Habari njema ya Mungu kuhusu Mwanawe
Paulo, mtumishi wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu, 2 Injili ambayo Mungu alitangulia kuiahidi kwa vinywa vya manabii Wake katika maandiko matakatifu, 3 yaani, Injili inayomhusu Mwanawe, Yeye ambaye kwa uzao wa mwili alikuwa mzao wa Daudi 4na ambaye kwa uwezo wa Roho wa utakatifu alidhihirishwa kuwa Mwana wa Mungu kwa ufufuo Wake kutoka kwa watu, yaani Yesu Kristo Bwana wetu.
Tuliona wiki iliopita katika mstari wa kwanza kwamba Paulo ni mtumishi wa Kristo. Kwamba, alinunuliwa na anamilikiwa na kutawaliwa na Kristo. Anaishi kupendeza Kristo. Na, tusije tukawa na fikira mbaya kuwa Kristo anategemea miradi na kazi ya utumwa wa Paulo, inafaa tuone katika Warumi 15-18 kuwa Paulo anategemea Kristo kwa yote afanyayo katika huduma ya Kristo: “Kwa maana sitadhubutu kusema kitu chochote zaidi ya kile ambacho Kristo amefanya kwa kunitumia mimi katika kuwaongoza watu mataifa wamtii Mungu kwa yale niliyosema na kufanya.” Kwa mukhtadha mwingine, Paulo anamtumikia Kristo kwa nguvu zile Kristo anamtumikia Paulo mwenyewe. “Kwa kuwa hata Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika. (Mariko 10:45; tazama pia 1 Wakorintho 15:10; 1 Petro 4:11). Tutasambaratisha maana yote ya Warumi kwanzia mwanzo tusipoona kuwa Paulo anamtumikia Kristo kwa kwa nguvu alizopewa kupitia Kristo, ndipo Kristo apokee utukufu kupitia huduma wa Paulo (tazama 1 Petro 4:11).
Hii ukuu wa kiungu, Kristo apeanaye vyote ndiye Yule tunayekutana naye katika tamshi lifuatalo, “ameitwa kuwa kuhani.” Kristo aliita Paulo njiani mwa kuelekea Damaski na kumpatia jukumu ya kuwa mwakilishi wake mwenye mamlaka ya kuweka msingi ya kanisa na mafundisho ya kweli. Baadaye tukaona Mungu mkuu, mikono yake ya kupanga katika andiko linalofuata,”lililotengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu.”Mungu aliteua Paulo kabla azaliwe, Wagalatia 1:15 inasema. Mungu ni mwenye wivu kwa kuwasili na kufunuliwa kwa Injili yake na hachukulii vitu kwa urahisi.
Leo tutaangalia kuhusu neno hili, “Injili ya Mungu” (1:1) na vile Paulo analifunua katika mstari 2 hadi 4.
“…ambayo Mungu alitangulia kuiahidi kwa vinywa vya manabii wake katika maandiko matakatifu…”
Jambo la kwanza ambalo Paulo anasema linaambatana kabisa na yale tumeona: kuwa Mungu ni mwenye wivu kuonyesha kwamba Injili ilipangwa kitambo kabla itendeke. Mstari 2: “[Paulo] alitengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu, ambaye Yeye [Mungu] aliahidi mapema kupitia manabii Wake katika maandiko matakatifu.”
Tilia manani mambo haya matatu kutoka mstari wa pili.
1) Injili ya Mungu ni timilizo ya ahadi za Agano la Kale.
Sio dini jipya. Ni timilizo ya dini la kale. Mungu wa Agano la kale ndiye Mungu wa Agano jipya. Yale alikuwa akipanga na kuahidi wakati huo, alitimiliza kupitia kuja kwa Yesu.
2) Mungu anahifadhi ahadi zake.
