Nia yangu: Kuhubiri mahali Kristo hajatajwa
Kwa maana sitadhubutu kusema kitu chochote zaidi ya kile ambacho Kristo amefanya kwa kunitumkiia mimi katika kuwaongoza watu mataifa wamtii Mungu kwa yale nilivyosema na kufanya, kwa nguvu za ishara na muijiza, kwa uwezo wa Roho wa Mungu, ili kuanzia Yerusalemu hadi maeneoyote ya kando kando yake, mpaka //iriko nimekwisha kulihubiri Habari njema, si pale ambapo Kristo amekwisha kujulikana, ili nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine. Lakini kama ilivyoandikwa: “Wale ambao hawajahubiriwa habari zake wataona, nao wale hawajaziskia watafahmu.” Hii ndiyo sababu nimezuyiliwa mara nyinginisiweze kuja kwenu. Lakini sas kjwa kuwa hakuna nafasi zaidi kwa ajili yangu katika sehemu ninatamani kuja kwenu kama ambavyo nimekuwa na shauku kwa miaka mingi, nimekusudia kufanya hivyo nitakapokuwa njiani kwenda Hispania. Natarajia kuwaona katika safari yangu na kusafirishwa nanyi mpaka huko, baada ya kufurahia ushirika wenu kwa kitambo kidogo.
Kuna mambo matatu katika andiko hili ambayo nafikiri yafaa tuyaangazie. Yote yanaguza maisha yako moja kwa moja (hata kama hufahamu hayo), na yote yalingana moja kwa moja kwa Mungu na lengo lake katika karne la ishirini na moja. Naona, kwanza, nia takatifu. La pili, hitaji isiyo na kipimo. Tatu, mpango wa ulimwengu. Basi wacha tuyachukue moja baada ya nyingine na kwetu sisi ni ulimwenguni wetu wa leo.
1. Nia Takatifu
Mstari 20: “Hivyo ni nia yangu kuhubiri Habari Njema, si pale ambapo Kristo amekwisha kujulikana, ili nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine.
Paulo alitawaliwa na nia takatifu. Nasema alitawaliwa kwa sababu anasema katika mstari 22, “Hii ndiyo sababu nimezuiliwa mara nyingi nisiweze kuja k, wenu.” Na anasema mwishoni mwa mstari wa 23, “Nimekuwa na shauku kwa miaka mingi kuwajia.” Ukiwa na shauku ya kutenda kitu kwa miaka na mikaka, na ukose kukitenda, kitu kinatawala. Na kile kilikuwa kikirtawala Paulo na kumfanya kwenda Roma ni kuwa hakuwa amemalizana na nia yake katika maeneo ya Yerusalem hadi Uirikamu (Albani wakati huu), na hangeweza kugeukia kutoka kwa nia hii hadi itimizwe. Lakini sasa kazi tayari imefanyika katika maeneo haya, na nia yake inamwelekeza Uhispania. Hiyo hatimaye inamruhusu kufanya yalke alitaka kuyatenda kwa miaka, yaitwayo, kutembelea kanisa la Roma na kufurahi kujumuika nao kwa muda mfupi.
Ni jambojema kutawaliwa nania takatifu. Je, unatawaliwa na nia takatifu? Naiita “takatifu” kwa sababu lengo lake ni takatifu—kuona watu kutoka kwa mataifa yote ambao hawajasikia juu ya Yesu wakimwamini na kumcha na kuokolewa naye kutokana na dhambi zao na ghadhabu za Mungu. Na ninaiita nia hii “takatifu” kwa sababu inatoka kwa Mungu na neno lake takatifu, vile tutaona baada ya muda mfupi. Ni haki na ni vyema kutawaliwa na nia tukufu. Je, una nia tukufu? Si kila mmoja anafaa kuwa na nia ya Paulo. Moja apanda na mwingine atia maji (1 Wakorintho 3:6-8). Kila mmmoja ana karama yake (1 Wakorintho 7:7) Kwa bwana wake tu Anasimama na kuanguka (Warumi 14:4). Lakini nafikiri Mungu angefurahi kama wanawe wote wangekuwa na nia takatifu.
