Kujulikana tangu mwanzo, kuchaguliwa, kufanana na Kristo
Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi Lake. 29Maana wale Mungu aliowajua tangu mwanzo, pia aliwachagua tangu mwanzo, wapate kufanana na mfano wa Mwanawe, ili Yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 30Nao wale Mungu aliotangulia kuwachagua, akawaita, wale aliowaita pia akawahesabia haki, nao wale aliowahesabia haki, pia akawatukuza.
Tulitoa ujumbe tatu kutoka Warumi 8:28 (“Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi Lake."). Na tulisema kuwa Warumi 8:28 ilikuwa sehemu ya hoja ya Paulo katika Warumi 8:18, "Nayahesabu mateso yetu ya wakati huu kuwa si kitu kulinganisha na utukufu utakaodhihirishwa kwetu." Kwa maneno mengine, mateso yetu yote yaweza kuvumiliwa kwa sababu, kila kitu, hata haya mateso, yatafanya kazi pamoja kwa wema wetu.
Sasa tutaendelea kwa mstari inayofuata (29) ambayo huanza na "maana" ambayo ina maana ya "sababu." Tunaelekea misingi mikubwa wa Paulo — nguzo yake baada ya ahadi ya mstari wa 28 — ukweli ambao huishikilia isianguke — na kutuzuia kuanguka naye.
Alisema, Tunajua mambo yote — mambo machungu na matamu — yafanyika kwa ajili ya wema wetu (v. 28), "SABABU — huu ni fungu la 29, msingi wa ahadi huo — "Maana wale Mungu aliowajua tangu mwanzo, pia aliwachagua tangu mwanzo, wapate kufanana na mfano wa Mwanawe, ili Yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi." Hizi ndizo kazi tatu za Mungu ambayo tutazingatia asubuhi huu — vitendo vitatu vya Mungu ambavyo vinafanywa kwa ajili ya kukupa ujasiri zaidi kwamba yote yatafanyika pamoja kwa wema wako na mateso yote ya maisha haya haina thamani ikilinganishwa na utukufu utakaofunuliwa (8:17).
Matendo mitatu ya Mungu yanaonekana katika maneno, 1) "Kujulikana Tangu Mwanzo," 2) "Kuchaguliwa," na 3) "Kufanana na Kristo." Tunajua kwamba yote yatendeka pamoja kwa wema wetu kwa sababu Mungu alitujua tangu mwanzo, alituchagua [alituteua] na anatufananisha na Kristo. Mawili kati yao ni yamepita (kutujua tangu mwanzo na kututeua) na moja wao ni wa kisasa na ya yajayo (Kufanana na Kristo).
Hivi sasa ninaweza kuwaza angalau sababu mawili ambao baadhi yenu wanaweza kusema hamna maslahi na haya. Kwanza, baadhi yenu wanaweza kusema, "Kwa kusema ukweli, sishughuliki na maamuzi yaliyotolewa kitambo — kama kabla ya uumbaji katika kujua awali kwa Mungu na kuchaguliwa tangu asili. Nashughulikia leo. Nami, zaidi, sioni haja ya kushiriki katika migogoro kuhusu mafundisho ya Biblia kama kuchaguliwa tangu asili.”
Pili, baadhi yenu wanaweza kusema, “Kusema kweli, sitaki kuwa kama Kristo. Jambo moja, hakuwaifanya mapenzi, na, isitoshe alikuwa amemakinika sana usingedhani aliwai ona raha; na pia alikuwa mtatanishi hadi akauwawa. Hivyo ikiwa kukuwa kama Yesu yapasa kunifanya kuamini kwamba kila kitu iko sawa kwangu, sahau; maanake haifanyi."
Wacha niseme kitu kwa wanao hofu kuhusu hayo mambo mawili.