Miaka mia moja inapita. Wayahudi wanashangaa kama Masiya kweli atakuja. Wanapitia katika mateso makuu. Hatimaye Mungu anatenda na ahadi inatimizwa. Hii inamaanisha kuwa Mungu anaweza kuaminika. Inaweza kaa ni kama amesahau ahadi zake. Lakini Hajasahau. Basi mstari wa 2 si tu neno kuhusu yale yalioko katika Injili Yake, bali ni sababu ya kuiamini. Ikiwa tanaweza kuona kuwa Mungu aliahidi Kristo karne nyingi kabla aje na katika njia nyingi anatimiza ahadi hizi, basi imani yetu inatiliwa nguvu.
3) Haya ni maandiko takatifu, yaliyotiwa uwezo wa Mungu ambayo yafaa tuyashikilie na kuyaamini.
Tazama mahadhara muhimu kabisa ya mistari hii miwili kwa ajili ya misingi ya andiko. Kwanza kuna Mungu; hatimaye kuna ahadi Mungu anataka kufanya; tena kuna manabii ambao kupitia kwao (kumbuka vizuri: sio kwao, bali kupitia kwao, Mungu mwenyewe akibaki msemaji) ananena ahadi zake, tena kuna maandiko; na maandiko haya yanaitwa matakatifu. Kwa nini ni matakatifu kwayo yenyewe. Soma mistari hii kwa makini: Yeye [Mungu] alitangulia kuahidi kupitia manabii Wake katika maandiko matakatifu.” Mungu aliahidi katika maandiko matakatifu. Mungu anaongea kupitia maandiko. Hilo ndilo linaloyafanya kuwa matakatifu. Huu ndio ufahamu wa Paulo juu ya andiko na unafaa uwe wetu pia. Kama umewahi shangaa kwa nini Biblia yetu inasema “Biblia Takatifu”mbele yake, Warumi 1:2 ndio jibu.
Na tusije tukapoteza umuhimu wa hii kwa mtazamo ya ndani ya Warumi, kumbuka mambo matatu: (1) Paulo anajiona katika 1:1 kama kuhani wa Kristo Yesu, akiongea na kundika kwa nguvu kwa niaba ya Yesu kama mwanzilishi wa kanisa. Kwa maneno mengine, kama vile nabii wa kale (Waefeso 2:20). (2) Paulo alisema katika 1 Wakorintho 2:13, “Haya ndiyo tusemayo, si kwa maneno tuliyoyafundisha kwa hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho.” Kwa mukhtadha mwingine, Paulo anasisitiza nguvu spesheli ya kiungu kwa mafundisho yake. (3) Katika 2 Petro 3:1, Petro anasema kuwa “watu wengine wanabadilisha [maandishi ya Paulo], vile wanavyofanya kwa maandiko mengine. Basi Petro anaweka nyaraka za Paulo katika kitengo sawa na maandiko matakatifu ambayo tunayasoma hapa.
Ndiyo maana mahubiri ni ya muhimu sana katika maisha yetu. Tunaamini kuwa waraka wa Paulo kwa Warumi ni neno la Mungu, wala si neno tu la binadamu. Injili iliahidiwa kupitia maandiko matakatifu kwa uwezo wa Mungu. Hilo ndilo tunaamini, na linaleta tofauti kubwa jinsi tunatazama ukweli na maadili na mahubiri na kuabudu na vitu vyote katika ulimwengu.
Basi jambo la kwanza Paulo anasema kuhusu Injili ya Mungu ni kwamba ilipangwa na kutabiriwa kitambo (1:2). Ndiyo Injili “ambayo alitangulia kuahidi kupitia manabii Wake katika maandiko yake matakatifu.”
“…Kumhusu Mwanawe…”
Jambo la pili anasema kuhusu Injili ya Mungu (1:3) ni kuwa inamhusu Mwanawe.” . . . Injili ya Mungu, aliotangulia kuahidi kupitia manabii Wake katika maandiko yake matakatifu, kumhusu Mwanawe . . . ” Injili ya Mungu ni kumhusu Mwanawe. Inafaa tuelewe mambo mawili kuhusu Mwana wa Mungu sasa hivi, ama tunaweza kupotea.
1) Mwana wa Mungu alikuwa kabla afanyike binadamu.