Nia takatifu kwa wasichana na wanaume
Wana wadogo, mnisikilize kwa makini, kwa muda. Nayajua maneno, “Nia takatifu”, si ya kawaida na hayatumii kila siku. “Nia takatifu”inamaanisha kitu ambacho unataka kufanya kewa hakika ambacho Mungu anataka ukifanye. Kile unataka kukifanya sana kwa kiasi kwamba kinakuzuilia kufanya vitu vingine ambavyo kwa hakika ungependa kufanya. Paulo kwa hakika alitaka kwenda Roma kwa miaka. Lakini hakuenda kwa sababu alikuwa anataka kitu kingine zaidi. Alikuwa antaka kuhubiri injili Asia na Ughiriki mahali watu hawakuwa wamejua kuhusu Yesu. Kwa hakika zaidi alitaka kuifanmya hii. Tunauita aina ya shauku hii”nia” Na tunauita “nia takatifu” kama ni kitu Mungu antaka ukitende.
Je unayo yoyote? Labda bado. Wewe ni mtoto tu. Hiyo ndiyo unastahili uwe. Lakini wakati moja hatakuwa mtoto tena. Na mojawapo kati ya tofauti kati ya kuwa na mtoto na kua ni kwamba kua kama mkristo kunamaanisha unapokea nia takatifu. Wengi wa wasichana wachanga, Tabitha wangu akiwa moja wao, wanahitaji kumiliki na kucheza na vikaragosi. Ni kitu kizuri. Lakini siku itawadia, wasichana wadogo, mtakapoweka kando raha ya kucheza na vikaragosi na mkue katika furaha kubwa na vyema ya kuwalea watoto wa kweli katika shule za Chekechea. Na labda mtaongoza huduma ya kuwalea watoto walio na njaa mahali mbali siku moja, ama watoto pweke ambao hawana mama wala baba. Na kwa wengine wenu hii itakuwa nia takatifu na kwa wengine wenu nia yenu takatifu itakuwa kitu kingine.
Na wanaume, msikize. Kama mko vile nilivyokuwa, kile mnahitaji ni mpira, gari, na bunduki na mtu wa kucheza nayo. Sijawahi kuwa na bunduki ya kweli (isipokuwa bunduki la chembe) Lakini nilifyatua watu wengi wabaya na bastola yangu ya Matt Dillon, na bunduki langu lenye mkono mduara linalofanana na bunduki aina ya Lucas Mc Cain. Nilipenda kucheza kabumbu na marafiki yangu na kuchimba barabara njiani kwa ajili ya magari yangu na kuchomoa bastola yangu kwa kasi sana hungeweza kuiona. Ilikuwa raha. Na hiyo ilikuwa nzuri.
Lakini siku mmoja hautakuwa mvulana mdogo tena. Na mojawapo ya tofauti kati ya kuwa mvulana mdogo na kua ni kwamba kua kama Mkristo kunamaanisha kuwa unapokea nia takatifu. Na hiyo inamaanisha furaha ya bunduki na magari na mipira inadidimia na furaha ya kupigania haki na wokovu inakuwa kubwa. Kua kunamaanisha kupata nia mtakatifuya kubeba panga la Roho kwa ukuu na kuendesha gari lililojaa upendo kwa walio na hitaji na kupiga teke matako ya shetani katika jina la Yesu.
Mama na baba, makpera, wazee kwa wachanga,Wakristo wanafaa kuwa na nia takatifu. Kitu ambacho hakika unataka kufanya kwa utukufu wa Mungu. Kitu ambacho kinakutawala. Inakusaidia kutoenda Roma kwanza. Inakupa mtazamo wa milele na arikatika maisha yako.
