapoingia katika mwaka wa 1998 na kuwa na shauku ya kuwa takatifu na kupenda na kudumu katika njia za Mungu katika mji na mataifa, lazima tuwe watu wa kuficha Neno la Mungu moyoni mwetu, lakini zaidi – watu wanaojua juu ya hali yetu ya kuhitaji isipokuwa Mungu na kuwa ameteua maombi kama njia ya macho yetu kufunguliwa ili tuone maajabu katika Neno na kubadilishwa. “Yafungue macho yangu kupata kuona mambo ya ajabu katika sheria yako.”
Alikuwa na juhudi ya kiwango gani katika aina hizi za maombi? Inatupasa tuwe na juhudi gani? Jibu mmoja limepeanwa katika Zaburi 119:147 , “Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada, nimeweka tumaini langu katika Neno lako.” Anaamka asubuhi na mapema! Ni jukumu kuu. Unaweza kulifanya liwe hilo?