Tazama Warumi 8:3, “Kwa maana kile ambacho sheria haikuwa na uwezo wa kufanya, kwa vile ilivyokuwa dhaifu katika mwili, Mungu kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe kwa mfano wa mwanadamu mwenye mwili ulio wa dhambi.” Mungu alimtuma ili achukue mwili wa mwanadamu. Basi Mwana alikuweko kama Mwana wa Mungu kabla ya kuwa mwanadamu. Inamaanisha kuwa Kristo ni na alikuwa Mwana wa Mungu katika njia ya ajabu mno—si kwa njia tulivyo wana wa Mungu (Warumi 8:14, 19)
2) Kristo mwenyewe ni Mungu.
Katika Warumi 9:5, tunapotazama fursa za Israeli, Paulo anasema, “ . . . Wao ni wa uzao wa mababa wakuu wa kwanza, ambao kutoka kwao Kristo alikuja kwa jinsi ya mwili kama binadamu, Yeye ambaye ni Mungu aliye juu ya vyote, mwenye kuhimidiwa milele! Amen. Na katika Wakolosai 2:9 Paulo anasema, “Maana ukamilifu wote wa uungu umo ndani ya Kristo katika umbile la mwili wa kibinadamu.” Paulo anaposema kwamba Injili ya Mungu ni kumhusu Yesu, anamaaanisha kuwa ni kuhusu kuwa kiungu kwa Mwana hapo kabla. Injili ya Mungu sio kuwa Mungu kupanga mambo ya binadamu kwa njia mwafaka. Ni juu ya Mungu kupenyelea mambo ya wanadamu kutoka nje kupitia kwa mtu ambaye ni Mwanawe ambaye ni sura kamili ya Baba na Yeye mwenyewe ni Mungu.
Basi Paulo anaweka uzito kuu katika “Injili ya Mungu” kwa kusema, kwanza, kuwa imeahidiwa—kupangwa—na Mungu kabla ya ifanyike, na, pili, kuwa inahusu Mwana wa Kiungu. Mungu muumba wa dunia, amepanga mambo mazuri kwa dunia, na kiini cha mpango wake ni Mwanawe.
“…Yeye ambaye kwa uzao wa mwili alikuwa mzao wa Daudi…”
Jambo la tatu Paulo anasema kuhusu Injili ya Mungu ni kuwa Mwanawe wa kiungu “alizaliwa kwa uzao wa mwili katika uzao wa Daudi.” Inasema mambo mawili kwa pamoja:
1) Mwana wa Mungu alifanyika mwanadamu.
Alizaliwa. Kazi alistahili afanye—jukumu alilokuwa kwalo—ilimuhitaji achukue umbile wa mwanadamu, pamoja na umbo lake la kiungu. Mungu hakuchagua mwanadamu na kumfanya Mwanawe; alichagua Mwanawe wa kipekee na wa milele kuwa Mwana wa adamu.
2) Alizaliwa katika uzao wa mfalme Daudi wa Agano la Kale.
Kwa nini hilo ni sehemu ya Injili ya Mungu? Kwa nini ni habari njema? Jibu ni kwamba ahadi zote za Agano la Kale zinategemea kuja kwa Masiya—aliyepakwa mafuta—ambaye atatawala kama mfalme katika uzao wa Daudi na kuchua mateka maadui wa watu wa Mungu na kuleta haki na amani milele. Yeye atakuwa Ndiyo kwa ahadi zake.
Tazama ahadi za Agano la Kale kadhaa. Yeremia 23:5, “Siku zinakuja, nitakapomwinulia Daudi Tawi lenye haki, Mfalme atakayetawala kwa hekima na kutenda lililo haki na sawa katika nchi.” Ama Isaya 11:10, “Katika siku hiyo, shina la Yese [kusema, mwana wa Daudi, uzao wa Yese] litasimama kama bendera kwa ajili ya mataifa, mataifa yatamkusanyikia na mahali pake pa kupumzika patakatifu.”
Basi Injili ya Mungu ni habari njema ambapo sasa, baada ya miaka mia na mia, Mungu ametenda ili atimilize mpango wake na ahadi kuwa mfalme atakuja kupitia shina la Daudi, na, vile Isaya 9:6-7 inavyosema, “nao utawala utakuwa mabegani mwake. Naye ataitwa: Mshauri wa ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa Amani. Kuongezeka kwa utawala wake na amani hakutakuwa na mwisho.”