“Sishughuliki na maamuzi yaliyotolewa kitambo”
Mtu akija kwako asubuhi huu na akasema, "Nitakupa dola milioni," bila shaka una haki ya kuwa na tuhuma na mashaka. Na je, wakikuonyesha karatasi mzee iliyo kunjana na kusema, "Babangu tajiri alikufa miezi kadhaa iliyopita na aliandika katika wosia wake kwamba ungepokea sehemu ya urithi, dola milioni?" Utaweza sema, "Sishughuliki na maamuzi yaliyotolewa kitambo. Ninajali ya leo. Isitoshe kutatua maana ya hati za zamani, hasa wosia, zinaweza kuwa na utata! Kwa hivyo tu sahau tu hiyo dola milioni?" Nakuahidi, yale ambayo Mungu alijua tangu awali, na kuteua ni muhimu zaidi kwa maisha yako kuliko kurithi dola milioni.
“Sitaki kuwa kama Kristo”
Na ukisema, kusema kweli, sitaki kuwa kama Kristo,” inaweza kuwa ni kwa sababu unawaza kuhusu huu mfano wake, si kwa njia ambayo umepotoka tu, lakini pia ni nyembamba. Je, na vipi ukifa? Unataka kuwa kama Kristo ukifa: Unataka kukataliwa na Mwamuzi wa ulimwengu na kuhukumiwa katika ghadhabu wa milele, kwa sababu ulimkataa Mwanawe, au unataka kufufuka kutoka kwa wafu ukiwa umependwa na kukubaliwa? Unataka kufufuka kama Kristo au kama sio Kristo na kuangamia? Si swala ndogo. Na nikusihi usikize.
Hivyo basi tuangalieni matendo mawili ya Mungu yaliyofanyika kitambo awali, alafu tuangalie yale ambayo Mungu anayafanya leo na kesho.
“Kwa wale aliowajua tangu mwanzo”
Fungu la 29: “Maana wale Mungu aliowajua tangu mwanzo, pia aliwachagua tangu mwanzo, wapate kufanana na mfano wa Mwanawe.” “Kujua tangu mwanzo” ina maana gani? Wengine wameichukua kumaanisha kuwa Mungu huona mbele wenye watamwamini na kuwachagua kukuwa kama Yesu. Lakini hii ina sadiki mambo mawili ambayo si ya kweli. Kwanza ni kwamba imani ambayo Mungu huona mbele, hatimaye ni kazi yetu, si yake. Yaani, kiini cha tafsiri hii ni kwamba Mungu hasababishi imani yetu, yeye huona tu imani ambayo sisi husababisha.
Sasa hii sio kifundishwacho katika Biblia, si pengine (Wafilipi 1:29, Waefeso 2:8-9; 2 Timotheo 2:24-26, Mathayo 16:17), wala katika muktadha. Paulo anaposema katika Warumi 8:30, "Nao wale Mungu aliotangulia kuwachagua, akawaita, wale aliowaita pia akawahesabia haki," ana maanisha wote walioitwa wamehesabika haki. Lakini ili kuhesabika haki lazima tuamini (Warumi 5:1). Lakini ana wezaje kusema kwamba wote walioitwa wanaamini? Sababu, nilivyo jaribu kuonyesha katika ufafanuzi wa "kuitwa" katika fungu la 28, ni kwamba mwito ni kazi ya Mungu wenye nguvu ya kufanyisha madai yake. Ni mwito wenye ufanisi. Ni mwito unaojenga kile kinachoamrisha. Ni mwito kama "Lazaro, toka nje!" na aliye wafu huishi. Ukweli ni kwamba, kuamini kwa ajili ya haki si kitu fulani ambao mimi najifanyia kwa uweza wangu. Mungu ananiwezesha. Lazima niifanye. Kuamini ni kitu ninachofanya. Lakini kufanya kwangu ni zawadi ya Mungu. Sipokei sifa. Ninashukuru Mungu kwa ajili yake. Nimeokolewa na neema tukufu kutoka mwanzo hadi mwisho.
Hivyo ni kosa kudhani kwamba Warumi 8:29 inaposema, "Mungu aliwajua wengine tangu mwanzo" ina maana aliona tu mbele kwamba wangeamini kwa uwezo wao wenyewe. Alipeana huo uwezo, hivyo basi zaidi yatendeka hapa kushinda kuona tu mbele ya yale tufanyalo.