Chanzo cha Nia Takatifu
Inakuja kutoka wapi? Sehemu muhimu la jibu limepeanwa katika kiunganisho kati ya mistari 20 na 21.” Hivyo ni nia yangu kuhubiri Habari njema, si pale ambapo Kristo amekwisha kujulikana, ili nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine. Lakini kama ilivyoandikwa, [halafu Paulo ananukuu Isaya 52:15] ‘wale ambao hawajahubiriwa habari zake wataona, nao wale hawajaziskia watafahamu.’”
Sasa huu hapa ni jambo la ajabu na yenye maana kuhusu hii kwa ajili yetu.Tunajua kutoka kwa Matendo 9 na 22 na 26 kuwa Paulo aliitwa na Kristo aliyefufuka njiani ya kuelekea Damaski. Yesu alimpa Paulo huduma zake katika Matendo 26:18, “Nakutuma [kwa watu wako na watu Mataifa], uyafunge macho yao ili wageuke kutoka gizani waingie nuruni na kutoka kwenye nguvu za shetani, wamgeukie Mungu ili wapate msamaha wa dhambi na sehemu miongoni mwa wale waliotakaswa kwa kuniamini Mimi.” Basi alipokea mwito kutoka kwa Kristo mwenyewe aliyefufuka, anayeishi, na tukufu kuwa nuru kwa watu Mataifa.
Lakini hiyo si kile anasema katika Warumi 15:21. Hasemi, “Nikaona nia hii kuwa nuru kwa mataifa wasiomjua Kristo kwa sababu Yesu aliniita njiani ya kuelekea Damaski. Anasema, “Hivyo ni nia yangu—Ninatawalwa na shauku ya kuhubiri pahali Kristo hajatajwakwa sababu Isaya 52:15 inasema,”Wale ambao hawajahubiriwa habari zake wataona, nao wale ambao hawajazisikia watafahamu.”
Je unaelewaje hiyo? Hili ndilo ninalifahamu kwalo. Wakati Yesu alipoita Paulo njiani ya kuelekea Damaski ili apeleke Injili kwa watu Mataifa ambao hawakuwa wamesikia, Paulo alienda kwa Agano la kale na akatafuta dhibitisho na sababu ya mwito huu ili kuona vile inaambatana na lengo la kuunganisha la Mungu. Na akaipata. Na Kwa ajili yetu ananena kwa njia hii. Haneni tu kuhusu tukio lake njiani ya kuelekea Damaski ambalo hatutakuwa nalo. Anaongea kulihusu neno la Mungu ambalo limeandikwa an ambalo tunalo. Na ametilia mkazo nia yake hapo.
Basi jibu langu la swali ‘Je nia yako takatifu yatokea wapi? Ni hili: Inakuja kutoka kwa mkutano wako wa moja kwa moja na Kristo aishiye (Si lazima kimatukio kama ilivyo katika njia ya Damaski) ikiwa imeundwa na kuelimishwa na kuhimizwa na neno lililoandikwa la Mungu. Unapotafakari juu ya amri ya Bwana usiku na mchana (Zaburi 1:2)—Unapojitumbukiza katika neno la Mungu—anakuja na kuuchukua ukweli mwingine juu ya neno hilo na kuuchomelea rohoni mwako mpaka lifanyike nia takatifu. Kama halijatendeka bado, jitie zaidi ndani ya neno la Mungu na ukamwombe kwayo.
2. Hitaji lisiloweza kupimika
Mungu hatuelekezi katika nia isiyo na maana—ambayo utajutia mwishoni mwa maisha yako. Kila mara kuna hitaji la kutimizwa—si hitaji katikaMungu, lakini ulimwenguni—na nia takatifu. Nia takatifu si juu ya kujitukuza wewe mwenyewe. Huwa ni aina ya upendo. Huwa hukutana na hitaji la mtu.