Basi “Injili ya Mungu” ndio habari njema ya wakati kuwadia na Ufalme wa Mungu kuwa karibu (Mariko 1:14-15, “Yesu aliingia Galilaya akaanza kuhubiri Habari njema za Mungu, akisema 'Wakati umewadia, Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema.'”). Kuja kwa Mwana wa Mungu duniani ilikuwa kuja kwa “Mwana wa Daudi,” mfalme wa ahadi. Atatawala mataifa na kushinda maadui wa Mungu na atatawala kwa haki na amani na, kulingana na Isaya 35:10, “Waliokombolewa na Bwana watarudi, wataingia Sayuni wakiimba, furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao. Watapata furaha na shangwe, huzuni na majonzi vitakimbia.” Hilo ndilo linalofanya mstari wa 3 “Injili ya Mungu.” Kuja kwa Mwana wa Mungu kama Mwana wa Daudi itamaanisha furaha milele katika uwepo wa Mungu—kwa waliokombolewa kwa Bwana.
“…Kwa uwezo wa Roho wa utakatifu alidhihirishwa kuwa Mwana wa Mungu kwa ufufuo wake kutoka kwa wafu…”
Lakini kuna jambo lingine mmoja ambalo Paulo anasema kuhusu “Injili ya Mungu.” Sio tu kwamba ilipangwa na kuahidiwa kabla itendeke; na sio tu kuhusu Mwanawe wa kiungu, aliyekuwa; na sio tu kwamba ni habari ya kuwa Mwanawe amezaliwa kama Mwana wa kimwili wa Daudi kutimiliza matumaini ya Agano la Kale na ndoto ya haki na amani na furaha katika ufalme wa Mungu; lakini katika mstari wa 4, Paulo anasema kitu cha kutamausha na ya kutia nguvu. Anasema kwamba Mwana wa Mungu “Kwa uwezo wa Roho wa utakatifu alidhihirishwa kuwa Mwana wa Mungu kwa ufufuo Wake kutoka kwa wafu.”
Kwa nini nasema ni ya kutamausha? Wengi wa Wayahudi katika nyakati za Paulo walitarajia kuwa Masiya atakuja kwa nguvu na kwa njia ya kisiasa, na kuwa watawala watesi wa dunia, Warumi, na kujenga ufalme wa kidunia katika Yerusalemu na kuishi kwa ushindi milele pamoja na watu Wake. Lakini yale Paulo anayasema katika mstari wa 4 inamaanisha kuwa kati ya mstari wa 3 na nne Mwana wa Daudi alikufa. Alikufa! Wale walifikiria kuwa Yeye ni Masiya walitamaushwa. Masiya hawafi. Wanaishi na kushinda na kutawala. Hawashikwi na kupigwa na kudharauliwa na kusulubishwa na kuwacha watu wao kama mayatima. Ilikuwa ya kutamausha. (Luka 24:21, “Lakini tulikuwa tumetegemea kwamba Yeye ndiye angeliikomboa Israeli”).
Paulo atarejelea kifo cha Kristo katika fungu la 3 na 4 na 5 na 8. Lakini kwa sasa anaenda kwa jambo la kutia nguvu ya ushindi wa Injili ya Mungu. Huyu Masiya aliyekufa, Paulo anasema katika mstari wa 4, alifufuliwa kwa wafu. Hili liko moyoni mwa Injili ya Mungu. Na Paulo anasema mambo mawili kuhusu ufufuo huu.
1) Ufufuo huu kutoka kwa wafu ulikuwa ”kupitia uwezo wa Roho wa utakatifu.”
Hili linamaanisha nini? Nalichukua hili kuwa mambo mawili.
a. Roho Mtakatifu wa Mungu alifufua Yesu kutoka kwa wafu.