Huu ndio wazo mwingine potofu wa mtazamo huu. Inasadiki kwamba maana ya “kujua tangu mwanzo” si lile maana iliomo katika wengi wa maandishi za Agano la Kale na Agano Jipya ambazo zingepeana maana zilizoambatana zaidi na kifungu hiki.
Sikiza matumizi ya haya "jua" na ujiulize na ujiulize nini zinazomaanisha. Katika mwanzo 18:19 Mungu asema kuhusu Abrahamu, "Kwa maana nimemchagua yeye, ili kwamba aongoze watoto wake na jamaa yake kumtii BWANA." Karibu matoleo yote ya Kiingereza yanatafsiri hivi, "Nimemchagua." Katika Amos 3:2 Mungu anawaambia watu wa Israeli, "Ni ninyi tu niliowachagua kati ya jamaa zote za dunia." Alijua kuhusu familia zote, alichagua tu Israeli. Katika Matayo 7:23 Yesu aliwaambia wanafiki, siku ya hukumu, "Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!" Zaburi 1:6 inasema, “Kwa maana BWANA huziangalia njia za mwenye haki, bali njia ya mwovu itapotea.” Anajua njia za waovu pia. Lakini anajua njia za wenye haki kwa maana ya kuidhinisha ha kutambua na kupenda. Katika Hosea 13:5 Mungu asema kwa Israeli, "Niliwatunza huko jangwani, katika nchi yenye joto liunguzalo." kumaanisha aliona hatma yenu na kuwatunza. Na Mwanzo 4:1 inasema, Adamu akakutana kimwili na mkewe Eva, akapata mimba, akamzaa Kaini." Maanake, alimfanya wake, akamjua kwa undani na kumpenda.
Kwa sababu ya hayo maandiko yote ninadhani John Stott na John Murray wote wako sawa kwa kusema, "Kujua' . . . imetumika kwa maana sawa na "kupenda" . . . "ambao yeye alijua tangu mwanzo'. . . hivyo basi ni sawa na "ambao yeye alipenda tangu mwanzo." Kujua tangu mwanzo ni "upendo tukufu unaotofautisha" (John Stott, akimdondoa Murray, Warumi, kurasa wa 249). Ni sawa na kuweka mapenzi yako na kujichagulia mwenyewe.
Hivyo maana ya tendo la Mungu la kwanza katika Warumi 8:29 ni kwamba Mungu alijua watu wake tangu mwanzo maanake anawachagua na anawapenda na kuwashughulikia. Paulo ataongea kuhusu hayo baadaye kwa lugha ya "kuchagua" na "uteuzi" (Warumi 8:33; 9:11; 111:5, 7).
Yote yatatendeka pamoja kwa wema wako ikiwa umeitwa, na unampenda Mungu, maanake, ilivyo katika mstari 29, Mungu amekujua, na kukuchagua, na kukupenda, tangu kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu (Waefeso 1:4; 2 Timotheo 1:9; 1 Petro 1:20, Ufunuo 13:8, 17:8)
"Pia aliwachagua tangu mwanzo"
Tendo la Mungu la pili iliofanywa kitambo awali ili kuhakikisha chini ya ahadi kwamba yote hufanyikia Mungu wako ni kwamba “aliwachagua tangu mwanzo.” “Maana wale Mungu aliowajua tangu mwanzo, pia aliwachagua tangu mwanzo.” Hii ina maana ya kuwa, kwa kuwa alikuchaguwa kuwa wake na kuweka mapenzi yake kwako na kukushughulikia hata kabla ya kuwepo kwako, aliamua utakayokuwa, yaani, kubadilishwa kufanana na Mwanawe.