Sasa ni nini hitaji lisiloweza kupimika ambalo Paulo aongea kwalo katika andiko hili? Mstari 20: “Hivyo ni nia yangu kuhubiri habari Njema, si pale ambapo Kristo amekwisha kujulikana.” Hiyo inamaanisha kwamba Paulo ameelekeza mtazamo wake kama nuru unaong’aa kuhubiri Injili kwa wale ambao hawajasikia juu ya Kristo. Hawamjui hata kwa jina lake
Mataifa Hawana Udhuru (Kijisababu)
Sasa hapa ni swali. kama hawa watu hawajui hata jina la Yesu, je basi wana sababu ya kumwamini kwa ajili ya wokovu? Na kama sivyo, basi si ingekuwa shwari kwao kuwaacha tu katika hali yao ya kutomjua na kutoamini kuwa Mungu atawarehemu na wataokolewa kwa kuwa hawajasikia habari kumhusu Yesu? Kwa nini, Paulo, unateseka sana kuhubiri Injili kwa watu ambao hawajasikia jina la Yesu?
Paulo alipeana jibu katika Warumi 1:18-23. Isome nami taratibu na bila fikira yoyote na usikie uzito wake vile Paulo yawezekana aliusikia. Maneno haya yameandikwa juu ya watu na mataifa yote ambao hawajasikia jina la Yesu na nia ya Paulo inalenga kuwafikia.
Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi wote na uovu na wanadamu ambao huipinga kweli kwa uovu wao, 19 kwa maana yote yanayoweza kujulikana kumhusu Mungu ni dhahiri kwao, kwa sababu Mungu mwenyewe ameliweka wazi kwao. 20 Kwa maana tangu kuumbwa kwa uweza wake wa milele na asili yake ya Uungu, umeonekana waziwazi ukitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru. [hayo ni maneno yaliyo na athari ya kifo ambayo yanaeleza hitaji lisilokuwa na kipimo Paulo aonayo; mataifa ambayo hawajasikia juu ya Yesu hawatakuwa na udhuru katika siku ya hukumu.] 21 Kwa maana ingawa walimjua Mungu hawakumtukuza yeye kama ndiye Mungu wala hawakumshukuru bali fikira zao zimekuwa batili na mioyo ya ujinga ikatiwa giza. 22 Ingawa wakijidai kuwa wenye hekima, wakawa wajinga 23 na kubadili utukufu wa Mungu aishiye milele kwa sanamu zilizofanywa zifanane na mwanadamu ambaye hufa, ndege, wanyama na viumbe vitambaavyo.
Paulo anasema katika Warumi 2:12, “Watu wote waliotenda dhambi pasipo sheria wataangamia pasipo sheria, nao wote waliotenda dhambi chini ya sheria watahukumiwa na sheria.” Kila mtu atahukumiwa kulingana na yale waliyoyapokea. Na watu wote wataangamia yule hajasikia Injili, kwa sababu watu wote wanapinga ukweli walio nayo na kuishi wakimuasi Mungu. Kuna tumaini moja tu: Kuisikia na kuamini injili ya Yesu Kristo.
Hitaji la mataifa ambao hawajasikia jina la Yesu ni hitaji isiyo na kipimo. Ni hitaji isiyo koma milele. Hitaji kuu ambalo laweza kufikiriwa ni hitaji la mataifa kuisikia Injili ya Yesu Kristo na kuiamini. Kwa maana aaminiye, kwanza kwa Myahudi pia kwa Myunani.” (Warumi 1:16). Na hakuna anayeokolewa isipokuwa kwalo.
Si kila mmoja wenu anaitwa kuenenda kama Paulo. Lakini huwezi kuwa mtu wa upendo na usitake maisha yako ihesabike kukutana na hitaji hili.