Nachukua hisia zangu kutoka Warumi 8:11, “Nanyi ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, lakini roho zenu zi hai kwa sababu ya haki.” Hii inafundisha kwamba tutafufuliwa na Roho wa Mungu anayeishi ndani yetu, kwa ile njia Kristo alivyofufuliwa. Basi Roho alishiriki kwa kufufua Yesu kutoka kwa wafu.
b. Lakini ni kwa nini Paulo analitumia neno hili lisilokuwa ya kawaida, “Roho ya utakatifu” (halipatikani pahali popote kwenye Biblia)?
Hii ndio maoni yangu. Kuhusika na wafu ilikuwa jambo mbaya. Wakati Mfalme Suleimani alitaka kushiriki na wafu alienda kwa Mchawi wa Endori (1 Samueli 28:7 kuenda mbele) na ilkuwa jambo la siri na isiyo halali. Vyombo vya uchawi na watabiri na waganga walikuwa machukizo katika nchi ya Israeli. Wakati wafu wamekufa, wachana nao na usiwe na uhusiano yoyote nao. Juhudi za kuwasiliana na wafu zilikuwa na bado si ya kisheria kwa waaminiyo. Kushiriki pamoja na wafu ni aina ya ushirikina, sio ya kupendeza, safi, na jambo takatifu. Chochote isipokuwa tu. Maongezi kuhusu Yule aliyeuawa akifufuliwa kwa wafu ilisikika masikioni mwa watu wengi kama ya kutisha na chafu, kama ushirikina na uchawi.
Juu ya hii Paulo anasisitiza jambo la kinyume: Kristo alifufuliwa kwa wafu kupitia Roho wa utakatifu, sio roho wa giza ama roho uliochafuliwa, lakini Roho Yule wa Mungu mwenyewe ambaye ametiwa juu ya utukufu Wake wote. Hakuchafuliwa kwa kufufua Yesu. Ilikuwa jambo takatifu kulifanya. Ilikuwa hakika, vyema na safi na ya kupendeza na ya kutukuza Mungu, sio yao kudunisha Mungu. Ilikuwa takatifu.
2) Kupitia ufufuo huu Kristo “alifanywa [ama, aliteuliwa] Mwana wa Mungu mwenye uweza.”
Neno kuu hapa ni “kwa uweza.” Nafikiri NASB na KJV na RSV ni sawa kwa kuonyesha kuwa neno hili linathibitisha “Mwana wa Mungu.” Jambo sio kwamba Kristo hakuwa Mwana wa Mungu kabla ya ufufuo. Jambo ni kwamba wakati wa ufufuo Kristo aliacha kuwa Mwana wa Mungu katika kujidunisha na upungufu wa kibinadamu na udhaifu na kuwa Mwana wa Mungu mwenye uweza. Neno kuu ni “kwa uweza.”
Hili ndilo Yesu alimaanisha baada ya ufufuo aliposema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani” (Mathayo 28:18). Ndiyo Paulo alimaanisha katika 1 Wakorintho 15:25-26 wakati aliponena kumhusu Kristo aliyefufuka, “Kwa maana lazima Kristo atawale mpaka awe amewaweka adui zake wote chini ya miguu yake. Adui za mwisho atakayeangamizwa ni mauti.” Kwa mukhtadha mwingine, Yesu ni Mfalme wa Kimasiya. Anatawala sasa ulimwenguni kote. Anawaweka adui zake wote chini ya miguu yake. Kutafika siku moja ambapo atajitokeza kutoka kwa utawala wake usioonekana kwa utukufu unaoonekana na kujenga ufalme wake kwa wazi na kwa utukufu katika dunia. Paulo anamaanisha haya katika “Mwana wa Mungu mwenye uweza.” Anatawala sasa. Anatimiza lengo lake kupitia Roho Wake na kanisa lake. Na siku itafika wakati Kristo atashinda adui yeyote, na kila goti kitapigwa na kila ulimi utakiri kwamba Yeye ndiye Bwana kwa utukufu wa Mungu Baba (Wafilipi 2:11).
Hayo ndiyo yatakuwa hitimizo ya Injili ya Mungu. Ambayo tunayasemea, “Amen, kuja Bwana Yesu.”