“Kuchagua tangu mwanzo” ina maanisha kuamuwa au kuamuru hapo awali hatima yako itakavyokuwa. Na sababu mstari huu unaweka Na sababu mstari huu unaweka msingi mkubwa katika ahadi ya Warumi 8:28 ni kwamba wale ambao wanampenda Mungu na wameitwa kulingana na ahadi yake hatimaye watakuwa kama Yesu — wapate kufanana na mfano wa Kristo. Yote yafanyika kwa wema wako kwa sababu ulichaguliwa na kupendwa kabla ya kuwepo kwako, na jinsi chagua na penzi lake inadhihirika yenyewe ni kwa kukuamuria wakati ujao ulio imara isiowezakutamkwa, yaani, kukuwa kama Kristo. Yote yafanyika kwa wema wako kwa sababu yote yatendeka kukufananisha na Yesu. Kwa maana hii ulipendwa, na kwa maana hii ulichaguliwa.
Hii ni fungu yenye thamani ya dola milioni katika wosia wa rafiki ya baba yako. Kama vile kifungo la sheria linakuhakikishia mali yako humu duniani, ndivyo kujua na kuchagua tangu mwanzo wa Mungu inakuhakikishia utukufu na furaha wa milele.
“Kutufananisha na mfano wa Mwanawe”
Ambao inatuelekeza hadi pingamizi zilizotajwa hapo mbeleni. Labda haitafurahisha ku kuwa kama Yesu. Labda ku kuwa kama Yesu haifanyi mateso yote ya wakati hu isikuwe na thamani ikilinganishwa na utukufu utakaofunuliwa. Hivyo tutaendela hadi tendo la Mungu la mwisho uliotajwa katika mstari wa 29: Mungu afanya kazi ili “tupate kufanana na mfano wa Mwanawe, ili Yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.”
Na kwa hayo tutangoja hadi wiki miwili yajayo kwa sababu mawili: mmoja, hamna wakati wa kutosha leo; na pili, kufanana na Kristo katika mstari wa 29 na kutukuzwa katika mwisho wa mstari wa 30 zimelinganishwa kwa karibu, zitakuwa mwanzo na mwisho wa ujumbe wa wiki ijayo.
Lakini wacha nifunge na maneno machache kuhusu kufanana na Kristo na maandiko ya leo. Ni muhimu sana kwa sababu hiyo. Hadi akili yako ifananishwe na ya Kristo, funzo kutoka katika nakala hii pengine utazalisha migogoro badala ya faraja. Nakala hii yapasa kukufariji na kukuimarisha na kupa tumaini kwamba mambo mabaya na mazuri katika maisha yako yatakuwa kwa ajili ya wema wako, kwa sabau unampenda Kristo na umechaguliwa na kuteuliwa kwa ajili ya utukufu. Lakini utadhihirika wakati Mungu atakupa kiasi cha akili na roho (nafsi) ya Kristo.
Sisemi haya ili kuwakemea au kuwahukumisha ikiwa mnapambana. Bali ni kinyume tu. Nasema haya ili kuwa changamsha kuwa vile kufanana na Kristo kitabia ni vita vya maisha dhidi ya matendo mabaya, ndivyo kufanana Kristo katika hisia zetu ni vita vya maisha dhidi ya hisia bovu, hivyo kufanana na Kristo, kitaaluma, ni vita vya maisha dhidi ya fikira bovu. Hivyo kamwe mimi sina shangaa wakati wengine wanajikwaza juu ya mafunzo magumu ya Maandiko. Ulinganishi na Kristo haiji zote tu mara mmoja, wala, kitabia, wala hisia, wala kitaaluma.
Kwa hivyo tuombiane, ili kwamba kwa kila njia Kristo atainuliwa tunapofananishwa naye, nasi tufurahie uhakika mkubwa kwamba kwa sababu ya kujulikana kwetu na uchaguzi wetu na kuteuliwa kwetu yote yatatendeka kwa wema wetu. Na ukiwa umekaa hapo ukishangaa: Niko kati ya waliochaguliwa, waliojulikana tangu mwanzo, walioitwa, hivi ndivyo jinsi utavyo weza kujua: Je, wamwona Yesu kama wa kumtamani zaidi ya vitu vyote, atosha kwa kukukomboa kutoka dhambini, na kuridhisha moyo wako milele? Huo ndio alama wa Mwana wa Mungu. yeye aliye na Mwana, anao uzima (1 Yohana 5:12). Kwa wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu (Yohana 1:12). Mpokee!