3. Mikakati ya Ulimwenguni kote
Lakini wengine wenu Mungu anawaita ili muungane na Paulo mwenyewe na kwa likizo katika mikakati hii ya kipekee ya ulimwenguni kote. Huu hapa ndipo mikakati. Na ni ya ajabu. Kama wewe ni mgeni Bethlehemu, sikiza kwa makini vile tunavyoelewa miito. Hapa ni matamshi ya ajabu ya Paulo.
Kwanza mstari 19b, “Kuanzia Yerusalemu hadi maeneo yote ya kando kando yake mpaka Ihiriko nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa ukamilifu .” Ni kusema kutokea Yerusalemu hadi juu Siria kupitia Asia ndogo (Uturuki), hadi chini kupitia Ugiriki kaskazini mwa Italia pahali Albania ipo leo. Paulo anasema amekamilisha Injili huko. Na anahitimiza jambo hili la ajabu katika mstari 23 kwa kusema, “Kwa kuwa hakuna nafasi zaidi kwa ajili yangu katika sehemu hii.” Na baadaye katika mstari 24 anasema, “Naenda Hispania.”
Alimaanishaje kuwa hakuwa na nafasi zaidi ya kufanya kazi Yereusalemu hadi Iliriko? Si hatari kusema kwamba kulikuwa na watu zaidi ya kumi elfu ambao walikuwa hawajahubiriwa katika maeneo hayo. Tunajua hili kwa sababu Paulo anamwandikia Timotheo huko Efeso (katika eneo hili) na kumuamuru “kufanya kazi ya mhubiri (2 Timotheo 4:5). Kwa maneno mengine, kuna watu wanaohitaji kuhubiriwa. Na Paulo anasema kazi yake imekamilika katika eneo hili.
Tunachukua hili kumaanisha: Paulo si muhubiri wa kitaifa; Yeye ni mhudumu wa kupita mipaka, mhudumu mwanzilishi. Ni kusema, mwito na nia yake si kuhubiri pahali ambapo tayari ushajengwa. Kanisa linafaa kufanya hilo. Mwito na nia ya Paulo ni kuhubiri injili pahali hakuna kanisa la kuhubiri. Pahali hakuna Wakristo. Hawajawahi kulisikia jina la Yesu.
Huduma, kuhubiri, na Nia Takatifu
Msamiati si kile cha muhimu. Kile muhimu ni tofauti. Kuna wahudumu waanzilishi na wanaopita mipaka, na kuna wahubiri. Wahudumu wanapitia tamaduni na kujifunza lugha. Na wahudumu wa kupita mipaka wanamwagilia maisha yao kupitia neno na vitendo, kupitia uweza wa ishara na maajabu, kupitia uweza wa Roho wa Mungu ”Kuvunja maelfu ya miaka ya giza na utawala wa shetani juu ya watu ambao hawamjui mfalme wa wafalme na mwokozi wa ulimwengu.
Hii ndio ilikuwa nia ya Paulo. Na ikiwa bado mwito mkuu wa kufanya wanafunzi kutoka ulimwenguni kote bado ipo na kuna watu hivi leo ambao hawajui Habari Njema, basi kila kanisa lastahili liombe kuwa Mungu aweze kuwainua wahudumu wa kupita mpaka wengi, na kutufanya wote kuwa wahubiri.
Naweza kutafakari—hakika naomba –kuwa miaka kumi kutoka sasa mtu fulani—labda kumi miongoni mwenu—wataandika barua nyumbani kwa watu ambao hawajafikiwa na kusema, “Niko hapa kuwahubiria Injili wale ambao hawajaiskia, kwa vile ilivyoandikwa katika Warumi 15:20 “Hivyo ni nia yangu kuhubiri Habari Njema, si pale ambapo Kristo amekwisha kujulikana, ili nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine.” Mungu alichomelea neno hilo moyoni mwangu na akaligeuza kuwa nia takatifu katika Kanisa la Ubatizo wa Bethlehemu, Agosti, 2006.
Bwana, tafadhali, tenda hilo. Amina.